GS unampongeza raisi kwa lipi? goli la kuotea??Mheshimiwa Rais hongera kwa kutambua udhaifu wa watanzania na kuwa very smart katika kutumia udhaifu huo.
Mgaya hajamuangusha yeyote kwa kuahirisha mgomo. Tuseme TUCTA wametumia busara kufanya hivyo kwa sababu ingelikuwa ni loosing war. Nguvu ya raisi wa TZ inajulikana kikatiba na lolote ambalo lingetokea angekua na uwezo wa kuwatupia lawama TUCTA hivyo bora hiyo subira izidi kuwatia hasira watanzania ili siku wakisema mgomo na wawe tayari kwa hizo risasi za moto.
Kwa ile hotuba ya raisi tayari alishawagawa wafanyakazi na kumtwisha Mgaya mzigo kwamba yeye ndiye anashinikiza mgomo kwa kutumwa na wapinzani wa JK. Cha maana wafanyakazi tuzidi kushikamana na kuendeleza mapambano kwa njia zote, kelele, mahakama, vitisho na mkakati wa mgomo mwingine wenye ufanisi zaidi.