Huyu ndiye mtoto wa kwanza wa baba wa Taifa Mwalimu Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu ndiye mtoto wa kwanza wa baba wa Taifa Mwalimu Nyerere

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwitongo, May 19, 2012.

 1. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Nimeona mjadala mkali unaomhusu Andrew Nyerere. Wapo wanaomkejeli kwa jina lake, na wengine wanamzushia tu mambo.

  Nimeona nieleze haya machache...

  Andrew Nyerere ndiye first born wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Burito. Jina lake la kuzaliwa ni Burito.

  Burito ni babu yake Mwalimu Julius Nyerere.

  Andrew ana wadogo zake. Mtiririko wao wa kuzaliwa ni Anna Watiku, Emil Magige, John-Guido Nyerere, Charles Makongoro, Godfrey Madaraka, Rosemary na Pauleta.

  Nimeona nitoe elimu hii fupi nikiamini kuwa katika JF suala la kuelimishana limepewa umuhimu mkubwa.

  Kama lipo swali, nawakaribisha.

  Asanteni sana.
   
 2. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  yule aliyekufa kwenye ajali ya ndege kipindi cha vita ya idd amin alikuwa akiitwa nani?
  je nikweli mwalimu alikuwa anavuta ile sigara kubwa na baadae akaanza kuvuta sigara za kawaida kabla ya kuacha kabisa?
  je nikweli wazanaki wakishirikiana na mwalimu nyerere ndo walio tunga kanuni za tanu na kuziandika kwenye mawe ya mwisenga ili wazungu wasigundue kabla ya uhuru?
   
 3. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna mtoto wa mwalimu aliyefariki katika ajali ya ndege wakati wa vita. Andrew alikuwa Fighter pilot kama alivyokuwa mdogo wake, John. Makongoro alikuwa mtaalamu wa mizinga. Wakati wa vita Makongoro alipigana mstari wa mbele. Kwa kifupi niseme hakuna mtoto wa mwalimu aliyekwishafariki, iwe vitani au kwa namna nyingine. Wote wakingali hai. Mwalimu alikuwa mvuta sigara, na aliacha baada ya Uhuru. Hakuna kumbukumbu za yeye kuvuta siga kubwa! Kuhusu hilo la katiba ya Tanu ni kweli, lakini aliandika katika pango kule Ikizu.

  Nawasilisha
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Big up brothers....! Watoto wa mpigania uhuru ni wanajeshi wa ukweli...!
   
 5. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli kabla ya uhuru Mwl Nyerere alikwenda Bagamoyo kuombewa na Sheakh Ramia na waislam wengine?

  Kuna tetesi alilala makaburini uko Kaole je tetesi hizi ni za kweli?

  Mwl Nyerere alipokuwa alipoanza kuumwa serikali ya Mkapa ili mchelewesha kumuwaisha hospital mpaka alipozidiwa na kumpeleka kwa mahsimu wake waingereza Je kuna ukweli gani kuh hili?

  Hivi kwa nini kukiwa na mjdala unaomuhusu Mwl serikali inaogopa na kusema uko ni kuhatarisha usalama wa taifa nini maana ya hili?
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,605
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwitongo, asante kwa taarifa hii.
  Naomba sasa ututajie mmoja baada ya mwingine, wako wapi na wanafanya nini?.
  Baba wa taifa alipokuwa hai, ni kweli alizuia vile viwanja pale mbele ya Msasani vibaki open space lakini baada ya kifo, amepuuzwa?. Jee ni kweli alipokuwa hai, Mwalimu alizuia yale makazi ya squater pale jirani yake Msasani yabakie ili aishi na watu wa kawaida ila baada ya kufariki wamefukuzwa na sasa makakazi yake yamezungukwa na majumba, hadi nyumba yake ilitokuwa jumba wakati ule sasa ni kijumba tuu?.
   
 7. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli watoto wa Mwalimu wapo na kila mmoja ana shughuli zake. Andrew na John wapo Msasani. Emil, Madaraka, Makongoro na Rosemary wapo Butiama. Anna Watiku yupo Tarime. Wana shughuli za kawaida kama watanzania waungwana wengine.

  Mwalimu akiwa hai alizuia bonde lote kuanzia pale kwake pasijengwe. Hoja yake ilikuwa kwamba kukibaki na uhalisia wake, kutasaidia kuchuja hewa na kuweka mandhari katika uhalisia wake. Pia aliamini kuwa bonde lile ni mkondo bahari ambao unakuwa na maana sana wakati wa majanga kama ya tsunami na mengine. Pia kulikuwa na viwanja vya ndugu zetu wamakonde kukutana kila wikendi na kuburudika kwa ngoma.

  Kuhusu wane wananchi waliokuwa katika kijiji cha butiama-Msasani, wengi waliponzwa na tamaa ya fedha. Mwalimu waliwatetea kwa kuzuia kina KItwana Kondo kuwapoka maeneo yao, lakini kwa njaa zao, baada ya mwalimu kufariki dunia wakauza kwa bei ya kutupa. Wengi wamekufa kwa kihoro, maana wapo waliouza kiwanja hadi kwa sh milioni mbili. Walitapeliwa sana na yule Rwegarisa (Silent Inn) ambaye sasa anajifanya mtu wa Mungu.

  Kama kuna swali, lete
   
 8. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sorry, nilimaanisha Rwegasira!
   
 9. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Vipi mkuu Mwitongo na wewe ni wa ukoo wa Nyerere?
   
 10. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu, mimi si wa ukoo huo, lakini nimekuwa karibu nao kwa sababu napenda sana kuyajua mengi kuhusu ukoo wa Nyerere Burito.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jamani kuna mjeda alipigana vita ya kagera kasema yule aliyekuwa pilot alifariki baada ya ndege yake kutunguliwa.
  Ivi ni kweli mzee alinunua hisa TATA?
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,605
  Trophy Points: 280
  Naomba ufafanuzi wa hili, ni kweli?. Jee maandiko hayo kwenye hilo pango bado yapo?. Jee aliyeandika ni Mwalimu mwenyewe au aliwaelekeza waashi ndio wayaandike?. Na kama aliyaandika yeye Mwalimu, jee aliyatunga yeye au ni sehemu za mapokeo ya Kizanaki kama "manza nganyanza"!.
   
 13. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwitongo , binafsi nakushukuru kwa taarifa hii, umetoa somo zuri. mm sina swali!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mie bado siamini hii taarifa yako mpaka Rais mstaafu Benjamin Mkapa adhibitishe.
  Unless Mkapa adhibitishe hii habari yako itakuwa na walakini mkubwa sana
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,279
  Trophy Points: 280
  Mwitongo Mwe!!.... nilidhani Che Nkapa yuko peke yake anayejuwa Familia za watu kuliko Familia yake kumbe na hata huyu Mwitongo naye yupo kama Mkapa?

  Haya sasa twende, Taratibu, kwanza ningependa kujuwa kama wewe umeteuliwa kuwa msemaji rasmi wa Familia ya Baba wa Taifa? Pili swala la Andrew Nyerere kuwa First born wa Baba wa Taifa alishalisema yeye mwenyewe hapa hapa JF na hakuna jipya hapa unalotueleza.

  Kuhusu unachosema kushambuliwa hapo mimi ndio nazidi kukushangaa, hivi inawezekana vipi thread hujaanzisha wewe halafu unawaomba Admin/mods eti wafute post zako!!....ina maana siku hizi hapa JF hakuna access ya mtu kufuta yeye mwenyewe post zake kama anaona kuna ulazima huo!! am just curious

  Hivi inaingia akili thread ya miaka 3 iliyopita ndio mtu aje kusema leo kwamba yale aliyoyasema hayakuwa sahihi!! suspension number 1, Ganesh ndiyo Andrew Nyerere na watuhumiwa ni Jeetu Patel na ndugu yake, je hujacconect dots hapa bado!!?? ni kwa nini mswahili alikuwa na Mahaba ya kutumia jina la kihindi na kujiita Ganesh?

  Kinachoshangaza na kusikitisha taarifa za Andrew kukanusha kile alichokisema kimetkea siku chache tu baada ya yeye kuwa Verified user. Tusifanyane watoto wadogo hapa.

  Mwisho kwa kuwa unaijuwa vizuri Familia ya Nyerere ningependa utujurishe Nyerere alikuwa na wake wangapi? nadhani unazifahamu vyema mila za kizanaki.
   
 16. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  mwl alikuwa na watoto ambao ajazaa na maria?
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,605
  Trophy Points: 280
  Naomba utueleze zaidi kuhusu watoto wa Chief Burito. Inasemekana Julius Kambarage, Joseph Kisurira na John Kiboko ni watoto wa mama mmoja. Ila baba yao alikuwa na wake wengi. Jee alikuwa na wake wangapi?. Jee ndugu wengine wa Nyerere kwa baba mmoja ni wangapi na wanaitwa kina nani ukiondoa hao ndugu wa tumbo moja wanaotumia majina ya JK Nyerere?.
   
 18. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Na vipi kuhusu kuwa kuna wakati Mwalimu alitaka kuachana na Mama Maria sababu alihisi kutumiwa kumfitini kisiasa,akamrudisha kijijini Butiama mpaka Muadhama Kardinal Rugambwa alipowapatanisha..!??
   
 19. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Swali gumu nini?
   
 20. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Chifu Nyerere Burito ambaye ni babake Mwalimu, alikuwa na wake 26. Mamake Mwalimu aliitwa Mgaya Nyang'ombe. Huyu alikuwa mke wa tano. Mwalimu alikuwa na ndugu zengine kwa babake, baadhi yao ni Justine Nyerere, Wisigana, Joseph Muhunda,Jackton, Wanzagi, Mukami, Tagazi, Nyasisenye, Daniel, na wengine wengi sana. Fikiria wanawake 26 si mchezo!!
   
Loading...