Huyu ndiye mgunduzi wa magari aina ya BENZ

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
Karl Friedrich Benz alizaliwa tar. 25 Novemba 1844 akiitwa Karl Friedrich Michael Vaillant huko Mühlburg / Karlsruhe Ujerumani wa Kusini Magharibi.
430dedc5303ffb8d0ee3d4e41556e2b6.jpg

Baada ya kumzaa mamake Josephine Vaillant akaolewa na babake Johann Georg Benz. Hivyo akaitwa Karl Friedrich Michael Benz lakini baadaye akajiita Carl Friedrich Benz .
Alikuwa mhandisi Mjerumani mwenye sifa ya kuwa alitengeza motokaa ya kwanza au gari la kwanza lililotumia nguvu ya nishati ya petroli .
Mwaka 1864 alichukua digri ya uhandisi , mw. 1871 alianzisha kampuni yake ya kwanza.
edccceb34a3d1b22812620db5f5c0a4f.jpg
Hapo alitengeneza injini ya petroli ya mapigo mawili mwaka 1878/79 aliyoendeleza kuwa injini ya
mapigo manne .
7565e6b37d482a00025c3980d6f66b93.jpg

Injini aliyotengeneza

Benz hakuwa mhandisi wa kwanza kutengeneza injini za aina hii, Mjerumani mwenzake Nikolaus Agosti Otto aliwahi kuchukua hataza ya injini ya mapigo manne mwa. 1876. Injini za aina hii zilifanya kazi viwandani vikiendesha mashine mbalimbali.
1886 Benz alikuwa mtu wa kwanza aliyeweka injini ya petroli kwa gari. Gari lake la kwanza lilikuwa na magurudumu matatu yenye nguvu-farasi 0.8.
a730c011c0de9633c0b14c980f91d68e.jpg

Mke wake Bertha Benz alifanya safari kubwa ya kwanza kwa gari hili kwa umbali wa km 89 kutoka Mannheim kwenda Pforzheim (yote Ujerumani wa Kusini Magharibi). Alipoishia petroli alipaswa kuinunua katika duka ya madawa kwani hapakuwapo na kituo cha petroli bado.
Benz aliendelea kutengeneza gari lenye magurudumu manne. Kwa jina la "Velo" lilikuwa motokaa ya kwanza iliyotengenezwa kwa wingi duniani.
Benz aliona kupanuka kwa biashara yake watoto wake wakiendelea kuendesha makampuni yake. Mwaka 1926 kampuni ya Benz iliunganishwa na kampuni ya Gottlieb Daimler kwa jina la " Daimler-Benz ".
Karl Benz aliaga dunia tar. 4 Aprili 1929 .
8f850acb2810d608a6a6b05d5ea4bf68.jpg

Leseni ya kwanza ya udereva

12f36299a32aec19fce283a4495e958d.jpg

Makumbusho ya Benz
 
Habari
"Jandaruma"
Unapenda documentary za ugunduzi wa mambo mbalimbali..?
Fanya hivi..
Ingia you tube search kipindindi kinaitwa SCIENCE QUIRKY kinachorushwa kwenye Televishen ya Da Vinvi Learning ujionee gunduzi mbalimbali za Tecnology..

Aksante:)
Aisee! hebu nitafutie historia ya mvumbuzi wa ndege
 
Ona sasa. Mtoto ambaye hamjui baba ndio kaleta mambo mazuri hivi. Maana mama yake alizaa kwanza ndio akapata mme
 
Karl Friedrich Benz alizaliwa tar. 25 Novemba 1844 akiitwa Karl Friedrich Michael Vaillant huko Mühlburg / Karlsruhe Ujerumani wa Kusini Magharibi.
430dedc5303ffb8d0ee3d4e41556e2b6.jpg

Baada ya kumzaa mamake Josephine Vaillant akaolewa na babake Johann Georg Benz. Hivyo akaitwa Karl Friedrich Michael Benz lakini baadaye akajiita Carl Friedrich Benz .
Alikuwa mhandisi Mjerumani mwenye sifa ya kuwa alitengeza motokaa ya kwanza au gari la kwanza lililotumia nguvu ya nishati ya petroli .
Mwaka 1864 alichukua digri ya uhandisi , mw. 1871 alianzisha kampuni yake ya kwanza.
edccceb34a3d1b22812620db5f5c0a4f.jpg
Hapo alitengeneza injini ya petroli ya mapigo mawili mwaka 1878/79 aliyoendeleza kuwa injini ya
mapigo manne .
7565e6b37d482a00025c3980d6f66b93.jpg

Injini aliyotengeneza

Benz hakuwa mhandisi wa kwanza kutengeneza injini za aina hii, Mjerumani mwenzake Nikolaus Agosti Otto aliwahi kuchukua hataza ya injini ya mapigo manne mwa. 1876. Injini za aina hii zilifanya kazi viwandani vikiendesha mashine mbalimbali.
1886 Benz alikuwa mtu wa kwanza aliyeweka injini ya petroli kwa gari. Gari lake la kwanza lilikuwa na magurudumu matatu yenye nguvu-farasi 0.8.
a730c011c0de9633c0b14c980f91d68e.jpg

Mke wake Bertha Benz alifanya safari kubwa ya kwanza kwa gari hili kwa umbali wa km 89 kutoka Mannheim kwenda Pforzheim (yote Ujerumani wa Kusini Magharibi). Alipoishia petroli alipaswa kuinunua katika duka ya madawa kwani hapakuwapo na kituo cha petroli bado.
Benz aliendelea kutengeneza gari lenye magurudumu manne. Kwa jina la "Velo" lilikuwa motokaa ya kwanza iliyotengenezwa kwa wingi duniani.
Benz aliona kupanuka kwa biashara yake watoto wake wakiendelea kuendesha makampuni yake. Mwaka 1926 kampuni ya Benz iliunganishwa na kampuni ya Gottlieb Daimler kwa jina la " Daimler-Benz ".
Karl Benz aliaga dunia tar. 4 Aprili 1929 .
8f850acb2810d608a6a6b05d5ea4bf68.jpg

Leseni ya kwanza ya udereva

12f36299a32aec19fce283a4495e958d.jpg

Makumbusho ya Benz
Jina la Mercedes Benzi llilitokana na nn??
 
Back
Top Bottom