Huyu ndiye mh. Mbowe na hatari ya kujikanyagakanyaga kwenye kauli zake,amekosa msimamo kupita kiasi


M

Mtela Mwampamba

Verified Member
Joined
Dec 19, 2012
Messages
537
Likes
11
Points
35
Age
36
M

Mtela Mwampamba

Verified Member
Joined Dec 19, 2012
537 11 35
Wana-Jukwa,

Nimeshitushwa kama sio kupata sintofahamu kuhusu huyu mtu anayeitwa Freeman Mbowe(Mwenyekiti wa CHADEMA).Kilichonishitua ni kichwa cha habari kwenye gazeti la Mwanachi leo tar.10/06/2013 "CHADEMA YAKUBALI SERIKALI TATU" sub headings zanafupisha kwa kusema Mh.Freeman Mbowe aikubali rasimu ya katiba Mpya.

Hii habari ya Mh.Mbowe kuikubali rasimu ya katiba mpya ni Mwendelezo wa siasa zake za kinafi,uogo,upepo, na undumila kuwili mbele ya umma wa watanzania.

Naomba kuonesha sehemu tatu tofauti ambazo Mh.Mbowe amekuwa akibaka kauli zake za awali na kabadirika kama kinyonga kusifia jambo husika.

1.Wanajukwaa wote manakumbuka wazi kuwa Mh.Mbowe bunge la kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo CHADEMA waliunda kambi rasmi ya upinzani bungeni.Mbowe alikataa mbele ya kiti cha spika kuendelea kutumia gari la serikali (Kambi ya Upinzani Bungeni-KUB).Alisema hawezi kutumia gari hilo kwa sababu nila kifahari sana,pia linatumia mafuta mengi sana hivyo ni ufujaji wa mali za umma.

LAKINI,Hadi kufikia jana kwenye mkutano wa kata ya iyela Mbeya Mh.Freeman Mbowe alikuwa na gari hilo KUB.Huu ni unafiki na uongo mkubwa kwa watanzania,haiwezekani "ukasafisha kikombe nje wakati ndani ni kichafu kupindukia"Mh.Mbowe anakwenda kwenye vyombo vya habari na kudanganya umma kuwa hataki gari la serikali,Lakini nyuma ya pazia analitumia tena hadi kwenye mikutano yake ya chama. Huu ni upuuzi mkubwa unaofanywa na Mh.Freeman Aikael Mbowe ambao watanzania ni lazima wafunguke macho.

2.Mh.Freeman Mbowe akiwa kama mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni aliongoza kambi yake kupinga posho bungeni kwa wabunge kwamba ni ufujaji wa fedha.Alisisitiza yeye na wabunge wote wa CHADEMA wataacha kuchukua posho mara moja,na hata wakilazimishwa hawatapokea.Ikatokea Mbunge wa CHADEMA Mh.Shibuda akapingana na kauli ya mwenyekiti kwa kusema naomba posho ziongezwe sio zipunguzwe.Kauli ile ya shibuda ilikuwa ni yakishujaa kwake kwa sababu alijua namna Mbowe alivyomuongo mbele za Umma.Shibuda akaingia kwenye msuguano na Mh.Mbowe wa kisiasa ndani ya chama.

LAKINI,Hadi kikao hiki cha bunge la bajeti Mbowe anaongoza wabunge wenzake kuchukua posho za vikao vya bunge.Je huyu mbowe ni mtu wa aina gani?Ni kiongozi wa mwenyetabia za kinyonga ambaye hajitambuim,hanamsimamo na anajidhalilisha sana kwa kuwa na ndimi mbili halafu bado anajiita kamanda.Mh.Mbowe huu unafiki na uongo utaacha lini?.

3.Kutomtambua Rais kikwete.Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Mbowe na Katibu mkuu wake Dr.slaa aliongoza kupinga kutomtambua Rais kikwete mara tu baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.

LAKINI Huyu huyu Freeman Mbowe aliongoza wabunge wenzake kwenda ikulu kwa Rais kikwete kuongea naye na kupata Breakfast,Juice n.k(Picha zipo zinazoonesha Mbowe na team yake walivyokuwa wanabadilisha mikao ikulu).Je ikulu walikwenda kwa Rais yupi?.

Mbali zaidi Mh.Mbowe alipokuwa jimboni kwake HAI alikiri wazi hakuna Rais kama kikwete katika maisha yake ya siasa kwa sababu ni mchapa kazi.Huu si uongo video hii hapa Freeman Mbowe alipomfagilia JK kwa juhudi zake za kuendeleza miundombinu Tanzania - YouTube (Freeman Mbowe alipomfagilia JK kwa juhudi zake za kuendeleza miundombinu Tanzania - YouTube).

Kwenye video hii Mh.Freeman Mbowe anasema ametembea angani na nchi kavu hajaona Rais kama kikwete.Je mwaka 2010 si walipinga kuchaguliwa kwa kikwete? Mh.Mbowe hii tabia ya kukosa msimamo wa kauli zako ni urithi au ugonjwa ulionao ambao wewe huuujui?Hii ni dharau na ni fedheha kwa chama cha siasa kuongozwa na mtu anayekosa pa kusimamia,Upepo unafanya afuate mwelekeo wake.
Huyu ndiye mbowe.

5.SASA SWALA LA KATIBA MPYA.
Mh.Freeman Mbowe akihutubia bunge kama Waziri mkuu kivuli bunge la tanzania,Alisema CHADEMA wanapinga mchakato wa katiba mpya kwa sababu hauna maoni ya wananchi,haujafuata misingi ya kidemokrasia.Pia alienda mbali zaidi kwa kusema TUNA TOA MUDA WA SIKU 15 KWA TUME YA KATIBA KUSITSHA MCHAKATO HUO,NA ENDAPO UTAENDELEA CHADEMA ITAJITOA KWENYE MCHAKATO WA KATIBA MPYA.Hii kauli ilisemwa na Mbowe,

Pia kwenye mkutano wa chadema viwanja vya Temeke mwisho Mbowe na Tundu lissu walisema hawaungi mkono tume na mchakato mzima wa katiba mpya.

CHADEMA chini ya Mbowe wakaenda mbali zaidi kwa kuanza kumshawishi mjumbe wa tume ya katiba mpya ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Prof.Mwesigwa Baregu ajitoe kwenye mchakato wa katiba mpya. Huyu msomi na mwelevu Prof.Mwesigwa baregu akaweka uzalendo mbele kwa kusema" NIKIAMBIWA NICHAGUE KATI YA CHAMA CHANGU NA NCHI YANGU..HARAKA SANA NITACHAGUA NCHI YANGU" haya majibu ni yakizalendo na yenye ujazo wa Utaifa mbele sio chama.

SASA MBOWE AIKUBALI RASIMU YA KATIBA MPYA,Hapa ndipo paliponifanya nijisogeze karibu nanyi wadau wa siasa tutathimini huyu Mbowe ni binadamu wa aina gani?Ni kiongozi wa aina gani?Ni kiongozi au msaka umaarufu?.Kwa sababu haiwezekani ndani ya bunge hili linaloendelea ameongoza CHAMA chake kugomea mchakato wa katiba mpya,Hata bunge halijaisha anaongoza chama chake kuikubali rasimu ya katiba mpya,tena sio tu kuikubali kuunga mkono moja kwa moja rasimu ya katiba mpya kipengele cha serikali tatu.

Kimsingi kwa namna Mh.Mbowe anavyojikanyagakanyaga kwenye kauli zake ndivyo taswira ya chama chake kilivyo kuanzia ngazi ya Taifa hadi tawi,Viongozi wake wanajikanyakanyaga kwa kufuata kauli za mwenyekiti.
Nahofia ipo siku Mbowe ataongoza wabungu na wanachadema wote kugomea uchaguzi mkuu,then baada ya siku kadhaa akaunga mkono uchaguzi mkuu.Huyu sio kiongozi bora ni bora kiongozi watanzania tufunguke.

Kujikanyagakanyaga huku kwa Mh.mbowe ni matunda ya siasa za sifa,Siasa za kutafuta vichwa vya habari kwenye magazeti na media zingine.Siasa za msimu,Siasa na kutega masikio.CHADEMA wanatafuta tention ya kusikika kila mara kwenye masikio ya watu,wanatunga uongo,wanakuwa wanafiki ilimradi tu wasikike kuwa wapo.Hii ni hatari sana na lazima kuiogopa chadema kama ukoma.

MY TAKE:

Mh.Freeman Mbowe jikague hapo ulipo,Safisha ubongo wako kwanza ndipo usimame kuongea.Ninachojua sio ujinga kuuliza,Mbowe unanafasi ya kujiuliza kwa viongozi wenzako wa kisiasa na hata wale wasio wa kisiasa namna ya kuchambua mambo na kuja na kauli moja ya kusimamia. Bila kufanya hivyo ipo siku Mh.Freema Mbowe utajikuta mtupu mbele ya haraiki ya watanzani,ikumbukwe njia ya Muongo ni fupi.
 
habariyamujini

habariyamujini

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Messages
3,095
Likes
44
Points
145
Age
39
habariyamujini

habariyamujini

JF-Expert Member
Joined May 16, 2013
3,095 44 145
hawa chadema ni rangi mbili, hawajielewi walifanyalo..walitaka kujitoa, leo wanashabikia...siasa za upepo hizi
 
B

Bocho

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2013
Messages
1,489
Likes
3
Points
135
B

Bocho

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2013
1,489 3 135
Tatizo la viongozi wa CHADEMA ni wakurupukaji. Kuna mambo wanahitaji kukaa na kuyatolea maamuzi kwa pamoja badala ya kuwa na misimamo kinzani.

CHADEMA ilibidi wasimamie hoja ya mabaraza ya katiba kama ambavyo walikuwa wameanza tangu mwanzo. Cha kushangaza hilo wameshaliacha.
Kwa taarifa tu ni kwamba CCM ni wajanja sana wameweka mtego kwa wapinzani kuhalalisha mchakato wa ukusanyaji maoni.

Hapa wapinzani wote wamelewa na wanamsifu Warioba kwa rasimu nzuri.

Baada ya kupata ridhaa ya mchakato wa katiba, CCM wanakwenda kuibadilisha rasimu kwa kutumia mabaraza ya katiba na bunge la katiba iwe vile wanavytaka. Hapo ndipo wapinzani watakapolia na kuanza kuwaambia wananchi wapige kura ya hapana.

Katika hatua ya sasa wapinzani ilibidi kuungana kutaka mabadiliko katika mabaraza ya katiba ili tusijekubalishiwa yale ambayo wengi walikuwa wanayahitaji.
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
CHADEMA kilisema kuwa hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya, baada ya masharti kiliyotoa kwa serikali kikitaka kifanye mabadiliko kutotimizwa, na hivyo kumuagiza mwakilishi wao, Prof. Baregu ajitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwamba baada ya kujitoa kitaanzisha kampeni ya nchi nzima kuwahamasisha wananchi wasusie mchakato huo.


 
C

cheichei2010

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Messages
932
Likes
11
Points
35
C

cheichei2010

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2010
932 11 35
Mbona ulipokua CHADEMA ulikua unainanga CCM.Kwa hiyo saa hizi umeingia CCM unainanga CHADEMA. Ki fupi ni kwamba Huna Jipya.UNgekuja na maswali kama,Imekuwaje kwa sasa anaikubali?Kulikua na mazingira gani yaliyopelekea kukataa?Je Rasimu hii kutoka ina maana kwamba hakutakua na vikwazo kwenye mabaraza,ambayo CCM wameweka watu wao?
 
T

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,335
Likes
339
Points
180
Age
28
T

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,335 339 180
mbowe mimi sishangai anavyofanya mbowe simshangai yeye hufanya siasa za kuvizia na kuangalia aegemee wapi ila hana uwezo wa kuanziha hoja na akaitetea kwa mifano yenye mashiko.
 
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Messages
11,267
Likes
1,386
Points
280
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2012
11,267 1,386 280
Siasa za JF pasua kichwa.
 
Kijakazi

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Messages
3,546
Likes
52
Points
145
Kijakazi

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2007
3,546 52 145
Kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo mnavyozidi kugundua kwamba tatizo la TZ SIO CCM, bali ni la Mila Na Desturi zetu!

Huyo ndio Adui namba moja, nasema kila Mtz aliyezaliwa, kulelelwa na kukulia TZ yuko hivyo kama Bw.Mbowe au Bw.Kikwete, na wengi wetu tutafanya hivyo hivyo pindi tupatapo nafasi!
Tutaandika Katiba mpya nzuri tunavyotaka, tutaongea Majukwaani tunavyotaka lkn HAKUNA jipya!

Hakuna Mtanzania ambaye atakuwa tofauti na hao akina Bw.mbowe na Bw. kikwete, labda awe diaspora, yaani Mtanzania aliyelelewa ktk Mila na desturi za Jamii nyingine lkn siyo hii ya kwetu!

ANAYELALAMIKIA UFISADI TZ HAJAPATA NAFASI- Kardinali Pengo (Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Kanisa Katoliki
Tanzania)

 
T

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,335
Likes
339
Points
180
Age
28
T

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,335 339 180
Kijana kama wewe unaandika hivyo kisa, siasa ama? Pole sana, ila Mbowe ana umri kama wa baba yako mzazi, aliefukuzwa nae uanachama CHADEMA... ama hii ndio sababu?
mkuu siasa zinamambo mengi unaweza kumuona mtela ni mkosefu kumbe mbowe akawa mkosefu zaidi.
 
scramble

scramble

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Messages
1,593
Likes
0
Points
0
scramble

scramble

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2012
1,593 0 0
Uzi huu una ukweli mtupu. hongera Mwampamba kwa kutuonesha udhaifu na undumilakuwili wa CHADEMA na Mbowe!
 
Kijakazi

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Messages
3,546
Likes
52
Points
145
Kijakazi

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2007
3,546 52 145
Mbona ulipokua CDM ulikua unainanga CCM.Kwa hiyo saa hizi umeingia CCM unainanga CDM.Ki fupi ni kwamba Huna Jipya.UNgekuja na maswali kama,Imekuwaje kwa sasa anaikubali?Kulikua na mazingira gani yaliyopelekea kukataa?Je Rasimu hii kutoka ina maana kwamba hakutakua na vikwazo kwenye mabaraza,ambayo CCM wameweka watu wao?
Swala hapa sio kwamba mleta hoja ni CHADEMA au CCM, swala ni je, aliyoyaandika ni ya UKWELI au UONGO? Hilo ndilo swali la kujibiwa!
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
28,441
Likes
34,039
Points
280
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
28,441 34,039 280
Hapa inadhihirisha watu kuwa bora umeenda kwenye siasa za majitaka kuliko kama ungeenda kufundisha.
Ingekuwa ni janga kwa wanafunzi,

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Messages
8,416
Likes
3,937
Points
280
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2010
8,416 3,937 280
We umeishaambiwa kuwa CHADEMA wanakubaliana na maoni ya kuwa na serikali tatu,,, Ujue CHADEMA ni chama cha wananchi na kinategemea nguvu ya umma, kwa hiyo kama wananchi wamesema wanataka serikali tatu kupitia maoni yao kwa tume ya katiba, lazima chama cha kidemokrasia kama CHADEMA kifuate msimamo wa wananchi. CCM ni majizi yanayoangalia maslahi binafsi, wameona serikali tatu zitawazimbia ulaji na mianya ya wizi kwa kuwa Watanganyika ambao always ni wapole wameanza kudai haki zao, wanatumia hila kusiwe na serikali tatu. Hila wanazotumia CCM ni pamoja na kuwatuma vibaraka wao na wasaliti kama Mtela Mwampamba kupima upepo, kwa kuwa Mtela ni wa hovyo hovyo kwa watanganyika ataishia kupuuzwa tu. Mkitunyima Tanganyika yetu tutaidai kwa staili inayotumika kudai gesi
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Tume ya Katiba yaigawa CHADEMA


Mwandishi Wetu TUME ya Mabadiliko ya Katiba, imeanza kukivuruga Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Profesa Mwesiga Baregu, kugoma kujitoa kwenye tume hiyo kama anavyotakiwa na chama chake, huku Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa, akitaka suala hilo aulizwe Mbowe. Hivi karibuni akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani bungeni Msemaji Freeman Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA, alisema chama hicho hakiridhiki na mwenendo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kutekeleza majukumu yake na akatoa siku 30 za kurekebisha kasoro hizo

 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Mbowe alisema kuwa "Tume ya Mabadiliko ya Katiba imethibitisha haina Weledi wa kusimamia mchakato huru usiofungamana na upande wowote".
 
mwenezi

mwenezi

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Messages
505
Likes
14
Points
35
mwenezi

mwenezi

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2012
505 14 35
mwenyekiti wa gamba alizunguka nchi nzma anaahidi hovyohovyo,ila hakuahidi katiba mpya.makamanda walipowasha moto kuidai,mawaziri na makada wenu,ie kombani werema nawengine wakasema haiwezekani.leo vipi?there is no condition which is permanent.think big young boy.
 
T

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,335
Likes
339
Points
180
Age
28
T

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,335 339 180
Kwenye angalizo lako hapo mkuu, kwa kuzingatia elimu ya Mh. Mbowe, hawezi kuwa na upeo wa kuchambua mambo zaidi ya hapo,cha msingi tu CHADEMA wajitazame upya na kuona kama ni mtu sahihi wa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama taifa.
 
Kirikou Wa Kwanza

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2013
Messages
3,408
Likes
1,441
Points
280
Kirikou Wa Kwanza

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
Joined May 24, 2013
3,408 1,441 280
Uzi kama huo Chadomo, huwa hawataki kabisa kuuskia.
 

Forum statistics

Threads 1,272,606
Members 490,036
Posts 30,455,044