Huyu ndiye Nicholas Mgaya - Katibu Mkuu TUCTA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu ndiye Nicholas Mgaya - Katibu Mkuu TUCTA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, May 4, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  May 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Natambua kwamba wengi wetu tunamfahamu bwana huyu. Ni Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi TUCTA. Hivi Karibuni amjejizolea umaarufu baada ya kuonyesha ujasiri wa hali ya juu katika kutetea maslahi ya wafanyakazi wa Tanzania.

  Alionyesha ujasiri katika kupambana na serikali ilimardi masalahi ya Wafanyakazi yapatikane,aliwatia moyo wafanyakazi kwamba atahakikisha maslahi yao yanapatikana,ni mpaka kieleweke. Amejijengea imani kwa watanzania na hasa wafanyakzi na hivyo kupambwa katika Vyombo mbalimbali vya habari vya hapa nchini.. Aliweza kuwashawishi wafanyakazi mpaka wakafanya tukio la kihistoria la kuadhimisha siku ya Wafanyakazi bila kiongozi yeyote wa Serikali. Hebu soma hii moja ya editorial analysis ya gazeti la citizen la hivi karibuni likimpamba.

  Tanzanian workers need more - Nicholas Mgayas

  The Trade Union Congress of Tanzania (Tucta) deserves praise for its steadfast stand in fighting for the rights of Tanzania’s downtrodden workers.

  Also deserving special tribute is Tucta’s courageous and tenacious secretary-general, Nicholas Mgaya, who has been the public face of the workers’ body in its long-running dispute with the government over workers’ welfare.

  One needs to be as fearless and determined as Mgaya in fighting for workers’ rights.

  It’s rare to have a trade union official in a country such as Tanzania who can publicly declare that the President would not be welcome to the national May Day fete if workers’ grievances would not be addressed to the national body’s satisfaction.

  Tucta, under valiant leaders like Mgaya, refused to relent even under massive pressure from the government and other employers.

  The result is that the government has realised that Tucta means business, and that the nationwide strike scheduled for May 5 is no empty threat.

  Thanks to Tucta’s unwavering stand, the government has dropped its intransigence and promised to review the salaries of workers both in the public and private sectors before May 1.

  Workers would not have won these concessions from a hitherto indifferent government had it not been Tucta’s dogged tenacity.

  The government had all along appeared not ready to listen to Tucta until it dawned upon the powers that be that the workers’ body was not kidding.

  S.L. Manasse,
  Dar es Salaam.  Binafsi nilimuamini sana Mgaya na baada ya kuona wameadhimisha Mei Mosi bila viongozi wa serikali nikazidi kuwa na imani kuwa huenda kweli mgomo walioutangaza utafanyika; mwanzoni nilikuwa nina mashaka na mgomo huu kama kweli utafanyika.

  Leo nimeshangazwa sana baada ya kusikia eti TUCTA wamesitisha mgomo kwa muda. Natambua kwamba maneno ya Rais yalimtisha Mgaya akaamua kurudi nyuma. Rais was very clever and strategic alivyoamua kumshambulia Mgaya as if yeye ndio TUCTA pekee. Rais alitambua kabisa kwamba watanzania tu waoga na tunafuata mkumbo tu.

  Rais alitambua kuwa Mgaya ana ngvu za ajabu za kuweza kuamua mgomo ufanyike ama la kwakuwa alijua wafanyakazi wengi walikuwa hawajui kwanini wameamua kugoma bali wanafuata mkumbo tu. Ndio maana akawaambia akili za Mgaya mchanganye na za kwenu.Rais alithubutu kusema kwa umma wa watanzania kuwa Mgaya ametumwa. Strategy ya Rais imefanikiwa na hatimaye Mgaya karudi nyuma na kudni lake kwa madai kuwa wamesitisha mgomo kwa muda tu..

  Mgaya umewaangusha waliokuwa wana imani na wewe..

  Mheshimiwa Rais hongera kwa kutambua udhaifu wa watanzania na kuwa very smart katika kutumia udhaifu huo.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  GS - Nakubaliana nawe up to a certain point. Alichokifanya JK ni kuyasukuma matatizo ya umasikini wa Watanzania chini ya carpet tu ili yeye na serikali yake wapate ahueni ya muda mfupi. Viongozi hawa wa CCM wanaona hadi mwisho wa pua zao tuy, hawaoni mbali.

  Tukumbuke miaka miwili tu iliyopita akiwa Ufaransa alijitia aibu yeye na Watanzania wote kwa kusema eti hajui hata kwa nini Tanzania ina umasikini.

  Yatakayoikumba nchi kutokana na mtindo huu wa ku-sweep problems under the carpet unaweza kuingiza nchi katika janga kubwa baadaye. Na hii ndiyo sababu nchi nyingi za Bara la Afrika hutumbukika katika vita ya wenyerwe kwa wenyewe kwa sababu imekuwa infected na breed hii mbaya ya viongozi wasiojali kabisa wananchi wake.

  Lakini naamnini nchi hii itakuja kupata kiongozi mwadilifu. IKO SIKU!!!!
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  May 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0

  Nakubaliana na wewe Mkuu.Viongozi hawa wanafunika matatizo ya wananchi chini ya kapeti kwa kuwa wanajua sisi wenyewe tu waoga na wakifanya hivyo hakuna atakayewakataza,tutaishia kulalama bila kufanya vitendo..Na hili litatugharamu sana,uoga wetu..
   
 4. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Akili Mgaya huwei kabisa kufananisha na akili ya JK. Mgaya anachambua mambo JK anaongea kwa jazba huku akiishangiliwa na wapambe wake wa
   
 5. 2c2

  2c2 Member

  #5
  May 4, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  that is politics, if you know somebodies weakness you are the winner and you can make him/ her fall down easly and thats what is happening to tucta hawakuwa systematic walikuwa wanafanya mambo pasi kuangalia mbele, kama kweli walikuwa wanania ya kugoma terehe 5 wasingeafiki majadiliano ya tarehe 8, huu ni udhaifu mkubwa sana,
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  May 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ur extremely right Mkuu.
   
 7. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Kama ni weakness basi ni kwa Watanzania kwa ujumla kutokana na uoga wetu. Nafikiri Mgaya anatwishwa mzigo mkubwa kuliko anavyostahili katika sakata hili. He's just an individual - maybe a remarkable one. Ni aibu kwetu kukubaliana na kauli potofu, za kishabiki na zisizo na staha wala utu zilizotolewa na JK jana na kuziona kama mkakati mkubwa wa kisiasa. Alichofanya ni kunyanyasa ujinga, uoga na unyonge wa Watanzania wakiwakilishwa na "wazee wa DSM" waliokaa kihamnazo na kumshangilia bila uelewa makini wa kinachosemwa. Hiyo ni jeuri ya mmiliki wa vyombo vya dola asiyejali mustakabali wa nchi wala wa wananchi wake.
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi Mkuu.Hakuna nayemtisha mzigo Mgaya,soma between lines unanipata vizuri.Yeye ndiye kiongozi shupavu na jasiri tuliyetegemea angeongoza kile walichokisema kwamba watagoma ili kudai haki zao..Mheshimiwa Rais kamshambulia kaogopa kawithdraw lengo na wafanyakazi wasioviongozi TUCTA wakakubaliana naye kwa kuwa wengi wao ni waoga wanafanya kile wanachoambiwa na viongozi wao..Hivi walishindwa kugoma bila Mgaya?unafikiri ni kwanini Rais aliamua kumshambulia Mgaya?tafakari once again.
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Jamaa keshapata ujiko...haya atafte jimbo haraka uchaguzi ndo unakuja huo...!
   
 10. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Natofautiana na wewe. Ishu si uoga bali ni ukweli wa lile linalotaka kufanyika. Mie naomba nifaham CV za hawa watu wa TUCTA. Nami nawaona si wa kweli. Pamoja na watu wengi kujenga hoja kisiasa zaidi lakini lazima ufike wakati kila mmmoja wetu aseme ukweli hata kama unauma. Kuna concept ndogo tu ya kifedha hebu tuitumie then tukubalie.

  Kuna usemi unasema dhamana za sriakali zina attract interest ndogo kwa sababu serikali haiwezi kudefault. Ina maana kwamba serikali inaweza kuprint note za ziada na kulipa deni husika. Mf leo JK na serikali wangeamua kulipa mshahara wa TUCTA inamaana inflation ya hali ya juu ingehitokeza na hata hiyo pesa inayodaiwa isingekuwa na thamani tena.

  Kwahiyo madai ya mshara huo wa laki 3, takribani 300% increment hayaingii akilini. TUCTA walidai kisichowezekana. Ina maana hawana jopo la watu la kufanya tathmini ya madai yao badala ya kukimbilia kuandika madai kama hayo kwenye vyombo vya habari. Kwanini wasing'ang'anie kwenye inflation. Maana inflation kwa sasa ndiyo adui wa kipato cha mfanyakazi. Kwanini wasihakikishe serikali inachukua hatua kwenye kupanda ovyo kwa chakula na nyumba?

  Na kwanini wasidai kinachowezekana? Yaelekea hawa TUCTA hawajui collection ya serikali ni kiasi gani na wafanyakazi ni wapo wangapi?
   
 11. G

  Godwine JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  wapi tanzania inapoenda?
   
 12. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi nitatofautiana na wachagiaji wengi waliotangulia. Mgaya hakutangaza mgomo kwa matakwa yake binafsi bali kwa matakwa ya wafanyakazi kupitia vikao vyao husika. Na alikuwa na ujasiri wa kumfunga paka kengere kitu ambacho wengi wetu hatuna na wala hatuwezi. Tusikae kumlaumu Mgaya bali tujilaumu sisi kama watanzania wafanyakazi waoga tusioweza kusimamia haki zetu wenyewe mpaka Mgaya asimame jukwaani atushawishi. Ni nani kati yetu ambaye anaona serikali na vyombo vyake inatenda haki kwa wafanyakazi wa Tanzania? Ni nani anaweza kusema kwamba Kikwete ni mtu wa watu ambaye anawajali watanzania ktk shida zao zaidi ya propaganda zake za kwenda Muhimbili kuona wagonjwa huku akijua hawana hata panado?

  Watanzania tuache unafiki na ushabiki wa kijinga bila kunagalia mambo kwa kiina. Tulipaswa sisi wafanyakazi wa tanzania tone aibu kwa kushindwa kumpa msimamo wetu Mgaya ili mashambulizi aliyoshushiwa na Kikwete yasimtishe na asonge mbele tuko naye bega kwa bega.
   
 13. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,578
  Likes Received: 925
  Trophy Points: 280
  GS kwa kweli nakubaliana na wewe kabisa.Mgaya amekula ng'ombe mzima alafu kashindwa kumalizia mkia,what a shame!Kilichotakiwa ni kwamba jamaa angeendelea kukaza buti ukizingatia wafanyakazi walishakuwa katika MUNKARI wa mgomo toka siku ya Mei mosi.

  Ngoja tusimshambulie kwanza, tunaomba atueleze kilichosababisha asitishe mgomo kwa muda inawezekana kina mashiko kwa kiasi fulani.
   
 14. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mhh!.,huyu Mgaya amekuwa maarufu kweli, akigombea ubunge anaweza kupata huyu.
   
 15. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Napata uchungu sana kwa watanzania kuwa wajinga kiasi hicho.
  sasa tufanye nini,Mgaya ndio huyo karudi nyuma,Lakini namhakikishia Mgaya kuwa wafanyakazi wote Tanzania wamepata changamoto aliyoonyesha Mgaya mpaka hapa.
   
 16. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Acha kumpaka mgaya matope bwana bado ni Simba wa Yuda tu. Unadhani kwa siku moja hata wewe kuna mtu angeweza ku convince umati usimsikilize mkuu wa nchi? Kwanza angegoma na nani? pale alichofanya rais si kumtisha mgaya la hasha ni kutisha wengine wafanyakazi ambao wanatakiwa kugoma. Lakini Mgaya pale alipo anastahili sifa na pongezi hata kufanya ile temper ya rais kuonekana. Kwamba amekuwa mtu wa kwanza kupandisha munkari na hasira za rais mpaka akaongea unconsiously.
  Sasa ukianza kulemba hivyo mara vyombo vya habari vilimpamba na nini kwani chombo gani cha habari kimempaka matope kama sio wewe wa kwanza?
   
 17. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Chama cha walimu wenyewe kilikuwa cha mtoto .... kaka sifa yake mpe tu usimkatishe tamaa acha aende mbele hawa ni watu watakaotuletea mabadiliko
   
 18. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unajua nyie mnashindwa kuanalyse mambo vizuri, ukitaka kudai haki usikomoane na mtu. Mgaya alichofanya ndicho ambacho kila mtu mwenye akili angewaza kwanza kusubiri tarehe nane hiyo kwanza. Angefanya papara kaka mngegoma ? maana wagomaji ni nyie ati ... Sasa tarehe nane baada ya mazungumzo tutaona kitakachoendelea. Mpaka sasa mgaya amesababisha progress kubwa tu. Toka aanze mambo haya kuna mabadiliko yametokea na mengine yako njiani.
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Huyu ndo mbabe wa JK
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kwa nchi inayotawaliwa na USALAMA WA TAIFA usitegemee kutokea wazalendo wa kweli kwani wanazimwa kabla ya kufikia huo mlima wa uzalendo.

  Dawa ni Moja tu. Tujitolee kutoa elimu kwa kizazi chetu ili wakifika zama zao wasiwe kama sisi wenye hekima na heshima za uoga. Tuhesabu kwamba kizazi hiki hakina jipya kwa future ya Tanzania ila kizazi kijacho ndicho tukipe majukumu ya kusimamia nchi vyema. Tumeuzwa live lakini hatujauzwa milele, tumedanganywa live but hatujadanganywa milele. tutakufa na machungu yetu moyoni but tupande mioyo ya faraja, matarajio, misimamo thabiti na jitihada kwa kizazi kijacho.

  Kama hatutafanya hivyo naapa watanzania wataendelea kuchagua viongozi bomu kila ahsubuhi na kujutia jioni.
   
Loading...