Huyu ndiye kijana aliyepoteza maisha kwenye mvutano baina ya police na CHADEMA

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Hapo awali ilielezwa kuwa wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisitiza kufanya maandamano leo kisha mkutano mkubwa wa hadhara, kuliibuka mvutano baina yake na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kufuatia Kamanda wake, Faustine Shilogile kupiga marufuku mandamano hayo.

Kamanda Shilogile alieleza sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa ni udogo wa barabara za Morogoro na kwamba leo ni siku ya kazi hivyo yanawezesha kusababisha usumbufu kwa wakazi wa mji huo.

Wakati Shilogile akieleza kuzuia maandamano yanayotarajiwa kuanza saa 5 asubuhi, Mkuu wa Operesheni Sangara, Benson Kigaila, alisisitiza kuwa watafanya maandamano kwa kuwa waliskubaliana na Kamanda Shilogile kabla ya kuwageuka.

Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe la 27 August 2012, ilielezwa kuwa Kamanda Shilogile alidai kuruhusu baiskeli na watu kutumia barabara kwa sababu ya mikutano ya Chadema itakuwa ni kuwanyima haki wananchi wengine, na hivyo wataruhusu watu wasiozidi 50 kupita kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ishara ya kuonyesha kama wanaelekea katika maandamano.

Pichani ni kijana aliyeelezwa kupigwa risasi kichwani katika tafrani hizo na baadae kupoteza maisha Ametambulishwa kwa jina la Ally Zona, ambae alikuwa ansoma magazeti katika stendi ya Msamvu. Tukio hili lilitokea mapema leo asubuhi kuelekea saa sita mchana wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi hao wa chadema. Mtoa taarifa anasema Polisi wanadaiwa kutumia risasi za moto pamoja na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamani hao.

Watu wengine waliojeruhiwa katika tafrani hiyo wameelezwa kuwa ni mwenesha baiskeli Hashim Seif ambae amejeruhiwa kwa risasi mguuni akiwa napita na baiskeli yake na kijana mwingine aliielezwa kuwa ni muuza matunda Frank Valimba ambae amejeruhiwa na risasi tumboni.

JUMANNE, AGOSTI 28, 2012 05:52 NA ARODIA PETER, MOROGORO

kigaila%20akamatwa.jpg

Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila (katikati), akidhibitiwa na polisi wakati wa maandamano ya wafuasi wa chama hicho mkoani Morogoro jana.

*Wampiga risasi kichwani muuza matunda akisoma gazeti
*Vijana wawili wajeruhiwa, wakimbizwa hospitalini
*Chadema wakutana na polisi kujadili matukio hayo

ASKARI polisi mjini hapa, jana walimuua kwa risasi kijana mmoja, Ally Zona (22) wakati walipokuwa wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Taarifa zilizopatikana zinasema kuwa, wakati Zona anapigwa risasi, alikuwa akiuza matunda katika eneo lake la biashara lililoko eneo la Bene Msamvu.

Mbali na Zona kupigwa risasi, vijana wengine wawili waliotambuliwa kwa majina ya Ashim Seif na Frank Valimba, walijeruhiwa vibaya kwa risasi na wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Matukio hayo yalitokea jana saa saba mchana, wakati baadhi ya wananchi walipojikusanya katika eneo la Bene Msanvu, kwa ajili ya kuanza maandamano kuelekea eneo liitwalo Kiwanja cha Ndege.

Ndugu yake Zona, Hamisi Mlewa (22), aliliambia MTANZANIA kuwa, kaka yake alipigwa risasi na polisi wenye silaha waliokuwa kwenye magari wakizunguka kuzuia maandamano ya wafuasi wa CHADEMA.

Kwa mujibu wa Mlewa, Zona alipigwa risasi kichwani alipokuwa katika biashara zake akisoma gazeti.

"Karibu na biashara ya marehemu, kulikuwa na muuza magazeti, sasa kwa kuwa marehemu amezoeana na muuza magazeti huyo, alikuwa akisoma gazeti na hakuwa katika maandamano ya CHADEMA.

"Yaani kila mmoja anashangaa kitendo cha polisi kutumia nguvu kubwa kwa mtu ambaye alikuwa kwenye biashara zake," alisema.

Majeruhi waliojeruhiwa kwa risasi, Valimba na Seif, walipokuwa wakizungumza na MTANZANIA kwa shida katika hospitali hiyo, walisema wameshangazwa na polisi kuwajeruhi bila hatia.

Katika tukio hilo, Valimba ambaye alijeruhiwa kwa risasi ubavuni karibu na kiuno, alisema yeye ni mfanyabiashara wa ndizi na karoti katika Kituo cha Mabasi cha Msanvu.

"Sikuwa jirani kabisa na eneo ambalo watu walitaka kuandamana, maandamano yalikuwa eneo la Rupira kuelekea njia ya uhamiaji, wakati mimi nilikuwa Msamvu nikiendelea na biashara, mpaka sasa sijui ni kwa nini polisi waliamua kunijeruhi, sina la kusema namwachia Mungu," alisema Valimba.

Naye Seif, alisema alipigwa risasi mguuni wakati akiwa anaendesha baiskeli eneo la Mafisa, kuelekea mjini.

Polisi wasindikiza maandamano
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi na wananchi kuendelea na maandamano bila woga, polisi waliamua kusindikiza maandamano hayo hadi katika viwanja vya mkutano.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilisema kuwa, askari hao waliamua kusindikiza maandamano hayo baada ya taarifa za mauaji kuzagaa katika Mji wa Morogoro.

Katika mitaa mbalimbali ya Mji wa Morogoro hasa hasa eneo la Nanenane, makundi ya wananchi yalionekana kuendelea na maandamano kuelekea viwanja vya mkutano.

Kutokana na matukio hayo, Lissu alisema katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiwanja cha Ndege, kwamba uongozi wa CHADEMA ulikutana na viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ili kujadili matukio hayo.

Alisema kuwa, baada ya mjadala kumalizika, walikubaliana iundwe Kamati ya Kitaalam itakayoongozwa na Dk. Mataka wa jijini Dar es Salaam, ambaye ni mtaalam wa masuala ya vifo vyenye utata.

Katika kamati hiyo, alisema familia ya marehemu itateua mtu mmoja atakayekuwa katika kamati hiyo na kwamba CHADEMA wamesema mwili wa marehemu hautazikwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

Wakati huo huo, alisema amri ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, ndiyo iliyosababisha mauaji na majeraha kwa vijana hao.

"Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, maandamano hayajawahi kuwa kosa la jinai kama ambavyo polisi wamefanya.

"Namwambia Kamanda Shilogile, haya mauaji ya raia wasio na hatia ambayo ameyafanya leo (jana), ipo siku atakuja kuyajibu hadharani mbele ya Watanzania.

"Nakwambia Kamanda Shilogile, damu ya Watanzania haitamwagika bure, ipo siku tutakufuata ulipo, iwe umevaa unifomu au kiraia, tutakusimamisha mbele ya wananchi, ili ujibu kile ambacho umekifanya leo," alisema Lissu.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na awape nguvu na faraja familia yake, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu kwao~AMEN.
 
Life is one big road with lots of signs. So when you riding through the ruts, don't complicate your mind. Flee from hate, mischief and jealousy. Don't bury your thoughts, put your vision to reality. Wake Up and Live!

Mbona napata picture ya ajabu.Kama CCM wanahubiri kuwa CDM ni ya Kikristu.Mbona waliomwaga damu yao,kwa ajili ya ukombozi wa taifa kupitia CDM ni waislam?Angalau toka katika majina na wanaowaua ni machinery ya serikali?
(Arusha,Igunga,Morogoro)
 
Shida watu wakiambiwa hawachanganyi na zao na ndio maana mauaji ya kijinga yanatokea.wao wanadhani wanaidhoofisha CDM kumbe ndio wanachangia kuiimarisha..
 
Heading siyo hiyo:

HUYU NI KIJANA ALIYEUAWA NA POLISI AKITIMIZA HAKI YAKE YA KIKATIBA

Habari kama ni sahihi inasema:Pichani ni kijana aliyeelezwa kupigwa risasi kichwani katika tafrani hizo na baadae kupoteza maisha Ametambulishwa kwa jina Ally Zona, ambae alikuwa anasoma magazeti katika stendi ya Msamvu.

They have done this before, we did let them get away with it! They have done it again, they will do it again!
Kaka, damu yako itanyweshea mti wa uhuru. Matunda yake watakula watoto wako na wa ndugu zako. Aluta continua.
 
Kwanza nawasalimu kwa jina la M4C, ndugu zangu masikini never give up. Najua wengi tunawindwa, wakati wao wapo chini ya ulinzi wanalindwa. Waambieni tukichoka watasanda hao mamwela. Waambieni hata sisi tumechoka mbovu. Waambieni hatuna mkia wa kufyata. Waambieni hatuna chuki bali ukweli ndo una matter. Ally zona tunakuombea kwa baba upumzike kwa amani.
 
Mnaambiwa msifanye maandamano mnang'ang'ania, ona sasa, mnapoteza roho za watu kwa ubishi wenu.

Mkiulizwa maandamano ya nini? hamjui!

Hiki chama kifungiwe tu, hakina mwisho wa amani.
 
Ukombozi wa kweli umewadia ,ukiona moyo wa farao unazidi kuwa mgumu jua ya kwamba na anguko lake litakuwa ni kubwa sana. MUNGU akulaze maali pema peponi ndugu ye tu Ally.
 
Mnaambiwa msifanye maandamano mnang'ang'ania, ona sasa, mnapoteza roho za watu kwa ubishi wenu.

Mkiulizwa maandamano ya nini? hamjui!

Hiki chama kifungiwe tu, hakina mwisho wa amani.

Kweli wewe ni Zo.mbie kabisa!
 
[h=3][/h]

Hapo awali ilielezwa kuwa wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisitiza kufanya maandamano leo kisha mkutano mkubwa wa hadhara, kuliibuka mvutano baina yake na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kufuatia Kamanda wake, Faustine Shilogile kupiga marufuku mandamano hayo.

Kamanda Shilogile alieleza sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa ni udogo wa barabara za Morogoro na kwamba leo ni siku ya kazi hivyo yanawezesha kusababisha usumbufu kwa wakazi wa mji huo.

Wakati Shilogile akieleza kuzuia maandamano yanayotarajiwa kuanza saa 5 asubuhi, Mkuu wa Operesheni Sangara, Benson Kigaila, alisisitiza kuwa watafanya maandamano kwa kuwa waliskubaliana na Kamanda Shilogile kabla ya kuwageuka.

Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe la 27 August 2012, ilielezwa kuwa Kamanda Shilogile alidai kuruhusu baiskeli na watu kutumia barabara kwa sababu ya mikutano ya Chadema itakuwa ni kuwanyima haki wananchi wengine, na hivyo wataruhusu watu wasiozidi 50 kupita kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ishara ya kuonyesha kama wanaelekea katika maandamano.

Pichani ni kijana aliyeelezwa kupigwa risasi kichwani katika tafrani hizo na baadae kupoteza maisha Ametambulishwa kwa jina la Ally Zona, ambae alikuwa ansoma magazeti katika stendi ya Msamvu. Tukio hili lilitokea mapema leo asubuhi kuelekea saa sita mchana wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi hao wa chadema. Mtoa taarifa anasema Polisi wanadaiwa kutumia risasi za moto pamoja na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamani hao.

Watu wengine waliojeruhiwa katika tafrani hiyo wameelezwa kuwa ni mwenesha baiskeli Hashim Seif ambae amejeruhiwa kwa risasi mguuni akiwa napita na baiskeli yake na kijana mwingine aliielezwa kuwa ni muuza matunda Frank Valimba ambae amejeruhiwa na risasi tumboni.
Ama kweli CHADEMA ilaaniwe maana ni janga la kitaifa,sasa kama kamanda aliagiza maandamano no why wao CHADEMA walazimishe maandamano?ningekua na uwezo ili lichama ningelifuta kabisaaaaaa!
 
Mnaambiwa msifanye maandamano mnang'ang'ania, ona sasa, mnapoteza roho za watu kwa ubishi wenu.

Mkiulizwa maandamano ya nini? hamjui!

Hiki chama kifungiwe tu, hakina mwisho wa amani.
CHADEMA ni janga la kitaifa!
 
Back
Top Bottom