Huyu ndiye mtoto wa miaka 14 wa kitanzania anayetengeneza application za simu na kuwauzia nokia

englibertm

JF-Expert Member
May 1, 2009
9,253
6,207
IMG_2016.JPG

Alvin Walter Makundi ni kijana mdogo wa Kitanzania anayeishi na wazazi wake nchini Singapore. Akiwa na umri wa miaka 14 na mwanafunzi wa kidato cha pili huko Singapore, tayari ameshatumbukiza jina lake katika orodha ya wataalamu wa application katika moja ya makampuni makubwa duniani ya kutengeneza simu za mkononi ya NOKIA, ambapo anatengeneza applications ambazo anazituma katika kampuni hiyo ambayo nayo bila hiana huitumia.
 
Kumbe ni mtanzania anayeishi singapore? Nilidhani anaishi huku kwetu kweditilibe. Hakuna cha ajabu hapo. Mbona Obama ni mkenya lakini ni rais wa marekani.
 
Mbona wapo wengi wenye uwezo hapa Bongo!! tatizo ni mazingira ya kuonyesha uwezo wao na kupata support kutoka kwenye finance institutions.
 
Kama wakitengeneza magobole tuu mnataka kuwafunga jela

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Rais wako ndo kila kitu kwake ni ajabu ndo maana mpaka leo hajachoka kuzunguka na dunia
 
watz tupo safi hila mazingira ya hapa bongo sio mazuri kwa kukuza vipaji. Vijana wangapi tumesomanao walikuwa noma hila leo wako wapi? Watz wanaamua kuamia nchi za nje kwasababu mazingira ya kule nimazuri ktk kukuza vipaji. Embu tubadilike watz kwani nchi yetu itajengwa na sisi wenyewe na wala sio WAWEKEZAJI WA KUTOKA NJE.
 
Hongera bwamdogo Makundi jr. Tatizo la Watanzania cc bado ni pale pale, hatutaki kuukubali ukweli pale kwenye ukweli. Bwamdogo ni mkaree, kaka zake hapa bongo wana degree za computer science lakini hawana hata program mmoja ambayo wanaweza ipresent mahali kazi kulalamika tu.
Tengeneza hata kidata base kimoja umuuzie jirani yako mwenye ka super mrkt basi, ooo serikali, hata kwenye hili jamani? Makofi jamani kwa Waaaaaaaalter Makundiiiii.
 
Kumbe ni mtanzania anayeishi singapore? Nilidhani anaishi huku kwetu kweditilibe. Hakuna cha ajabu hapo. Mbona Obama ni mkenya lakini ni rais wa marekani.

Pengine ungeambiwa anauza madawa basi ungemkubali haraka!
 
Mbona wapo wengi wenye uwezo hapa Bongo!! tatizo ni mazingira ya kuonyesha uwezo wao na kupata support kutoka kwenye finance institutions.

Hizi ndo siasa za kitanzania za kujisifu na kuleta visingizio vya mbaazi!Kama yupo mwenye uwezo kampuni zitamtafuta tuu!Ila kwa elimu yetu ya 7x2=15 usitarajie kupata watu kama hao waandishi wa vitabu wenyewe ndo kina kambare Nyangumi bado unajidanganya eti hapa pia wapo?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kwa kiongozi makini angepata changamoto kutengeneza mazingira mazuri ya kuwarudisha watalaam wote watanzania walioko nje kuujenga mataifa mengine waje wasaidie kujenga taifa lao, lkn kwa huyu wetu sijui kama hilo lipo vichwani hata si yeye wala washauri wake!
 
Huyo kwa vile yupo sehemu yenye fursa ndio maana ametimiza ndoto na kipaji kimeonekana Ila labda tu nimwambie Mr president kua watoto wa aina hii wapo nchini na anaweza kuwapa mkono hapa hapa nchini kama atahamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa kwa watanzania kuhakikisha maisha bora yanapatikana kwa kuimarisha mambo ya msingi yanakua sawa lakini kwa chenga yake ya shule zaidi kata amechelewa sana kupanga kufika hapo
 
Tanzania hakuna utamaduni wa kudhamini chetu.
Kuna watu hapa USA ni wakufunzi wa vyuo vikuu wakiondoka katika vyuio hivyo kozi nzima inafutwa.
Ni vipanga hodari wa kutupwa.
Lakini serikali ya CCM inawaona mavi ya kunuka, hata wakija hapa wanashindwa kuongea nao.
Nchi nyingine serikali zingewafanya member wa faculties za vyuo vyake.

Tanzania ukigani mashairi ya kuisifu CCM hata Rais wa nchi anaweza kuairisha safari ya nje asikilize shairi lako.

Udakitari uinjinia na uana sayansi umebuyamiwa matacko na serikali ya CCM
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom