Huyu ndiye Mh. KAGASHEKI

Kenge (Eng)

JF-Expert Member
Dec 7, 2006
543
156
Wana JF nimesikia kupitia radio KASIBANTE (iliyoko Bukoba) ya huyu Bwana "live" wakati akiwahutubia watu waliokusanyika katika kufunga wiki ya shehere za miaka 33 ya CCM. Yafuatayo ni baadhi ya matamshi yake:

1. Siko tayari kuona mtu eti anakuja kugombea jimbo hili
2. Kwa nini nisiwe mgombea pekee
3. Nimewekeza hapa si nanyi mnaona, iweje mtu aje kuleta vurugu hapa.
4. Atakufa mtu hapa!
5. Wananchi msikubali mtu kuweka jina hata kwenye kura za maoni.
6. Chama ni kimoja na mimi nipo sasa mwingine wa nini, atakufa mtu hapa!

Yapo mengi namba mlio na uwezo wa ku access speach yake yote muiweke hapa tuone huyu bwana ni kizazi gani.

Mie namuona kwa mtazamo tofauti kutokana na heshima aliyonayo ila kwa matamshi haya huyu anaweza akawa nduguye HITLER.

Achilia mbali usumbufu waliowapa wasafiri wengine waliokuwa wanatumia barabara iliyofungwa na maandamano ya wafuasi wake kwa zaidi ya masaa mawili wakati wanatoka kwenye mkutano.

Inashangaza jana mikutano mingi wageni rasmi walikuwa wabunge badala ya viongozi wa chama na wengi walitoa matamshi kama ya huyu bwana.

Inaashilia nini?
 
Inashangaza jana mikutano mingi wageni rasmi walikuwa wabunge badala ya viongozi wa chama na wengi walitoa matamshi kama ya huyu bwana.

Inaashilia nini?
Hana tofauti na Mbunge Kamala wa Jimbo la Nkenge, naye nasikia hahitajiki tena.
 
kama yupo kijana ambaye ni below 36 nitamsupport aende akamngoe huyu
Siasa za Kanda ya Ziwa ni ngumu! Nilioyaona Busanda na Biharamulo.

Kuna baadhi ya waheshimiwa ni miungu watu, wamejipigilia misumari, ukijumlisha na siasa za matabaka, koo na ukabila, kazi ipo tena kubwa! Huko sio siasa za chama wala sera, huko ni sura!.
 
unasema siasa za KANDA? njoo JF uone jinsi the so called GREAT THINKERS walivyo kuwa obsessed na WAZEE ambao if anything after 40 yrs tuko kule kule

its really sad lakini you know what? wacha watulalamikie lakini sisi wengine tutaendelea na hii kampeni ya kutaka mabadiliko not kwa sababu ya umri tuu lakini si vibaya tukabadili huu mvinyo

personally anyone under 36 should be given a chance
 
Mimi nilisikia. Nilishangaa na sijawaelewa sisiem Kagera kwa jumla kama ni chama cha wananchi kweli au ni chama cha watu binafsi wanaoitwa wabunge.

Hata hizo sherehe za jana zilikuwa ni mipango ya wabunge na hayo maandamano yalijaa mabango yanayomzungumzia Kagasheki na si chama. Mhhh.

Huyu bwana kila kitu anajisifia yeye na si chama. Kitu nisichojua ana wasiwasi gani katika kugombea kwake kama aliyoyafanya ni mazuri? Siku hizi kila siku anaita makundi mbalimbali na ku host viparty kisha anawahonga. Alifanya hivyo kwa wachungaji. Alifanya hivyo kwa mabalozi wa nyumba kumi na alifanya hivyo kwa makatibu wa chama chake kwa kuwahonga simu za nokia kila mmoja ikiwa na line ya zain.

Gari za kubebea wagonjwa zilizotolewa na UN alipita kwenye kata akijaribu kusema ni yeye kazitoa kama zawadi. Haya bwana!

Moja ya mambo yanayonishangaza ni kwamba hata viongozi wengi wa sisiemu hapa hawakuwa naye katika maandamano haya ila zile sura zinazopata mlo toka kwake hizo ndizo zilisheheni.

Ngoja tusubiri tuone!
 
Wakuu jana niliona maandamano ya sisiem Bukoba na nilishangaa sana maana mabango yote na matangazo ya magari yalikuwa yakizungumzia Kagasheki na nimebaki nikijiuliza hivi bila Kagasheki sisiemu hakuna Bukoba? Je sisiemu imebaki ni mali miliki ya watu kumbe siku hizi?
Jambo hili limepunguza hata wingi wa wana sisiemu wenyewe katika maandamano ya chama chao.

Ilikuwa ni aibu kuona wanasisiemu kidogo hivyo katika maandamano ya chama chao yaliyofanyika jumamosi saa 7 mchana wakisheherekea siku ya kuzaliwa kwa chama. Tulizoea kuona watu wengi lakini kama hawa ndio wanachama wanaochangamkia chama! basi kwishney.

Wengi ni akina mama nao wamepungua sana ukichukulia na miaka iliyopita.

Angalieni picha hizi!

i1680_IMGP2024.jpg

i1681_IMGP2025.jpg

Kagashi enzi za kampeni 2005 alidai tena zaidi ya mara moja hadharani kuwa atabadilisha hospitali ya mkoa kuwa ya rufaa na kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa bukoba....mambo hayo kakeleza? kama bado ni mnafiki na hapaswi kuchaguliwa tena pamoja na vijisenti vyake!
 
naomba ufafanuzi,
je alisema atajenga hiyo hospitali na uwanja wa ndege
kwa pesa zake za mfukoni au kwa pesa kutoka wapi?
 
umetoa hukumu kwa maneno ya kusikia tuu? kazi kweli kweli

mkuu you may need to find a proper vocabulary sijaona hukumu hapo! nimeona unverified statement that need verification from anyone including you. say what you know
 
- Kampeni za siasa hizo, sasa ni vyema mpinzani wake katika ubunge akatumia maneno yake huyu goi goi kumuadhibu nayo, maana sitaki kuamini kwamba wananchi wa huko ni magoi goi kama huyu mbunge na watamruhusu kurudi tena bungeni!

- By the way, toka awe mbunge amewafanyia nini tofauti na kabla hajawa ndilo swali la msingi, regardless of what he said!

Respect.

FMEs!
 
unasema siasa za KANDA? njoo JF uone jinsi the so called GREAT THINKERS walivyo kuwa obsessed na WAZEE ambao if anything after 40 yrs tuko kule kule

its really sad lakini you know what? wacha watulalamikie lakini sisi wengine tutaendelea na hii kampeni ya kutaka mabadiliko not kwa sababu ya umri tuu lakini si vibaya tukabadili huu mvinyo

personally anyone under 36 should be given a chance

Khe.. Ndugu yangu January.. mbona humwambii baba yako aachie ngazi??
 
mkuu you may need to find a proper vocabulary sijaona hukumu hapo! nimeona unverified statement that need verification from anyone including you. say what you know

kwa mtazamo wangu haya maneno yenye nyekundu ni hukumu. hata hivyo wataalamu wa lugha wanaweza kutoa neno linalofaa zaidi katika hiyo sentensi

Hana tofauti na Mbunge Kamala wa Jimbo la Nkenge, naye nasikia hahitajiki tena.
 
unasema siasa za KANDA? njoo JF uone jinsi the so called GREAT THINKERS walivyo kuwa obsessed na WAZEE ambao if anything after 40 yrs tuko kule kule

its really sad lakini you know what? wacha watulalamikie lakini sisi wengine tutaendelea na hii kampeni ya kutaka mabadiliko not kwa sababu ya umri tuu lakini si vibaya tukabadili huu mvinyo

personally anyone under 36 should be given a chance

GT,hivi unaweza kutusaidia kubainisha MZEE ni mtu mwenye umri gani?Na kuna uthibitisho wowote wa kimazingira na kisayansi kuwa UJANA ni chanzo cha uongozi bora?

Anyone under 36 should be given a chance?Hata kama hana uwezo wa kujiongoza yeye mwenyewe?

Tunachohitaji ni wazalendo wenye uchungu na nchi regardless ya ujana au uzee wao.Nafahamu fika kuwa kwa mchambuzi mzuri kama wewe una mifano luluki kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni inayoonyesha watu wanaobadili jamii zao na hata dunia kwa ujumla licha ya umri wao mkubwa.

Steven Jobs,Richard Branson,Rupert Murdoch na wengineo ni over 36....
 
Wabunge wa CCM wanamatatizo!kwani yeye anamkataba na MUNGU kwamba ni yeye tu ndie anyefaa kwenye hilo jimbo?
 
These type of politics zinafaa kwa watu wasiosoma na mwisho wake upo karibu. Huyu anadanganya watu...
 
naomba ufafanuzi,
je alisema atajenga hiyo hospitali na uwanja wa ndege
kwa pesa zake za mfukoni au kwa pesa kutoka wapi?
Kwa wakazi wa bukoba hilo wanalijua mkuu, tena si kificho ndo ilikuwa giya yake... anaanza mamboooooo...wapambe: bomba...anarudia: bomba?..eeh! Inafuatia ahadi zake hizo kuu na alikuwa akitamba kweli kweli kuwa amekaa umoja wa mataifa siku nyingi ana watu na marafiki wa kushirikiana kufanya hilo....Naamini wapo wana JF tokea bukoba humu waweza thibitisha nisemayo mkubwa.......
 
Saitama-kein umenikumbusha,huyo jamaa ndivyo ambavyo amekuwa akifanya,niikuwepo huko likizo ya xmass na mwaka mpya,wanamwita Swahiba,alikuwa busy kwenye ukumbi wa kanisa pale Franscica,vikao visivyoisha,baadhi ya wajumbe nilipowauliza mbona wanapoteza muda kwenda kuhudhuria mikutano isiyo na tija,walinijibu kwamba mwisho wa kikao kuna bahasha....kazi kwelikweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom