Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 18,783
- 66,962
Apumzike kwa amani.
Je, wamfahamu mzee Obed Mgongo?Wakurugenzi,
Nilibahatika kuzaliwa kijiji kimoja na Chritopher Kasangatumbo, alikuwa si mbinafsi mjamaa wa kweli, nilibahatika kumjua nikiwa kijana mdogo sana pale kijijini kwetu ipole, alikuwa mzee mpole na kwenye hekma sana; kwenye misiba alikuwa anatumia muda mwingi kutuelimisha, nakumbuka alituambia mambo ya demokrasia na dhana nzima ya vyama vingi kipindi nipo darasa la tatu; sikuielewa philosophy yake hadi nilipofika kidato cha sita na kukutana na kitu kinaitwa vyama vingi (1995) hapo ndipo nikafungua macho na kujua ni nini hasa Kasangatumbo alimaanisha those days.
Kuna tetesi kwamba wale wote waliohoji au kwenda tofauti na mawazo ya mwalimu walipata ban; yule mzee Kasangatumbo alifanyiwa visa vingi sana hadi kufikia kuibiwa ngombe zake zote, Pamoja na kuishi uingeleza lakini hakuwa na mali yoyote ile mbali ya ngombe zisizozidi therathin alizorithi kutoka kwa wazazi wake. Nilibahatika kusoma na watoto wake, nakumbuka hata viatu hawakuwa navyo; tulienda shuleni pekupeku pamoja ingawa wenzangu waliyaonja maisha ya Uingeleza.
Mzee alikuwa mjamaa wa kweli na hilo halina ubishi, tatizo ni kwamba je alikorofishana vipi na mwalimu? Mimi na wewe hatujui, kuishi kijijini ilikuwa ni moja ya adhabu alizopewa toka juu. Kuna kipindi pale Tabora mjini Bendera ya taifa ilikuwa inashushwa, yeye hakusimama, akakamatwa kupelekwa kituo kikuu, pale kituoni akawaambia mapolice kwamba hawezi kuongea ya yeyote yule pale isipokuwa mwalimu tu. Police hawakumpa nafasi hiyo bali wakamsweka ndani - habari zikamfikia mwalimu ikulu na mara moja akawaambia wamfungulie aende zake - hizo zilikuwa moja ya story zake tukiwa kwenye misiba pale kijijini kwetu.
Kuna siku nilikuwa nimepanga foleni kwa ajiri ya kupata vitu adimu (sukari, sabuni), kwa wale mnaokumbuka yale maduka ya RTC basi watoto tuliambiwa twende mapema ili wakati duka linafunguliwa saa 9 basi tupate vitu hivyo; mida ya saa kumi duka linafunguliwa foleni ikiwa ndefu sana, nikamwona Kasangatumbo anafika eneo la duka, akatuambia tumsikilze dk tano, pale nakumbuka alituambia tutapanga foleni hizo hadi tutakapoamua kuwa na demokrasia ya vyama vingi - pale sikuelewa kitu kwamba hiyo demokrasia ndiyo italeta maduka mengi? I was young by age anyway. (9)
Inaendelea post #2 chini...
cc Ngongo, JingalaFalsafa, Mzee Mwanakijiji, Ogah, Mohamed Said, Nguruvi3, Mchambuzi, WOWOWO, Mkandara, Jasusi, Gembe, Phillemon Mikael, Mwanagenzi, Rutashubanyuma, Augustine Moshi, Pasco,
nafikiri baadaye ikawa order arudi kwao kijijini, na ndiyo maana anakarudi ipole; ni kweli alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na hakuwa na marafiki pale kijijini, alikuwa mpweke sana na muda wa kuongea na wanakijiji ulikuwa ni wakati wa misiba tu. Na kila utakapomwona lazima awe na radio yake ndogo maskioni na mara nyingi tulikuwa tukisogelea tunasikia habari za kiingeleza, nafikiri alikuwa nasikiliza BBC
Mzee huyu alikuwa anachunga ngombe kutwa nzima juani, mavazi duni sana, kiujumla hali ya miasha yake ilikuwa vigumu kuielezea.
Je, wamfahamu mzee Obed Mgongo?
Nilibahatika kukutana na huyu Mzee na alikuwa anapenda sana kueleza historia yake.
Alikuwa mwakilishi wa kwanza wa serikali ya tanu nchini Uingereza kama balozi.
Lakini alirudi Tanganyika 1962 akaanza kudai vyama vingi na kuanzisha NDP ndipo akapelekwa detention gereza la Uyui tabora huyu mzee alikuwa ni mfungwa wa kwanza kuwekwa katika Gereza la Uyui wakati huo bado jipya kabisa. Ina maana ni mfungwa namba moja.
Kuanzia hapo akaitupa kadi yake ya TANU akawa mpinzani bila chama na hakuwahi kurudi tena TANU wala kuwa mwanachama wa CCM.
Alisema kuna siku alikuwa analima shambani kwake akawa anasikiliza taarifa ya habari saa 7 mchana kwenye redio yake akasikia Nyerere anatangaza kuwa Tanzania tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi.
Akarudi nyumbani kwake haraka sana akamwambia mke wake ampangie vitu viwili vitatu kwenye begi lake safari ikawa moja kwa moja Dar es salaam na akakutana na akina Chief Fundikira na kuanzisha UMD.
Alikuwa kiongozi mpinzani wa kweli na kwenye historia ya wakati ule ni kiongozi wa upinzani pekee ambaye hakuwahi kuwa mwanachama wa UMD.
Wengine wote walishawahi kuwa wanachama wa CCM kwa namna moja au nyingine. Sababu kubwa ilikuwa huwezi kupata kazi bila kuwa mwanachama wa CCM kwa maana nyingine uanachama ulikuwa lazima.
Nyerere alikuwa dikteta
Kwasababu aliaminisha watu vyama vingi ni vita. Dikteta sana yule dingiNi kweli alikuwa dikteta. Nakumbuka hata kura ya maoni iliyopigwa kuhusu kuruhusu mfumo wa vyama vingi ulikataliwa lkn yeye akalazimisha. Bila yy tungekuwa na chama kimoja.
Mnyonge mnyongeni.......
Hapo vipi? Umatuchanganya.
Kwasababu aliaminisha watu vyama vingi ni vita. Dikteta sana yule dingi[/QUO
Hahahaaa.....Mwacheni BABA WA TAIFA apumzike. Mwisho a sikumtaanza kusema yeye ndo amekuwa akisaini mikataba ya kinyonyaji. Kwamba fisadi wote ni matokeo yake sio ujinga wetu watz
Kafa maskini kazikwa kienyeji; kaburi la udongo; just thinking kama wanafamilia watanikubalia basi nitalijengea. Huyu ndie balozi wetu wa kwanza nchini ui geleza baada tu ya uhuru wa nchi yetu 1961.Sidhani kama watanzania wengi wanajua h5istiria hii.At least I have seen someone who is unveiling the truth, What happened to him?