Huyu ndiye Hashim Dogo, Msanii bora wa Hip Hop Afrika

Dogo Hashim mimi ninamfahamu zaidi wakati alipoimba track moja ya Tunasonga aliimba na MC Kalapinna. Ni mkali sana wa freestyle namheshimu.
 
Hivi tuwage wakweli tu, huyo Hashim Dogo ukiacha hizo nyimbo 'Shadow of the dark destiny' na 'Tunasonga' alioshirikiana na Pina ana wimbo gani mwingine wa maana kiasi cha kumpaisha hivyo? Mi nikiwaambiaga watu wanaomtukuza huyu mtu wanitumie nyimbo zake nyingine hawatumi wanaishia kusema blaablaa tu. Haya naombeni mnitajie nyimbo nyingine Kali za huyu jamaa ukiacha hizo mbili
 
Hashimu hawezi kuwa mfame hata kidogo halafu tutachekwa kumpa mtu u king hata album hakuwai kutoa.....mnatudhalilisha sana jamii nzima inayofuatilia hiphop...please spare us your.....hii ni aibu siyo tuu kwenu bali kwa hashimu mwenyewe pia. Yeye pia hashimu anajua hilo hawezi kumpa mtu ukng kwa style hiyo
 
Hashim alitoa nyimbo moja tu iliyovuma...namfahamu huyu vzr tumekuwa pamoja maeneo ya Upanga alikuwa anakaa mtaa wa Lugalo kwny magorofa ya madaktari halaf akahamia Ilala
Mkuu taarifa yako si sahihi. Hapo kwenye kuishi Upanga, ghorofa (flat) la madaktari umechanganya habari!
 
Hivi tuwage wakweli tu, huyo Hashim Dogo ukiacha hizo nyimbo 'Shadow of the dark destiny' na 'Tunasonga' alioshirikiana na Pina ana wimbo gani mwingine wa maana kiasi cha kumpaisha hivyo? Mi nikiwaambiaga watu wanaomtukuza huyu mtu wanitumie nyimbo zake nyingine hawatumi wanaishia kusema blaablaa tu. Haya naombeni mnitajie nyimbo nyingine Kali za huyu jamaa ukiacha hizo mbili
Kuna SAA za kazi akiwa na Afro Reign.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom