Mtela Mwampamba
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 537
- 347
Wana-Jukwa,
Nimeshitushwa kama sio kupata sintofahamu kuhusu huyu mtu anayeitwa Freeman Mbowe(Mwenyekiti wa CHADEMA).Kilichonishitua ni kichwa cha habari kwenye gazeti la Mwanachi leo tar.10/06/2013 "CHADEMA YAKUBALI SERIKALI TATU" sub headings zanafupisha kwa kusema Mh.Freeman Mbowe aikubali rasimu ya katiba Mpya.
Hii habari ya Mh.Mbowe kuikubali rasimu ya katiba mpya ni Mwendelezo wa siasa zake za kinafi,uogo,upepo, na undumila kuwili mbele ya umma wa watanzania.
Naomba kuonesha sehemu tatu tofauti ambazo Mh.Mbowe amekuwa akibaka kauli zake za awali na kabadirika kama kinyonga kusifia jambo husika.
1.Wanajukwaa wote manakumbuka wazi kuwa Mh.Mbowe bunge la kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo CHADEMA waliunda kambi rasmi ya upinzani bungeni.Mbowe alikataa mbele ya kiti cha spika kuendelea kutumia gari la serikali (Kambi ya Upinzani Bungeni-KUB).Alisema hawezi kutumia gari hilo kwa sababu nila kifahari sana,pia linatumia mafuta mengi sana hivyo ni ufujaji wa mali za umma.
LAKINI,Hadi kufikia jana kwenye mkutano wa kata ya iyela Mbeya Mh.Freeman Mbowe alikuwa na gari hilo KUB.Huu ni unafiki na uongo mkubwa kwa watanzania,haiwezekani "ukasafisha kikombe nje wakati ndani ni kichafu kupindukia"Mh.Mbowe anakwenda kwenye vyombo vya habari na kudanganya umma kuwa hataki gari la serikali,Lakini nyuma ya pazia analitumia tena hadi kwenye mikutano yake ya chama. Huu ni upuuzi mkubwa unaofanywa na Mh.Freeman Aikael Mbowe ambao watanzania ni lazima wafunguke macho.
2.Mh.Freeman Mbowe akiwa kama mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni aliongoza kambi yake kupinga posho bungeni kwa wabunge kwamba ni ufujaji wa fedha.Alisisitiza yeye na wabunge wote wa CHADEMA wataacha kuchukua posho mara moja,na hata wakilazimishwa hawatapokea.Ikatokea Mbunge wa CHADEMA Mh.Shibuda akapingana na kauli ya mwenyekiti kwa kusema naomba posho ziongezwe sio zipunguzwe.Kauli ile ya shibuda ilikuwa ni yakishujaa kwake kwa sababu alijua namna Mbowe alivyomuongo mbele za Umma.Shibuda akaingia kwenye msuguano na Mh.Mbowe wa kisiasa ndani ya chama.
LAKINI,Hadi kikao hiki cha bunge la bajeti Mbowe anaongoza wabunge wenzake kuchukua posho za vikao vya bunge.Je huyu mbowe ni mtu wa aina gani?Ni kiongozi wa mwenyetabia za kinyonga ambaye hajitambuim,hanamsimamo na anajidhalilisha sana kwa kuwa na ndimi mbili halafu bado anajiita kamanda.Mh.Mbowe huu unafiki na uongo utaacha lini?.
3.Kutomtambua Rais kikwete.Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Mbowe na Katibu mkuu wake Dr.slaa aliongoza kupinga kutomtambua Rais kikwete mara tu baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.
LAKINI Huyu huyu Freeman Mbowe aliongoza wabunge wenzake kwenda ikulu kwa Rais kikwete kuongea naye na kupata Breakfast,Juice n.k(Picha zipo zinazoonesha Mbowe na team yake walivyokuwa wanabadilisha mikao ikulu).Je ikulu walikwenda kwa Rais yupi?.
Mbali zaidi Mh.Mbowe alipokuwa jimboni kwake HAI alikiri wazi hakuna Rais kama kikwete katika maisha yake ya siasa kwa sababu ni mchapa kazi.Huu si uongo video hii hapa Freeman Mbowe alipomfagilia JK kwa juhudi zake za kuendeleza miundombinu Tanzania - YouTube (Freeman Mbowe alipomfagilia JK kwa juhudi zake za kuendeleza miundombinu Tanzania - YouTube).
Kwenye video hii Mh.Freeman Mbowe anasema ametembea angani na nchi kavu hajaona Rais kama kikwete.Je mwaka 2010 si walipinga kuchaguliwa kwa kikwete? Mh.Mbowe hii tabia ya kukosa msimamo wa kauli zako ni urithi au ugonjwa ulionao ambao wewe huuujui?Hii ni dharau na ni fedheha kwa chama cha siasa kuongozwa na mtu anayekosa pa kusimamia,Upepo unafanya afuate mwelekeo wake.
Huyu ndiye mbowe.
5.SASA SWALA LA KATIBA MPYA.
Mh.Freeman Mbowe akihutubia bunge kama Waziri mkuu kivuli bunge la tanzania,Alisema CHADEMA wanapinga mchakato wa katiba mpya kwa sababu hauna maoni ya wananchi,haujafuata misingi ya kidemokrasia.Pia alienda mbali zaidi kwa kusema TUNA TOA MUDA WA SIKU 15 KWA TUME YA KATIBA KUSITSHA MCHAKATO HUO,NA ENDAPO UTAENDELEA CHADEMA ITAJITOA KWENYE MCHAKATO WA KATIBA MPYA.Hii kauli ilisemwa na Mbowe,
Pia kwenye mkutano wa chadema viwanja vya Temeke mwisho Mbowe na Tundu lissu walisema hawaungi mkono tume na mchakato mzima wa katiba mpya.
CHADEMA chini ya Mbowe wakaenda mbali zaidi kwa kuanza kumshawishi mjumbe wa tume ya katiba mpya ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Prof.Mwesigwa Baregu ajitoe kwenye mchakato wa katiba mpya. Huyu msomi na mwelevu Prof.Mwesigwa baregu akaweka uzalendo mbele kwa kusema" NIKIAMBIWA NICHAGUE KATI YA CHAMA CHANGU NA NCHI YANGU..HARAKA SANA NITACHAGUA NCHI YANGU" haya majibu ni yakizalendo na yenye ujazo wa Utaifa mbele sio chama.
SASA MBOWE AIKUBALI RASIMU YA KATIBA MPYA,Hapa ndipo paliponifanya nijisogeze karibu nanyi wadau wa siasa tutathimini huyu Mbowe ni binadamu wa aina gani?Ni kiongozi wa aina gani?Ni kiongozi au msaka umaarufu?.Kwa sababu haiwezekani ndani ya bunge hili linaloendelea ameongoza CHAMA chake kugomea mchakato wa katiba mpya,Hata bunge halijaisha anaongoza chama chake kuikubali rasimu ya katiba mpya,tena sio tu kuikubali kuunga mkono moja kwa moja rasimu ya katiba mpya kipengele cha serikali tatu.
Kimsingi kwa namna Mh.Mbowe anavyojikanyagakanyaga kwenye kauli zake ndivyo taswira ya chama chake kilivyo kuanzia ngazi ya Taifa hadi tawi,Viongozi wake wanajikanyakanyaga kwa kufuata kauli za mwenyekiti.
Nahofia ipo siku Mbowe ataongoza wabungu na wanachadema wote kugomea uchaguzi mkuu,then baada ya siku kadhaa akaunga mkono uchaguzi mkuu.Huyu sio kiongozi bora ni bora kiongozi watanzania tufunguke.
Kujikanyagakanyaga huku kwa Mh.mbowe ni matunda ya siasa za sifa,Siasa za kutafuta vichwa vya habari kwenye magazeti na media zingine.Siasa za msimu,Siasa na kutega masikio.CHADEMA wanatafuta tention ya kusikika kila mara kwenye masikio ya watu,wanatunga uongo,wanakuwa wanafiki ilimradi tu wasikike kuwa wapo.Hii ni hatari sana na lazima kuiogopa chadema kama ukoma.
MY TAKE:
Mh.Freeman Mbowe jikague hapo ulipo,Safisha ubongo wako kwanza ndipo usimame kuongea.Ninachojua sio ujinga kuuliza,Mbowe unanafasi ya kujiuliza kwa viongozi wenzako wa kisiasa na hata wale wasio wa kisiasa namna ya kuchambua mambo na kuja na kauli moja ya kusimamia. Bila kufanya hivyo ipo siku Mh.Freema Mbowe utajikuta mtupu mbele ya haraiki ya watanzani,ikumbukwe njia ya Muongo ni fupi.