MTEMI WA KIJANI
Member
- Mar 5, 2016
- 39
- 62
Pamoja na kwamba CCM ina hazina ya Vijana wengi wazuri lakini huyu kijana anafaa sana kupokea kijiti kutoka kwa Mwenyekiti wa sasa wa UVCCM taifa Juma Khamis Sadifa. Abel Magembe Lugimba ni kijana msomi mzalendo ambaye ana karama ya Uongozi, ana shahada ya kwanza ya Sayansi ya Elimu kutoka katika Chuo Kikuu cha St John-Dodoma,
Kwa ufupi ni mwalimu wa Sayansi kitaalamu ambaye amebobea kufundisha Biologia na Kemia.
Binafsi nimemfahamu huyu kijana tangia Mwaka 2014 nikiwa nasoma chuo kikuu cha Dodoma baada ya yeye kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM katika Chuo Kikuu cha St John.
Harakati za kisiasa ndizo zilizotukutanisha ndipo nilipoweza kufahamiana nae.Amekuwa mpambanaji mkubwa ndani ya CCM hususan katika Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu pamoja na UVCCM, Akiwa pale St john's university alifanikiwa kuisambaratisha CHADEMA katika Serikali ya wanafunzi ijulikanayo kama SOSJUT na kuiweka serikali ya wanafunzi inayoongozwa na CCCM.
Abel Magembe ni Kiongozi mwenye msimamo mkali katika mambo ya msingi, anachukia sana watu wa chini kuonewa, siku zote husimama na Wanyonge katika kupigania haki zao, pamoja na hayo kijana huyu anachukia sana rushwa na ufisadi.
Baada ya kuwa amehitimu Elimu yake ya Chuo Kikuu pale St John's University alirudi nyumbani kwao Mkoani Rukwa na kujitosa katika kinyang'anyiro cha UBUNGE katika jimbo la Kalambo katika kura za maoni ndani ya CCM ambapo pamoja na dhamira yake hiyo ya Kutaka kuwa Mbunge hakuweza kufanikiwa kupita yaani kura alizozipata hizikutosha kumuwezesha kupewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo hilo.
Abel Magembe ni Kijana ambaye huwa hakati tamaa, baada ya kuwa ameshindwa alikubaliana na Matokeo na kusonga mbele katika kuipigania CCM ili kuhakikisha inapata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 25/10 /2015.
Abel Magembe ni Kijana ambaye anauwezo mkubwa sana katika kujenga hoja chanya za kimaendeleo, Ujasiri wake mkubwa katika kutetea haki za watu wengine bila ubaguzi wowote ule na kusimamia haki ni mojawapo ya Vitu ambavyo vimekuwa vinanishawishi na kuona kuwa anafaa sana kuwa mrithi wa Mwenyekiti wa UVCCM taifa Ndg Juma Sadifa.
Katika awamu hii ya Hapa kazi tu inayoongozwa na Dkt Magufuli itafaa sana kama kijana huyu 2017 atapewa Uenyekiti wa UVCCM taifa ili amsaidie Rais Magufuli katika kuijenga upya CCM.
Kwa ninavyomfahamu Abel Magembe msimamo wake mkali dhidi ya Mafisadi wapiga dili hakika Rais wetu atakuwa amepata msaidizi makini katika utumbuaji wa majipu.
Mwisho, Ninawaomba Vijana wote WanaCCM muda utakapofika wa Uchaguzi mwakani Tumuunge mkono Abel Magembe Lugimba ili awe mwenyekiti wetu wa UVCCM taifa kama chama kitamteua kugombea nafasi hiyo. UVCCM mpya imara na mathubuti inawezekana chini ya abel Magembe Lugimba 2017.