Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha

Discussion in 'Celebrities Forum' started by fakenology, Jan 13, 2014.

 1. fakenology

  fakenology JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2014
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 763
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  [​IMG]
  Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi.

  Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.

  [​IMG]
  Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''

  Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

  [​IMG]
  Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

  Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.

  Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

  [​IMG]
  Watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

  Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

  [​IMG]

  Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi

  Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.


  [TABLE]
  [TR]
  [TD][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.

  Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

  Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

  kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.

  Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.

   
 2. K

  KAGAMEE JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2014
  Joined: Dec 20, 2013
  Messages: 460
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Very good to learn
   
 3. warumi

  warumi JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2015
  Joined: May 6, 2013
  Messages: 13,377
  Likes Received: 4,064
  Trophy Points: 280
  dah aiseh, jamaa anaweza sana, alivaa uhusika vilivyo, mpaka kesho najua kwel yule ndo yesu original, sasa sijui na yeye atakufa au la..maana kaponya wengi sana aiseh
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Apr 29, 2015
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,676
  Likes Received: 2,613
  Trophy Points: 280
  jesus.jpg


  Si nia yangu kujadili katika mlengo huu, bali kujifunza na kuielewa dunia ilikotoka na iendako, katika machapisho mengi ya kiroho hasa ya kikristu hutumia picha ya Brian Robert Deacon inayofahamika kuwa ni ya Yesu Kristu wa Nazareti, lakini upembuzi wangu umebaini kuwa Anaitwa Brian Deacon, a
  mezaliwa 13 February 1949 Huko Oxford Uingereza, Baba yake anaitwa Robert Thomas Deacon ambae aitaalamu alikuwa faundi magari, Mama yake anaitwa Eileen Mary ambaye alikuwa Nesi, Brian Deacon ni Mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yao, Brian Deacon alioa mke wa kwanza mwaka 1977 aitwae Rula Lenska ambae amezaa nae mtoto mmoja aitwae Lara Brian Deacon, Lakini Mwaka 1982 mkewe alimtuhumu mumewe kutembea nje ya ndoa na ndoa yao kuvunjika, Alikaa miaka 16 na Hawara yake Cecy Redknap mpenzi wake wa muda mrefu, Mwaka 1998 alioa kke mwingine aitwaye Natalie Block ambaye mpaka leo wako pamoja,

  Msanii Brian Deacon alipata tenda ya kuigiza katika Filamu kama YESU, Filamu alizowahi kushiriki ni A - Zed & Two Nought Mwaka 1985, Feather Seapent Mwaka 1976, Lillie Mwaka 1978 Na nk, Wakristo Sura Deacona huyu Msanii wanaitumia katika maombi yao mbele za Mungu kama sura ya YESU Mnazareti, Pia katika Makanisani Wameweka sura yake ikiwakilisha uwepo wa Yesu.
   
 5. J

  Jenerali Ambamba JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2015
  Joined: Sep 8, 2014
  Messages: 3,301
  Likes Received: 961
  Trophy Points: 280
  Ok..nimeelewa
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2015
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,877
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Yupo "Yesu mwingine" anaitwa Meil Gibson alicheza picha ya The Passion of Jesus Christ!

  Meil Gibson anafanana sana na Yesu wa Nazareti. Mwaka jana alikuja Bongo na kila alipokwenda alifuatwa na makundi ya makubwa ya watu wakimuita na kumfananisha na Yesu wa Nazareti.

  Baada ya kumaliza kucheza The Passion of Jesus Christ, Meil Gibson aliokoka na sasa anasambaza neno la Mungu.

  Wakati wanacheza picha ya the Passion of Jesus Christ huko Israel/Palestine, kuna wakati waigizaji waligoma. Basi Director wa movie akamwambia Meil Gibson, Wewe Yesu hebu kaongee na wafuasi wako wamegoma. "Yesu" baada ya kuongea na wafuasi wake wakaacha mgomo na kuendelea ku act hiyo picha.
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 23,756
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Jibu makini sana...bahati mbaya walio wa mwovu hawawezi anzia fikra hapo.
   
 8. ISLETS

  ISLETS JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2015
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 4,515
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  sasa mbona unarudia tu yaleyale yaliyojadiliwa humu.. .. au hoja yako ni ni ipi mkuu
   
 9. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2015
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 14,527
  Likes Received: 2,614
  Trophy Points: 280
  Huyu wako atakuwa feki make mie toka mdogo kichwa na akiri yote imemkubali mkubwa Deacon kwa kila kitu
   
 10. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2015
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,129
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Yeriko wewe Yesu wako unayemwabudu ni yupi kati ya Deacon na huyo uliyemweka leo, hakika mtafanya imagination nyingi lakini hakuna sura Yesu kati ya hao wawili.
   
 11. Econometrician

  Econometrician JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2015
  Joined: Oct 25, 2013
  Messages: 7,069
  Likes Received: 5,215
  Trophy Points: 280
  Je kabla huyo bria ajaigiza kama yesu kulikuwa na picha ya yesu? Tafadhali naomba jibu kwa anaye fahamu
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 23,756
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Zilikuwepo nyingi tuu...na movie nyingi tuu zilitengenezwa...ila kila movie ilitengenezwa kwa kutegemea simulizi za INJILI KM ILIVYOADIKWA NA NANI.Kuna picture ziishchorwa na kuna picture iliyopigwa ktk zulia wanaloamini lilikuwa sanda Yake na kuleta picture km hiyo.
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 23,756
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Actor mwingine haimaanishi ni character mwingine....kwanini usiwe serious ktk hilo.Nelson Mandela ataactiwa na watu wengi sana...ila historical Mandela atabaki yule yule.Najua ni rahisi sana nyie kufanya mizaha.Ila ulimwengu wa roho hauna mizaha kihivyo....
   
 14. k

  kenny the smart mind Member

  #14
  Apr 30, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  List of books in the Orthodox
  Tewahedo Bible
  Old Testament
  1. Genesis
  2. Exodus
  3. Leviticus
  4. Numbers
  5. Deuteronomy
  6. Joshua
  7. Judges
  8. Ruth
  9. I and II Samuel
  10. I and II Kings
  11. I Chronicles
  12. II Chronicles (incl. the Prayer of
  Manasseh )
  13. Jubilees
  14. Enoch
  15. Ezra-Nehemiah
  16. Ezra (2nd) and Ezra Sutuel
  17. Tobit
  18. Judith
  19. Esther
  20. I, II and III Meqabyan (Similarly
  named, but not the same as the four Greek
  Books of the Maccabees. )
  21. Job
  22. Psalms
  23. Messalë ( Proverbs ch 1–24)
  24. Tägsas ("Reproof"; Proverbs ch 25–31)
  25. Wisdom of Solomon
  26. Ecclesiastes
  27. Song of Songs
  28. Isaiah
  29. Jeremiah (incl. Lamentations , Letter of
  Jeremiah , Baruch and 4 Baruch)
  30. Ezekiel
  31. Daniel
  32. Hosea
  33. Amos
  34. Micah
  35. Joel
  36. Obadiah
  37. Jonah
  38. Nahum (or Nahium)
  39. Habakkuk
  40. Zephaniah
  41. Haggai
  42. Zechariah
  43. Malachi
  44. Sirach
  45. Josippon

  New Testament
  1. Matthew
  2. Mark
  3. Luke
  4. John
  5. Acts of the Apostles
  6. Romans
  7. I Corinthians
  8. II Corinthians
  9. Galatians
  10. Ephesians
  11. Philippians
  12. Colossians
  13. I Thessalonians
  14. II Thessalonians
  15. I Timothy
  16. II Timothy
  17. Titus
  18. Philemon
  19. Hebrews
  20. I Peter
  21. II Peter
  22. I John
  23. II John
  24. III John
  25. James
  26. Jude
  27. Revelation
  28. Ser`atä Seyon (30 canons)
  29. Te'ezaz (71 canons)
  30. Gessew (56 canons)
  31. Abtelis (81 canons)
  32. I Covenant
  33. II Covenant
  34. Ethiopic Clement
  35. Ethiopic Didascalia

  Wanajukwaa naomba niulize na kama kunamtu mwenye jibu sahihi tafadhali anifahamishe. Mtiririko huo hapo juu ni vitabu katika bibilia ya Ethiopia kinachonipa shida mm ni hivyo vitabu vingine ambavyo havipo kwenye bibilia nyingine zote isipo kuwa ya Ethiopia tu.
  Swali?..
  Ina maana hakuna tafsiri ya hivi vitabu au hapa iko vp?
  Mdau yoyote mwenye kufahamu kuhusu hili naomba anijuze
   

  Attached Files:

 15. k

  kenny the smart mind Member

  #15
  Apr 30, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na kuna madai mengi kuwa bibilia inabadilishwa kila baada ya miaka kadhaa ukichukua bibilia ya zamani kidogo na ya Sasa kuna Baadhi ya mistari inapishana je na huu ni ukweli?..
  Maandishi ya mwanzo kbs ya biblia yapo sehemu gani hasa au ni yapi hasa
   
 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 23,756
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Ethopia walikuwa central ktk kuibuka kwa dini za kiyahudi,kikristu na hata uislam,walideal na mitume wao directly.....lugha yao haijabadilika sana tangu zamani kwa hiyo choice ao ya vitabu ktk Biblia yao itakuwa yao zaidi kwani Kanisa lao pia lina Mamlaka tofauti pia.Tafrisi inaweza kuwepo ya lugha nyingine,ila Kiswahili tunaweza kuwa na shida kwani hatuna vyombo bora vyenye resources ktk kutafrisi.Pia ingekuwa nao wana uwezo wangeweza shawishika kutafsiri ili wakaendeze...Abyssinia hiyo..ni mojawapo ya mataifa yatakayokuwa katikati ya vita za dunia za kidini..na vita za kidunia kati ya shetani na watu wa Mungu.
   
 17. k

  kenny the smart mind Member

  #17
  May 1, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante Kwa majibu mazuri. Sema kama hivi vitabu vitakuwa katika tafsiri ya lugha chache basi kunautata mkubwa kuhusu real Hebrew, au Ten lost tribes of Israel.
  Nasema haya nikiwa na wasiwasi kwasababu kuna mambo yanayoendelea katika Baadhi ya vyuo vya historia pande zote za DUNIA kuwa wale wanaojiita Hebrew, Jews sio kabisa maana ukiwaambia WA prove kuwa ni real hebrews or real Jewish people hawawezi kutokana kwenye historia hawajatajwa. Nikimaanisha hebrews na Jews [wakizungu] wanashindwa kudhibitisha kuwa hao ndio real walikuwa ktk historia ya kale. Ila Kwa sisi watu weusi na waindi tunaweza kudhibitisha.
   
 18. k

  kenny the smart mind Member

  #18
  May 1, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu ni real Hebrew mchanganyiko WA black na india
   

  Attached Files:

 19. k

  kenny the smart mind Member

  #19
  May 1, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu ni fake nikihusianisha na Mambo ya walawi 19:27
   

  Attached Files:

 20. Mr Q

  Mr Q JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2015
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 4,192
  Likes Received: 3,630
  Trophy Points: 280
  kwahiyo kuna uwezekano mkubwa kwamba dini hetu inatupotosha?
   
Loading...