Huyu Ndiye Mohamed O. Mchengerwa

In fact LL.B alisoma Kampala University ya Uganda campus 2003-2006 kule ni miaka mitatu tu. Then LLM alipiga UDSM
Malangali alisoma mwaka gani mkuu? Ikiwezekana na mwaka aliosoma na kumaliza Makerere pia uweke
 
Kaona mbona watu hawanijui ngoja nijiuze hongera sana Mh Mchengerwa....hakika ni hazina ya baadae jifunze siasa za staha utafika mbali
Japo si mimi ila pengine salam atazipata.
Thanks mkuu 🙏🙏🙏
 
Yani unakaa kabisa unajiaminisha Waziri mzima wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi na Utawala Bora akae na apate muda wa kuandika humu JF kweli kwa hizi siku mbili walivyowekwa busy mzee????? Ni sisi wenye mudanwa haya wao saa hii ofisi za Moto sana .
🙏🙏🙏 hata mimi nashangaa kusemwa eti huyo ni mimi.
Dah!!!
 
Huyu Ndiye Mohamed O. Mchengelwa

Teuzi Mpya za Baraza la la Mawaziri zimemuibua kijana Mzalendo na Mchapakazi Mohamed Omar Mchengelwa.
Mh.Mchengelwa ni Mbunge wa Rufiji toka 2015 akichukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Afya wakati wa Mzee JK Dr Seif Rashid.
Mh.Mchengelwa ni Mwanasheria msomi na bobezi katika eneo la Mahakama alikofanya kazi kabla ya kuwa Mbunge.

Mchengelwa Ni Mwanafunzi wa Shahada ya Tatu (PhD) katika Siasa na Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu Cha "Girne America University" nchini Cyprus.

Ukiacha hayo amekuwa Msaidizi wa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa miaka sita(2009-2015).

Bungeni kwa muda mrefu amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria mpaka wakati huu Mh.Raisi anamteuwa kuwa Waziri.

Mh.Mchengelwa ni miongoni mwa Wabunge wenye kujenga hoja zenye maslahi makubwa kwa wananchi ya Jimbo la Rufiji na Tanzania kwa Ujumla.

Mfano hoja yake kwa nini tozo ya huduma inayopaswa kulipwa na Kampuni za kigeni zinazojenga Mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere ilipwe halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni badala ya Rufiji kwenye Mradi imepelekea wilaya Rufiji kupokea mabilioni ya pesa kutoka kwenye makampuni hayo na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendelo ya wilaya hiyo kongwe, (Rufiji ni Wilaya toka Mkoloni).

Michango yake Bungeni imechangia kiasi kikubwa kuanza kwa Mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere uliokwama kwa zaidi ya miaka 60(Rejea Ansad Bungeni).

Wakati fulani aliamshra fulaha Bungeni alipokumbusha ahadi ya Mwalimu Nyerere ya kujenga Barabara Tarafa ya Mkongo wilayani Rufiji aliyoitoa 1955 wakati wa Kikao Cha Halmashauri kuu ya Tanu kikichofanyika Tarafa ya Mkongo Rufiji.

Kwa Jitihada zake Mh Mchengelwa, halmashauri sasa wanajenga Shule ya Upili Tarafa ya Mkongo yenye jina la Muaaisi na Mpigani Uhuru wa Nchi hii Bibi Titi Mohamed.

Kwa Jimbo lake hakika ni Mwanasisa wa kupigiwa Mfano na kwa wanaojua siasa za Rufiji huwa ni ngumu Sana kwa Mbunge kupenya awamu ya pili lakini kwake haikuwa kazi ngumu sana kutokana na aliyoyafanya ndani ya awamu yake ya kwanza.

Kuanzia katika Utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji,Changamoto za maji,Barabara na Umeme.

Hatma ya hekari elfu hamsini zilizotengwa kando ya Mto Rufiji baada ya kukamilika ujenzi wa mradi Mwalimu Nyerere.

Kutowajibika ipasavyo kwa Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji/Rubada(Kwa mujibu wa tafiti kilimo Cha mpunga katika bonde hili kinaweza kulisha nchi mzima ya Tanzania).

Mara Kadhaa akijenga hoja bungeni kuwa ufumbuzi wa tatizo la sukari Tanzania utapatikana katika Bonde la Mto Rufiji(Kuna wawekezaji zaidi ya watatu wa viwanda vya Sukari Rufiji) ndio kusema.

Mh.Mchengelwa ni Mbunge wa kuwasemea Watanzania.

Hakusita kuwa Mkali na Kusimamia alichokiamini wakati fulani alihoji Bungeni kwa lugha Kali kidogo ni Kwa nini Kampuni ya Sukari ya Kagera kukopa mabilioni ya Pesa na Kwenda kuwekeza DRC wakati nchi inashida kubwa ya Sukari,hayo na mengine mengi yenye Maslahi ya Tanzania yamekuwa ndio Kilio chake.

Jimboni kwake amefanya mengi huwezi kuweka yote hapa ila mawili yatakayomfanya akumbukwe na wana Rufiji ni Kuhakikisha kila Tarafa inakuwa na Shule ya A level(Mkongo,Ikwiriri na Shule pekee ya mabinti Mohoro)

Kutekeleza kwa asilimia 100% agizo la Serikali kuu kujenga madarasa mapya kuchukua wanafunzi waliokwama kuingia kidato cha kwanza(Madarsa 13 ya kisasa ndani ya Mwezi mmoja) na kufanya kuwa miongoni mwa halmashauri zilizofanya vyema katika zoezi hilo nchini.
Michango yake bungeni pia imepelekea Rufiji kutengewa fungu na Tamisemi kujenga jengo jipya halmashauri ili kuondokana na Boma wanalolitumia sasa lililorithiwa toka kwa Mjerumani.

Bila kusahau hoja yake Bungeni kwa nini Mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere Rufiji utakaotoa ajira ya zaidi 6000 na serikali kuwekeza zaidi ya trilioni 6.5 unafanyika katika wilaya ambayo haina benki ya Serikali na hata binafsi imepelekea serikali kupeleka benki katika wilaya hio Kongwe.

Ndio kusema Mh.Mchengelwa anawasemea watu wake na taifa kwa Ujumla.

Ushauri wetu kwake aendelee kusemea wananchi wake na taifa bila kusahau Kilio chake cha muda mrefu juu ya ujenzi wa Barabara ya Kibiti Mloka kiwango cha lami.

Kwani asilimia kubwa Malighafi za mradi ya Mradi wa Umeme Mwl Nyerere hupita kwenye barabar hii ambayo haiko kwenye hali nzuri hasa kipindi Cha Mvua.

Pia asimamie ahadi na Ilani ya Chama Cha mapinduzi ujenzi wa barabara Nyamwage Utete ambapo wabunge kabla yake hawakufanikiwa kufanya hivyo.

Kwa uzalendo wako na uchapakazi tunaamini utatumikia taifa ipasavyo katika jukumu lako jipya la Waziri ofisi ya Raisi utumishi na Utawala Bora na Kumsaidia Mh. Rais katika kazi yake ya kuijenga Tanzania Tuitakayo.
Hizi sifa ndiyo mama hazitaki ziishie huku huku kwa kina Mchengerwa
 
Yani unakaa kabisa unajiaminisha Waziri mzima wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi na Utawala Bora akae na apate muda wa kuandika humu JF kweli kwa hizi siku mbili walivyowekwa busy mzee????? Ni sisi wenye mudanwa haya wao saa hii ofisi za Moto sana .
Huyu kasomea Dar-es salaam Kampala University mbona unasema alisoma Makerere?
huyu sasa ni Boss na mkwe, Mama keshas ema aningia mitandaoni hadi saa 11 alfajiri
hiyo mliyoiweka sio CV kwanini msiifuate kule Member of Parliament kila kitu kipo wazi, humuhumu tumeshamjadili Mohamedi Mchengerwa (na sio Mchengelwa)
 
Amepata nafasi nyeti sana lakini anahitahi kubadilika ili aweke integrity kwenye hiyo nafasi, na kutunza heshima ya aliyemteua.

Akiwa Msaidizi wa Jaji Mkuu alikuwa na element za UTAPELI. Kuna maamuzi ya kuhamisha Mahakimu ambayo alikuwa anafanya bila idhini ya CJ. Pengine alikuwa anapata chochote.

Nimeliweka hili kumjenga na siyo kumbomoa kwa hiyo halihitaji ubishi.
Chief Justice ana husika vipi na uhamishaji wa Magistrates ?

Judge Assistant ana husika vipi na uhamishaji wa Magistrates ?
 
Umeanza uchawa baada ya kusoma upepo! Vijana wa Bongo baada ya vyuo mnavyosoma vya kata hamna uwezo wa kubuni miradi mnakalia upambe kwa watu wenye mamlaka!
Siku zote Mchengerwa alizokuwa Bungeni mbona hukutupa CV yake?!
Acha kuwa CHAWA!
 
Kwa CV hiyo Jiwe kwanini hakumpa uwaziri mpk mama mkwe alipoingia madarakani.
 
Umeanza uchawa baada ya kusoma upepo! Vijana wa Bongo baada ya vyuo mnavyosoma vya kata hamna uwezo wa kubuni miradi mnakalia upambe kwa watu wenye mamlaka!
Siku zote Mchengerwa alizokuwa Bungeni mbona hukutupa CV yake?!
Acha kuwa CHAWA!
Kama huna akili huna tu.
Kipindi akiwa bungeni ningeandika ungesema kwa nini sikuandika kabla hajawa bungeni.
Akili kaazime
 
Back
Top Bottom