Huyu ndiye mh. Mbowe na hatari ya kujikanyagakanyaga kwenye kauli zake,amekosa msimamo kupita kiasi

Pole ndugu yangu. Unajipakazi sana kutafuta udhaifu wa viongozi wa CDM lakini hutafanikiwa zaidi sana utakuwa unajiaibisha kwa kutojua siasa. Mh. Mbowe ni Maarufu na hahitaji kuupata kupitia Rasimu ya Katiba. Wanaotafuta umaarufu kwa sasa ni viongozi wa CCM ambao, awali, walipinga kwa nguvu zote uundwaji wa katiba mpya, lakini sasa wako mstari wa mbele kuizungumzia. Mh. Mbowe is a Politician, knows what is better for the Tanzanians and what is not, hakurupuki.
 
Mkuu ataangaika sana kijana na propaganda..
lakini utachemka tu,chadema ni Taifa kubwa mambo ya ccm ya huku chadema hutayaweza ndg!
Mtela Mwampamba unatakiwa ujue kwamba mtu ambae ni flexible ni bora kuliko ambae ni rigid.Hii ni kwa sababu yule ambaye ni flexible ana nafasi ya kujisahihisha.Hili ni jambo zuri kwa kuwa hakuna binadamu hukosea.Sidhani kama hapa kuna jambo lolote la ajabu.Kuhusu gari na posho, wakati flan mtu unaweza uwe unakataa kitu ila mfumo ukulazimishe. Unakumbuka Zitto alivyokataa posho na hatua alizochukua spika kumlazimishia achukue posho?
 
Last edited by a moderator:
Nenda kamuulize Lukuvi na speaker wa bunge. Nina taarifa za uhakika kabisa kwamba Mbowe alilirudisha gari la KUB, lakini akaamrishwa kwamba lile gari anapewa kwa mjibu wa sheria za nchi. Kutokutumia kwake kunaweza kumfanya ashitakiwe kwa kushindwa kutekeleza sheria na taratibu za nchi. Na zaidi ya yote alitanabaishwa kwamba iwapo angepatwa na tatizo lolote la kiusalama serikali ndiyo ingelaumiwa kwa kutompa ulinzi anaostahili, likiwemo gari na dereva wa uhakika.

Nimekuwa na mazungumzo binafsi na wabunge wa CHADEMA akiwemo Zitto juu ya hela ya Ruzuku ambayo wabunge hawa walikuwa wakiikataa kwa muda kiasi. Ukweli ni kwamba hii hela ambayo wabunge wa CHADEMA waliikataa waliomba iongezwe kwenye shughuli za maendeleo majimboni. Lakini kilichotokea katika ile mikutano ambayo wabunge wa CHADEMA hawakupokea hizo hela, hakuna kilichoongezwa kwenye mifuko ya majimbo, badala yake ile hela ilikuwa inaliwa na watu wachache, jambo lililopelekea wabunge wa chadema kukubaliana kwamba waichukue ile hela na kuipeleka wenyewe majimboni. Katika wabunge wote wa CHADEMA asiyechukua posho ni Zitto tu ambaye amenitamkia kwa maandishi yake kwenye twitter kuwa hajali inatumikaje, anachojali, halipwi hela isiyo halali.

Wewe acha kudanganya na kupotosha watu hapa, Kama yeye Bw.Mbowe alilazimishwa kutumia gari (kama ni kweli!) basi ni kwanini hakuamua kuchukua la bei Rahisi angalau kuokoa pesa ya Serikali? Wapo viongozi wengi tena wakubwa Serikalini mpaka Mawaziri au Makatibu wakuu na hawatumii Magari hayo mapya, wameamua kutumia ya zamani!

Unaongelea kuhusu Hongo au posho, kama ni kweli unavyosema sasa ni kwa nini hawakurudi tena kwa Wananchi na nguvu ile ile kutuambia kwamba tumeamua kuendelea kuchukua Hongo au Posho yetu ndefu ya Ubunge kwa sababu hizo ulizozitaja?
Kwa nini wakati wanapinga Hongo au Posho walitanganza kila mahali, iweje washindwe kutanganza walipoaihirisha na kuanza kuchukua hiyo Hongo au Posho? wengine tulikuwa tunafikiri kweli wameacha kumbe, waliamua kuchukua tena, sasa tungezijuaje sababu za wao kuanza kuchukua tena Hongo au Posho ya Bunge?
 
Mbowe angeipinga rasimu bado Mwampamba et al wangepiga kelele, Mbowe kaunga mkono rasimu wanapiga kelele, Mbowe angekaa kimya wangepiga kelele. Kweli Mbowe kawashika pabaya
 
Ngoja wajevijana wa bivicha aka wanywa viroba upokee matusi badala ya hoja.
 
Jaji Warioba. Katika mikutano ambayo Tume imekwenda kuchukua maoni ya wananchi kuanzia mwezi Julai hadi Novemba mwaka jana kuhusu uundwaji wa Katiba Mpya, wananchi wengi wamependekeza madaraka ya rais yapunguzwe kwani yanampa nguvu kubwa kisheria. Jaji Warioba anasema kuwa hoja ya Muungano pia itahitaji uamuzi mgumu kwa kuwa ni moja ya maeneo yaliyotolewa maoni mengi. "Mawazo ni mengi tena yanakinzana, wapo wanaotaka Serikali za Majimbo wengine hawataki, huu ni mfano tu wa baadhi ya mambo yanayohitaji Tume kufanya uamuzi mgumu kama nilivyosema, lakini kwa maslahi ya taifa,"anasisitiza Jaji Warioba.
Pinda naye amnanga Mbowe Waziri Mkuu Mizengo Pinda naye anatofautiana na Mbowe kuhusu Mchakato wa Katiba unaondelea akieleza kuwa malalamiko ya chadema chake kuhusu mchakato huo yanatokana na homa ya uchaguzi mkuu mwaka 2015. Waziri Mkuu Pinda anatoa kauli hiyo wakati anajibu madai ya Mbowe dhidi ya mchakato wa katiba. Anasema malalamiko hayo ya Chadema, yanatokana na viongozi wake kuweka kipaumbele kikubwa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwaka 2015. "Nadhani Mbowe ameanza kuchanganya mambo na kupagawa na Uchaguzi wa 2015 wa nani atakuwa Rais 2015. Anasema Pinda akinuu sehemu ya hotuba ya Mbowe iliyosema "Tume ya Mabadiliko ya Katiba imethibitisha haina Weledi wa kusimamia mchakato huru usiofungamana na upande wowote". Waziri Pinda anaendelea "Mimi nadhani hii siyo lugha ya kiungwana Kwa Tume ambayo imeundwa kwa mujibu wa Katiba na yenye Watu wanaoheshimika sana Nchini." Pinda anafafanua kuwa Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya kupewa orodha ya majina yaliyopendekezwa na Vyama vya siasa vyenyewe vilivyo na usajili wa kudumu na asasi nyingine zikiwamo za kidini. "Katika Tume hii, wapo wajumbe wawakilishi kutoka Chadema wenye Weledi mkubwa wengine ni Maprofesa. Siamini Kama Mbowe anashindwa kutambua kwamba Mjumbe wake katika Tume hii ni Profesa Mwesige Baregu. Sasa ni Weledi upi anaozungumzia ambao Profesa Baregu hana," anasema Pinda.
 
Siku nyigi sana nilisema Freeman Mbowe ni syastem na hana upinzani wa kweli anawadanganya wachagga wenzake wauvae mkenge.
Mtela Mwampamba umethibitisha hayo na umefunga kazi. Nawasikitikia mabumbumbu wanaovaa magwanda kumfata mtu kama huyo.

Ama kweli posho mbaya sana huwa zinamfanya mtu awe kipofu asione ukweli, Kwahiyo Lusinde au Lameck ndio viongozi bora?
 
Last edited by a moderator:
Nenda kamuulize Lukuvi na speaker wa bunge. Nina taarifa za uhakika kabisa kwamba Mbowe alilirudisha gari la KUB, lakini akaamrishwa kwamba lile gari anapewa kwa mjibu wa sheria za nchi. Kutokutumia kwake kunaweza kumfanya ashitakiwe kwa kushindwa kutekeleza sheria na taratibu za nchi. Na zaidi ya yote alitanabaishwa kwamba iwapo angepatwa na tatizo lolote la kiusalama serikali ndiyo ingelaumiwa kwa kutompa ulinzi anaostahili, likiwemo gari na dereva wa uhakika.

Nimekuwa na mazungumzo binafsi na wabunge wa CHADEMA akiwemo Zitto juu ya hela ya Ruzuku ambayo wabunge hawa walikuwa wakiikataa kwa muda kiasi. Ukweli ni kwamba hii hela ambayo wabunge wa CHADEMA waliikataa waliomba iongezwe kwenye shughuli za maendeleo majimboni. Lakini kilichotokea katika ile mikutano ambayo wabunge wa CHADEMA hawakupokea hizo hela, hakuna kilichoongezwa kwenye mifuko ya majimbo, badala yake ile hela ilikuwa inaliwa na watu wachache, jambo lililopelekea wabunge wa chadema kukubaliana kwamba waichukue ile hela na kuipeleka wenyewe majimboni. Katika wabunge wote wa CHADEMA asiyechukua posho ni Zitto tu ambaye amenitamkia kwa maandishi yake kwenye twitter kuwa hajali inatumikaje, anachojali, halipwi hela isiyo halali.

Hii hoja umeileta bila tafakari. Mbowe na wabunge wa CDM walisema hawatamtambua Kikwete hadi akubaliane na pendekezo lao la katiba mpya. Na msimamo wao ulipozidi kukazwa, Kikwete akanywea kutokana na msimamo wao mkali na kuamua kuwaalika ikulu kujadili kuhusu hoja yao ya katiba mpya. Na kutokana na mkutano kati ya Raisi na viongozi wa CHADEMA, hivi leo Tanzania mpya inaundwa. Katika hili Mtela acha unafiki. CHADEMA wamefanya kazi nzito, kubwa na ya kukumbukwa katika historia ya Tanzania.

Kwa uelewa wako finyu ulitaka Mbowe apinge hata ukweli ulio wazi hasa katika mambo ambayo matokeo ya utendaji wake yapo wazi?

Tatizo lao halikuwa kwenye Rasmu ya katiba bali kwenye mchakato wa katiba. Ni bahati mbaya kwamba hujui kuwa hii ni rasimu tu na siyo katiba. Na ni bahati mbaya nyingine kwamba hujui kwamba CHADEMA walikuwa wanapinga utaratibu wa upatikanaji wa wawakilishi katika mabaraza ya katiba ambayo ndiyo yanakwenda kuipitisha hii rasmu ya katiba ili kuwa katiba.

Huu ni uongo uliopindukia. CHADEMA haikuwahi kuipinga tume ya katiba. Bali walimshawishi mjumbe wa tume ya katiba ajitoe kwa kuwa walikuwa wanapinga uhuni wa CCM wa kupenyeza watu wao kwenye mabaraza ya katiba, na wakaona ya kwamba uwepo wa mjumbe wao mmoja tu kwenye tume usingetosha kushawishi mambo mhimu ambayo CCM wangeyalazimisha kupitia hao wajumbe waliochaguliwa kimizengwe.

Kimsingi, huna point maana unaonekana hujui unaongelea nini?

Mkuu umejaribu kujibu hoja za Mtela ila kwa bahati mbaya umeingia chaka hauna uliojibu hata moja.
Kauli zote zilizotoka katika kinywa cha Mbowe kama mwenyekiti wa chama ambazo zilizikuwa zinawakilisha msimamo wa chama tena akizitoa publically kwanini kinyume chake zisitolewa publically bali ukimya ukatawala kwa mzungumzaji?
Mkuu chadema hakina tofauti na ccm tena chenyewe ndicho chenye madudu na watenda madudu kuliko ccm.
Fikiria sasa hizi kipo nje ya utawala viongozi wake ni hawa wasioleweka,kila mtu ana msimamo wake anaeamka usingizini kuna mwanachama mwenzako kamuuzi anamfukuza kisa yeye yuko top management kweli ni lipi jipya watalileta hata wakiwa ikulu?
 
Mbowe angeipinga rasimu bado Mwampamba et al wangepiga kelele, Mbowe kaunga mkono rasimu wanapiga kelele, Mbowe angekaa kimya wangepiga kelele. Kweli Mbowe kawashika pabaya
kajishika mwenyewe pabaya..anababaika na hivi shule hana
 
Wewe acha kudanganya na kupotosha watu hapa,

Kama yeye Bw.Mbowe alilazimishwa kutumia gari (kama ni kweli!) basi ni kwanini hakuamua kuchukua la bei Rahisi angalau kuokoa pesa ya Serikali? Wapo viongozi wengi tena wakubwa Serikalini mpaka Mawaziri au Makatibu wakuu na hawatumii Magari hayo mapya, wameamua kutumia ya zamani!
Kwa hiyo Mbowe angetoa hela yake ya mfukoni kununua gari la bei nafuu na linalotumia mafuta kidogo? Hilo gari la zamani lilikuwa wapi ambalo Mbowe angeweza kwenda kulitumia?

Unaongelea kuhusu Hongo au posho, kama ni kweli unavyosema sasa ni kwa nini hawakurudi tena kwa Wananchi na nguvu ile ile kutuambia kwamba tumeamua kuendelea kuchukua Hongo au Posho yetu ndefu ya Ubunge kwa sababu hizo ulizozitaja?
Hili linategemeana zaidi na uelewa wako wa siasa. Nafikiri kwa mwanasiasa makini angejua ni kwanini kuna baadhi ya sera huwa zinatangazwa na mwisho wa siku zikishindikana zinaachwa kimya kimya. Hivi wewe umeshawahi kujiuliza ni kwanini Nape hajapita tena kwa wananchi kuwatangazia kwamba zile siku tisini alizoyapa magamba zimeshindikana? Inaonekana hujakomaa kisiasa.

Ama kweli posho mbaya sana huwa zinamfanya mtu awe kipofu asione ukweli, Kwahiyo Lusinde au Lameck ndio viongozi bora?

Ndugu yangu najua unajitahidi kuandika humu ila ukweli umekukaa moyoni may be unashindwa kuuonyesha kuhofia usije kosa nafasi yako uliyoahidiwa iff ikiwa.
Wafuasi wa chadema mmegeuzwa mazuzu hata uhuru mnakosa, elimu yenu ni useless kujadili issues na mmebakia kusema mtayamaliza kwenye vikao halafu ndio imeisha. Kuwa huru jibu hoja za mtela kama una uwezo.
 
Duh! Huu uzi ni hatari sana! Una ukweli mtupu na Umeangaza Maisha ya Mbowe! Mbowe kwa Mambo haya sasa ajifunze kuwa na msimamo katika Kauli!
 
Kwa hiyo Mbowe angetoa hela yake ya mfukoni kununua gari la bei nafuu na linalotumia mafuta kidogo? Hilo gari la zamani lilikuwa wapi ambalo Mbowe angeweza kwenda kulitumia?

Hili linategemeana zaidi na uelewa wako wa siasa. Nafikiri kwa mwanasiasa makini angejua ni kwanini kuna baadhi ya sera huwa zinatangazwa na mwisho wa siku zikishindikana zinaachwa kimya kimya. Hivi wewe umeshawahi kujiuliza ni kwanini Nape hajapita tena kwa wananchi kuwatangazia kwamba zile siku tisini alizoyapa magamba zimeshindikana? Inaonekana hujakomaa kisiasa.

Bw.Nape hajapita kwa Wananchi kwa sababu ni msanii na CCM ni Wasanii na ndio maana Watz wanafuta Chama mbadala ambacho hakina wasani kama CCM, sasa kama kila kukicha hata ambao labda wangekuwa mbadala wanafanya yale yale ambayo CCM wanayafanya tofauti iko wapi?

Mwisho wa siku wote wako hapo kwa ajili tu ya kuwatumia Wananchi na Si Vinginevyo!
 
Leo imechoma watu hii kitu tena naa ushahidi juu. Ni hatari kutokuwa na msimamo. Chadema hakuna vichwa hapo vinavyoweza kupewa uenyekiti? Coz jamaa hauziki kabisa cku hizi. Asante Mwampamba.
 
Mkuu umejaribu kujibu hoja za Mtela ila kwa bahati mbaya umeingia chaka hauna uliojibu hata moja.

Kauli zote zilizotoka katika kinywa cha Mbowe kama mwenyekiti wa chama ambazo zilizikuwa zinawakilisha msimamo wa chama tena akizitoa publically kwanini kinyume chake zisitolewa publically bali ukimya ukatawala kwa mzungumzaji?
Sometimes kama chama mnalazimika kukaa kimya kwa ajili ya mstakabali wa taifa na usalama wa nchi. Siyo kila jambo ni la kulipeleka kwa wananchi pale linapokuwa limeshindikana. Maana ukitaka kulirudisha kila jambo kwa wananchi kwa kuwa umeshindwa kushawishi basi unaweza kujikuta unawapandisha hasira wananchi na kuvuruga amani ya nchi.

Fikiria sasa hizi kipo nje ya utawala viongozi wake ni hawa wasioleweka,kila mtu ana msimamo wake anaeamka usingizini kuna mwanachama mwenzako kamuuzi anamfukuza kisa yeye yuko top management kweli ni lipi jipya watalileta hata wakiwa ikulu?
Kwahiyo ulitaka CHADEMA nao waendekeza kulindana kama wanavyofanya CCM kiasi cha kuifilisi nchi na kusababisha umaskini uliopindukia? Chama chenye uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya yeyote, bila kujali nafasi yeke ndiyo chama chenye uhakika wa kuweza kuchukua nafasi ya kiuongozi katika nchi. Maana hakitamwonea haya yeyote atakayeamua kuenenda kinyume na sheria na taribu za uongozi.
 
Ndugu yangu najua unajitahidi kuandika humu ila ukweli umekukaa moyoni may be unashindwa kuuonyesha kuhofia usije kosa nafasi yako uliyoahidiwa iff ikiwa.
Wafuasi wa chadema mmegeuzwa mazuzu hata uhuru mnakosa, elimu yenu ni useless kujadili issues na mmebakia kusema mtayamaliza kwenye vikao halafu ndio imeisha. Kuwa huru jibu hoja za mtela kama una uwezo.

Mkuu ukweli upo wapi hapo kama sio majungu na umbea wa Lameck na Nape unaopikwa hapo kazini kwenu Lumumba?
 
Bw.Nape hajapita kwa Wananchi kwa sababu ni msanii na CCM ni Wasanii na ndio maana Watz wanafuta Chama mbadala ambacho hakina wasani kama CCM, sasa kama kila kukicha hata ambao labda wangekuwa mbadala wanafanya yale yale ambayo CCM wanayafanya tofauti iko wapi?

Mwisho wa siku wote wako hapo kwa ajili tu ya kuwatumia Wananchi na Si Vinginevyo!
Soma jibu langu kwenye post namba 58
 
Back
Top Bottom