Huyu ndiye FIRAUNI/FARAO na maajabu ya maiti yake kutokuoza

Mwanzoni mwa miaka ya 1800, mwili huu ulipatikana tena pembezoni kidogo mwa bahari ya Red sea. Hapa sasa Prof Maurice anadai kuwa Ramesses ll, hakufa kwenye Gharika la Mussa kama watu wanavyodai, mwili wake hadi sasa unathibitisha kuwa alikufa akiwa mzee, zaidi ya miaka 80 kwa maradhi ya kawaida. Pia si mwili wa Ramesses ll tu uliopo kwenye makumbusho ya Misri pale mjini Cairo, ni miili mingi ya Mapharao tofauti na baadhi ya watu walioishi kwenye Egypt ya kale.
Hivi hawa waandishi hizi habari huwa mnashindwa kuwahoji ? Hapa nakuuliza wewe swali, mnao ushahidi ya kuwa mwili huo ni wa huyo mnaemzungumzia ?
 
Wamisri wa kale wakipinga kabisa madai hayo na kudai Sese alifariki akiwa na miaka zaidi ya 87 kutokana na maradhi ya kibinadamu. Moja ya ushahidi ni wa mwili wake ambao unaonekana wazi kuwa mtu huyo alifariki akiwa mzee kabisa kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi wa mambo ya kale ulioongozwa na Prof Maurice.
Mbona hamtupi ushahidi ya kuwa huyo ndiyo Remesses II mwenyewe, kinyume chake mnatupigia stori tu.
 
Hadithi za abunuwasi tu
kwa akili tu ya kawaida, kama kweli firauni alisema hayo maneno ni nani aliyeyasikia na kuja kuyasimulia ? hivi kwa mfano mimi ningekuwa ni abiria wa meli iliyozama baharini kabla sijafa niseme maneno fulani alafu nife na abiria wenzangu, nyie huku jamiiforums mtayajuaje hayo maneno ?
 
Wewe leta uthibitisho Firauni hakuwa muislamu?
Hujajibu swali,nimesoma sijaona ndio uniambie sasa,Firauni alikuwa muislamu kivipi ? Nithibitishie hilo.

Usiwe na papara,unachotakiwa hapa kile unachokiongea a kukiandika uwe na elimu nacho na uweze kukijengea hoja,nasubiri uthibitisho ya kuwa Firauni alikuwa Muislamu.
 
Hujajibu swali,nimesoma sijaona ndio uniambie sasa,Firauni alikuwa muislamu kivipi ? Nithibitishie hilo.

Usiwe na papara,unachotakiwa hapa kile unachokiongea a kukiandika uwe na elimu nacho na uweze kukijengea hoja,nasubiri uthibitisho ya kuwa Firauni alikuwa Muislamu.
Kwanini Timu ya Misri wanajiita Mafirauni?
 
Hiyo picha siyo ya Pharao Rameses.. linganisha na hii hapa.. hiyo uliyoweka ni ya albino. Rejea jinsi maalbino walivyokuwa na hila kutaka wao ndo wafahamike kama mafarao.. wakati walikuwa tu vikaragosi enzi za Khemet..

View attachment 1170990
Historia yako ya uongo wakati wa zama za kale watu waliishi miaka mingi sana we unatuambia alikufa na miaka themanini Yan mzee sana acha uongo wakat huo ni kijana tu
 
Historia yako ya uongo wakati wa zama za kale watu waliishi miaka mingi sana we unatuambia alikufa na miaka themanini Yan mzee sana acha uongo wakat huo ni kijana tu
Soma vizuri uelewe dogo.. acha kukurupuka
 
Kuna kitabu kimeandikwa kushoto kulia mwanzo hakijulikani wala katikati story haijulikani imeanzia wapi wala mwisho, kitabu kinamlaani farao kwa kutesa Taifa la Mungu israel lakini kitabu hichohicho wafuasi wake wanawaona waisrael kama mahetani. Hata hivyo huyo mumiani hakuwa hivyo kwa ajili ya laana bali wa misri walikuwa na madawa ya asili ya kuhifadhi miili wa watawala wao.ushahidi kila siku unapatikana kwenye makaburi ya wafalme wa kale
 
Jama jama warumi hadi huku umoo ?

Tumesha zoea zile mada kama family ya drama Bi sandra na wanawe
 
Wana historia wa kisecular huwa wana vituko sana,wakiona jambo limewazidi ukubwa na maarifa basi wana hoji kitoto sana,hii si hoja bali ni wasi wasi tu.

Firauni alizama katika katika kuhaha kwake alisikia akizungunza maneno na huo ndio ushahidi tosha ya kuwa Firauni alikufa na Allah aliye juu aka ahidi ya kuwa ata uhifadhi mwili wa firauni ili watakao fata waone na wapate kujifunza. Lakini swali lina kuja je walio kusudiwa kuuona huo mwili ni kina nani na je ni kweli mwili wa Firauni upo kweli mpaka leo ? Ukweli uko kinyume.

Allah aliye juu anasema katika surat Yunus :

90. Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea!
91. Ala! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa mafisadi!
92. Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu. (Yunus : 90 - 92 )

Nipo ......

Chief naomba nielimishe zaidi; Kwahiyo kwa mujibu wa hiyo aya ni kwamba hakufa bali aliokolewa? Na kama ndivyo then possibility ya yeye kuishi mpaka utu uzima ipo? Lakini swali kuu ni; mwili halisi (the original body) yake ni ipi na iko wapi?
 
kwa akili tu ya kawaida, kama kweli firauni alisema hayo maneno ni nani aliyeyasikia na kuja kuyasimulia ? hivi kwa mfano mimi ningekuwa ni abiria wa meli iliyozama baharini kabla sijafa niseme maneno fulani alafu nife na abiria wenzangu, nyie huku jamiiforums mtayajuaje hayo maneno ?
Aliye simulia Apo si Allah mwenyewe,hakuna kinachojificha kwa Allah,kiwe Cha Siri Wala dhahili

Sent from my Infinix X5516B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom