Huyu ndiye mwanzilishi wa chama kipya cha Umoja Party (UP)

Naona dalili ya chama chenye sera makini na chenye uwezo wa kujenga hoja karibu sana muda kinaweza kuwa chama kikuu cha upinzani!
Tuliaminishwa watu wenye vipara huwa na busara na utajiri ndani yake,lkn kwa kupitia wewe naendelea kuamini kuwa akili ni nywele
 
NCCR ni chama mtoto wa ccm.
Yaani bila aibu unailinganisha nccr mtoto wa ccm na CDM ?
Ukapimwe mkojo wewe siyo bureeee
Marando,dk Ringo tenga labda tatizo ni Lyatonga Mrema hata Ccm c si ilimchukua Lowassa!
 
Disclaimer (Andiko hili ni kutoka clickhabari.com)

Imebaki miaka minne kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 nchini Tanzania. Chama kipya cha siasa kilijulikano kama Umoja Party (UP) kimeibuka kuomba usajili wa muda. Chama hicho tayari kimewasilisha maombi ya usajili wa muda ili kuanza kutafuta wadhamini kwa lengo la kupata usajili wa kudumu. Mwenyekiti wa chama hicho kitakachokuwa na makao makuu yake Dar es Salaam, Seif Maalim Seif amesema kuwa dira cha chama chake ni kuondoa umasikini Tanzania.

SEIF MAALIM SEIF NI NANI?
Mwaka 2020 Seif Maalim Seif aligombea nafasi ya urais kupita Chama cha Wakulima (Alliance for Africa Farmers Party). ambapo kupitia chama hicho mwaka 2020 Seif Maalim Seif alijipambanua kwa itikadi ya Uchumi wa Kilimo (Agricultural-based economy). Taarifa zinaonesha kuwa Seif Maalim Seif ana umri wa miaka 47. Seif anasema kuwa ni umoja pekee ndio unaweza kutatua matatizo ya nchi hii ndio maana Chama hicho kinaitwa Umoja.

Seif ni muumuni wa siasa za utulivu na kuleta mabadiliko kwa njia za majadiliano. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 aliwahi kunukuliwa akipinga vikali siasa za kusambaza maneno ya uchochezi ambayo yangehatarisha amani nchini. Seif alisema kuwa vyama vyote vina lengo moja la kuongoza dola, hivyo basi lazima vifanye siasa za kiungwana, pasi kuchochea vurugu kwani Tanzania ni moja na hakuna nyingine.

ITIKADI YA CHAMA CHA UMOJA
Chama cha Umoja kinajipambanua kiitikadi kuwa kinaazimia kutumia utajiri wa rasilimali uliopo Tanzania kunufaisha wananchi kwanza na kutatua tatizo kubwa la ajiri linalowakabili watanzania. Kupitia bendera yake yenye rangi nyeupe, nyeusi, dhahabu pamoja na kijani, Seif Maalim Seif amesema kuwa nyeupe ina maana ya amani, uwazi na upendo, na kijani ni rasimali za nchi yetu, nyeusi ni uafrika wetu pamoja na dhahabu ni tafsiri kuwa nchi ya Tanzania imebarikiwa rasilimali ya madini.

Naibu Msajili wa vyama vya siasa nchini, Sisy Nyahoza amethibitisha kuwapo kwa maombi ya usajili wa Chama hicho mezani kwake, na kwamba sheria ya vyama vya siasa inawataka kutangaza kwenye gazeti la Serikali na kutoa muda kwa wananchi pamoja na vyama vya siasa kupinga jina la chama kwa ofisi ya msajili. Baada ya mchakato huo kumalizika, hatua nyingine zitafuata kama sheria inavyoelekeza

Seif Maalim Seif si mgeni kwenye siasa za Tanzania, kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 Seif aligombea nafasi ya urais kupitia Chama cha Wakulima (AAFP)

View attachment 1997494

View attachment 1997495
JamiiForums330662192.jpg
 
Kadawi Limbu alianzisha CCK , baadaye akaanzisha ACT lakini mwishowe akahamia ccm

Sio akahamia ccm, bali akarudi ccm, maana hakuwahi kuondoka bali alikuwa anatumika kwa shughuli maalum. Hiki chama nilianza kukisikia toka enzi za Magufuli, kulikuwa kianzishwe kwa lengo la kuipiku CDM baada ya Magufuli kutokuikubali ACT kwa ajili ya Zito. Chenyewe kitakuwa kinafanya upinzani unaotakiwa na CCM, ndio maana unasikia wanasema watafanya siasa za majadiliano!
 
Aiseeh! Hii nchi hii, inaongozwa na chama kisichojiamini, Pamoja na kuwasweka ndani na kuwaziba midomo wapinzani bado mna mbinu zile zile za karne ya 19 ya kulundika Vyama watoto!

Huyo jamaa huyo kwa kumuangalia TU hayuko smart kisiasa, yupo yupo TU Kama mpiga dili kwa mgongo wa chama huku akibebelewa kwenye mbelezo ya CCM!
Ni Matangulizi tuu, wenye njia wapo kutoka kwenye vyama vyote hasa Ccm na chadema walipkubaliana na mwelekeo wa Mwamba, na wengi wao ni vigogo haswaaa na wasomi wandamizi kutoka serikalini na vijana wengi walioko mavyuoni walimkubali mwamba wa Africa
 
Aiseeh! Hii nchi hii, inaongozwa na chama kisichojiamini, Pamoja na kuwasweka ndani na kuwaziba midomo wapinzani bado mna mbinu zile zile za karne ya 19 ya kulundika Vyama watoto!

Huyo jamaa huyo kwa kumuangalia TU hayuko smart kisiasa, yupo yupo TU Kama mpiga dili kwa mgongo wa chama huku akibebelewa kwenye mbelezo ya CCM!
Huyo jamaa ukimuangalia unaona tumbo la njaa na ubongo uliooza kwa njaa.
 
Back
Top Bottom