Huyu Ndiye MAGUFULI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu Ndiye MAGUFULI

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Steph Curry, Sep 23, 2015.

 1. Steph Curry

  Steph Curry JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2015
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 5,672
  Likes Received: 2,132
  Trophy Points: 280
  Tafadhali Mods naomba msiunganishe wala kuufuta huu uzi.. Tuacheni tujadili mambo kwa uwazi..

   
 2. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2016
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,442
  Likes Received: 3,693
  Trophy Points: 280
  ebana daah!
   
 3. kopites

  kopites JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2016
  Joined: Jan 28, 2015
  Messages: 4,898
  Likes Received: 4,144
  Trophy Points: 280
  Yaani view ni 1064 lakini comment ni 2 tu!...ebana watu washachoka aisee hawana hamu
   
 4. minji

  minji JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2016
  Joined: Sep 2, 2016
  Messages: 1,466
  Likes Received: 1,582
  Trophy Points: 280
  Mmmh
   
 5. Justine_Dannie

  Justine_Dannie JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2016
  Joined: Dec 1, 2014
  Messages: 1,211
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hatujachoka bali tunamuogopa
   
 6. The Great Emanuel

  The Great Emanuel JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2016
  Joined: Apr 3, 2015
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1,967
  Trophy Points: 280
  Naziona m7 zileeee uchochezi huu shauri yako.
   
 7. tejay

  tejay JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2016
  Joined: Dec 26, 2015
  Messages: 1,003
  Likes Received: 560
  Trophy Points: 280
  Hayaa
   
 8. kopites

  kopites JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2016
  Joined: Jan 28, 2015
  Messages: 4,898
  Likes Received: 4,144
  Trophy Points: 280
  Ndo hivo!..mliyataka wenyewe haya kuishi kama swala porini kwa hofu!..miaka 5 ya kuishi kwa hofu hii sasa!..nchi tungempa mzee wetu tu ingetulia bila wasiwasi.
   
 9. Diva Beyonce

  Diva Beyonce JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2016
  Joined: Mar 6, 2014
  Messages: 12,953
  Likes Received: 6,064
  Trophy Points: 280
  Ni kweli juma ponda Mali ana kisasi, anapenda kukomoa hana utu plus roho mbaya hivi kanisani huwa anaenda kufanya nini loh
   
 10. G

  Gojaga Nize JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2016
  Joined: Jul 1, 2015
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,325
  Trophy Points: 280
  Leo kuna dogo kaja ofisini wakati namuhoji ili nimuhudumie akawaananijibu nyodo. Nilidhamilia huyu dogo lazima arudi kwao maana hawezi kumchezea ofisa wa chuo kikuu hivihivi.

  Baada ya kama masaa mawili nikiwa na hasira, nilijihoji huyu dogo hata nikimfanyia figisu arudi kwao nitamuumiza bure tu.

  Nimeamua kumsamehe. Sina kisasi tena moyoni. Kwani hapa mnajadili mambo ya visasi?
   
 11. Sky Eclat

  Sky Eclat JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2016
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 23,749
  Likes Received: 62,928
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa ni msomaji zaidi kuliko mchangiaji kwa muda mrefu lakini nimekuwa nikishangaa sana watu wanapokuwa wanaongea vitu wasivyovielewa ama kwa ushabiki au kwa kutokuelewa.

  Mfano watu wameandika sana kuhusu uwezo wa Dr John Pombe Magufuli kuwa anafaa kuwa rais wa jamhuri ya muungano watanzania kwa kutumia vigezo dhaifu sana kuwa kila anapopewa Wizara hufanya vizuri nafikiri hicho si kigezo tosha kabisa cha mtu kuwa rais.

  Kwa wasio mjua Mh. Magufuli nilitaka leo wamfahamu kwa ufupi tu kidogo ili na wao wapime kama kweli anafaa kuwa kiongozi wa nchi katika nafasi kubwa kama ya urais.

  Magufuli ni mtu mwenye visasi sana na yu tayari kuumiza Umma wa watu katika kulipa visasi kwa wasio mjua Mh. Magufuli alipata kugombea Ubunge jimbo la Biharamulo mara mbili bila kupita mara zote aliangushwa na kina marehemu Phares Kabuye kwa kura nyingi sana .

  Aliweza kupata Ubunge pale tu wilaya ya biharamulo ilipogawanywa majibo mawili yaani Biharamulo Magharibi na Biharamulo mashariki Hivyo akafanikiwa kuin gia bungeni kwa rushwa kubwa sana na kuwa mbunge wa Biharamulo mashariki wakati upande wa Biharamulo magharibi akiwa Mh. Choya.

  Baada ya kupata Ubunge Aliapa kiapo kama atahakikisha Biharamulo mashariki inakufa, kipindi hicho Magufuri alipata Naibu Waziri hivyo alitumia nafasi hiyo kuivuruga Halmashauri ya Biharamulo na na kwa influence miradi yote mikubwa ya Wilaya ikawa inaenda jimboni kwake moja kwa moja bila hata kupitia Halmashauri watu wote walitishwa makao makuu ya wilaya na hakuna aliyeweza kusema lolote kama manakumbuka vizuri alifikia kugombana na Mbunge mwenzake wa mashariki aliyefikia kusema kama magufuri anatumia uwaziri wake kumhujumu jimboni mwake (kitendo kilicahomluudihi sana magufuri na kuhakikisha nakufanikisha Mh.Choya anadondoka ktk ubunge wa Biharamulo Magharibi.

  Alifikia kuwa analeta wageni wakitaifa direct Jimboni kwake hata bila kupitia Makao Makuu ya Wilaya lakini nia ikiwa ni kiapo alichokiweka kuwa lazima ataiua biharamulo Magharibi kwa kumnyima Ubunge mara mbili hapa nataka kuwaonyesha kiongozi huyu mcheshi mchapa kazi lakini mwenye visasi vyenye kuleta maafa kwa wazee wanawake na watoto.

  Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa Umma?

  Mwaka uliofuatia mheshimwa Magufuli alipita bila kupingwa baada mgombea mwingine aliyekuwa tishio kwake (jina nalihifadhi) kufanyiwa mizengwe wakati wa kurudisha form mpokea form alijificha na alijitokeza wakati mda wa kurudisha form umekwisha akaonekana mrudisha form amerudisha form too late lakini Mh. Magufuli alikuwa ameisha watisha viongozi wa chama na serikali Wilayani Biharamulo atakaepokea form za Bwana huyo basi yeye ni Naibu Waziri atahakikisha hana kazi watu wakatii na wakafanya dhuruma ya kumpitisha Magufuli bila kupingwa.Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

  Mwaka 2005 kijana mdogo anaitwa nahifadhi jina lake kupitia chama cha CUF ambaye alikuwa katibu wa wilaya wa CUF Wilayani Biharamulo alichukuwa form kugombea jimbo la biharamulo mashariki kwa Magufuli huku akiwa na suport kubwa sana ya vijana na alikuwa anaenda kumwamgusha Mh. Magufuli katika kinyanganyiro hicho, alichofanya Mh. Magufuli alimteka kijana huyo na kumpakia kwenye gari hadi mwanza kutoka mji mdogo wa Buseresere walimpelekea mke wa huyo bwana pesa wakampatia simu aongee na mme wake wakimshawishi waende hadi Mwanza wampatie pesa aondoe jina kwani pesa kidogo ya matumizi wameishamwachia mke wake yule bwana.

  Alipofika Mwanza akapandishiwa dau hadi milioni 60 akubali kutorudisha form za Ubunge ikiwa hapo imebaki siku 4 kabla form kurudishwa kijana akakabidhi form zake kwa Magufuli wakaenda nae hadi bank kijana kabaki kwenye bench Mh. Waziri akaingia ndani akatoka akamwambia account yake pale haina pesa waongozane hadi Dar es salaam.

  Wakapanda ndege hadi Dar kijana akafikishiwa kwenye 3 star hotel kwa bili ya mheshimiwa siku tatu bila kuonanana Mh. Magufuli.

  Siku ya nne kijana anaona kwenye TV Magufuli amepita bila kupingwa akashtuka kaulizia hadi ofisini kwa waziri kafika akakaribishwa Mh. kama hamjui akamuuliza shida yako nini akasema nipe pesa zangu mh. akamwambia unakuja kuniomba rushwa nikuachie ubunge wewe kijana huna adabu kabisa.

  Mkifuatilia CUF, hiki kisa wanakijua vizuri kwani walipelekewa taarifa kama kuna mgombea wao ameenda kuuza ubunge kwa Magufuli ikabidi Green GUARD ya CUF iende kum-arrest na kumpeleka Buguruni makao makuu na kurudi Biharamulo kwa aibu kubwa lakini baadae alimtafutia kazi kwenye mgodi huko Tulawaka anafanya kazi kumziba mdomo kwa sababu kijana alikuwa ameapa kumfanyizia.

  Huyu ndiye Magufuli, je anaweza kuwa kiongozi wa nchi katika uhuni wa namna hii?

  Sinema ya Magufuli haiishi hapo; kile kiapo chake cha kulipa kisasi Biharamulo Magharibi kiliendelea alipolazimisha kupindisha barabara ya lami kuingia Chato toka Mwanza kwenda Bukoba kupitia Biharamulo makao makuu ya wilaya akaipindidhia Chato nyumbani kwake na kuua makao makuu ya wilaya ya Biharamulo. Huyu ndiye kiongozi anayeweza kuongoza watu?

  Mh. Magufuli alipigana na kulobby kwa nguvu zote kuhakikisha Chato inakuwa wilaya ili Biharamulo Magharibi wasifaidi mapato ya ziwa ambalo yanapatikana upande wa Chato na Nyamirembe na ndiyo kilichokuwa chanzo kikuu cha mapato cha wilaya ya Biharamulo lengo ikiwa ni katika kuendelea kulipa visasi kwa nini upande wa magharibi walikuwa hawampi kura kwa mihura takribani miwili alifaulu na Chato ikawa wilaya mpya toka Biharamulo.

  Alipojikuta amesahau kuwa mgodi wa Tulawaka upo Biharamulo na haupo Chato alianza kuharasi uongozi wa Wilaya ya Biharamulo kuwa ule mrahaba wa mwisho wa mwaka unaotolewa na migodi kwenye halmashauri za wilaya migodi ilipo alitaka Biharamulo igawane nusu kwa nusu mrahaba wake na wilaya ya Chato.

  Huyu ndiye Mh. Magufuli, Je rais anaweza kuwa na tabia hizi chafuchafu namna hii?

  Iliposhindikana akiwa waziri wa ardhi Mh. Magufuli kwa makusudi kabisa alibadilisha mawe ya mpaka kwa amri kama Waziri wa Ardhi kuiingiza Tulawaka ndani ya wilaya ya chato hivyo siku si nyingi Chato itadai Tulawaka ipo kwao na watapola haki ya wana biharamulo swala hili lipo wazi kabisa halmashauri ya Wilaya kupitia baraza la Madiwani limelalamika sana kuhusu ushenzi huu wa Magufuli huyu ndiyo mtu anaweza kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

  Mwaka jana katika mpaka mwingine wa Biharamulo na chato kijiji cha biharamulo kinachopakana na chato huko kata ya Runazi wanakijiji waligundua kuna dhahabu na kuna wachimbaji wadowadogo Mh. Magufuli yupo analazimisha kubadili mipaka ili hiki kijiji kihamie wilayani chato na kumekuwa na mgogoro wa kiutawala unochochewa na yeye Huyu ndiyo Mh. Magufuli anaepigiwa debe humu ndani kama anaweza kuwa rais rais huangaliwa pande zote mafanikio na madhaifu kwangu mimi madhaifu ya magufuri ni mengi kuliko mafanikio mtakumbuka kilio cha nyumba za serikali lakini huyu jamaa mkumbuke ni bingwa wa kusimamia wakandarasi na kutaka viwango kktk ujenzi lakini yote tisa kumi Mh. anajenga ghotofa pale kwake anapoishi Osterbay yeye nendeni mkaone maajabu ya mussa wajenzi mafundi mchundo hata ramani hazijapitishwa sababu wachoraji ni watu wa mitaani na mafundi ni ni vibaruwa mchundo huyu ndiyo Mh. Magufuli.

  Lakini skendo kubwa ya huyu bwana ambayo waandishi wangefuatilia kumjua vizuri ni jinsi alivyochezea mipaka ya Wilaya ya Biharamulo kubadilisha DN za vijiji na kusogezwa mawe yalioizinishwa na serikali bila hata serikali kujua kuzipeleka Chato hii ni hujuma kubwa na anastahili kujiuzulu waandishi nendeni mkawahoji wananchi na viongozi wa wilaya biharamulo mjue huyu mtu kitu alichofanya mtu namna hii hawezi kuwa kiongozi kabisa .

  Huko jimboni kwake wafanyakazi wa serikali wote walio against naye amewaumiza sana wengine hata kufunga vibiashara vyao vidogovidogo ili tu wakubaliane naye kifupi hajawahi kupita bila kupingwa ila amekuwa akipita kwa hila kubwa.

  Naomba kuwakilisha ili tumpime kwa pamoja. Je, tabia hizi zinaweza kumpa urais kweli?

  TUMPIME KWA PAMOJA HAYO NI MAONI YANGU TU.
   
 12. m

  mg4 Member

  #12
  Sep 2, 2017
  Joined: May 21, 2017
  Messages: 54
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 25
 13. jingus

  jingus JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2017
  Joined: Nov 17, 2013
  Messages: 338
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Unafaaa kuwa mgombea 2020

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 14. Buobaty

  Buobaty JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2017
  Joined: Jul 26, 2017
  Messages: 315
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 80
 15. n

  ngonza JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2017
  Joined: Sep 29, 2014
  Messages: 318
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...