Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

Da ila me simlaumu ticha wala katumbo. Ukichungulia upande wa mwalimu unaweza kuta alilinda maslahi yake na taifa letu changa la tanganyika!

Katumbo nae anaweza akawa alikua na maono yake ambayo nyerere aliona yatamuatarishia uongozi wa taifa na sifa zote alizo jikusanyia yeye kama kiongozi wa taifa.

Siwezi kumchukia Mwl. Katika maisha yangu kwani mwarimu alinikomboa na kuwa huru mungu amesha wapatanisha wazee wetu huko walipo.
Hakika
 
Ukweli ni kwamba histori ya Tanganyika imechakachuliwa sana na Baba CCM yaani Tanu, yapo mengi kama haya. Na miaka 20 ijayo yanaweza yasipatikane tena. Maana wale wazee waliokuwepo wakati huo wanaishia. Namkumbuka Zuberi Mtemvu, Michael Sanga, Patric Kunambi, Kasela bantu, Lifa Chipaka, Kassim Hanga, Oscar Kambona, Aboud Jumbe, Mwamwindi the Great, NK. Ni vizuri kujua upande wa pili wa historia.
Historia ya Tanganyika haijawahi kuchakachuliwa,na sio kweli kuwa kila kitu ni lazima kiandikwe.kwa mfano wewe umeandika nn juu ya historia ya tanganyika.unaposema imechakachuliwa,maana yake ipo iliyo sahihi unayoijua wewe,je umeiandika wapi?
 
Mmm, sasa huu uzi unakuja vizuri, kama kuna mwanahabari makini achukue mambo hapa, awatafute wazee waliobakia na kuoanisha hizi taarifa, ili tuboreshe historia yetu. Swali je kwa nini vyama vingi vilifutwa Tanganyika? Vilikuwa vingapi? Na viongozi wake walikuwa ni nani?

Nakumbuka siku ile tulipokua ikulu tukizungumzia mustakabali wa vyama vingi Tanganyika, mara Mtemvu na Julius walipokwidana. Mmoja akisema "By the way did you call me another Shombe in Afrika" Mkutano ukavunjika na vyama vingi vikalwakatariwa. Chipaka sijui bado anakumbuka? maana ndio alikuwa muamuzi wa mechi.
Sio kweli.vijana acheni kudandia hoja.kama hujui kaa kimya.
 
Nasiki walikuwepo wengi wa aina hii? Wakabaki wale wa Gerezani tu, katika historia. Na huyu si alikuwa mpambanaji mzuri wakati wa kutafuta uhuru? Mbona sijamwona katika kitabu chochote kile.
Unaweza kudhibitisha kuwa kasanga tumbo amewahi kushiriki kupigania uhuru?!!
 
Nilibahatika kukutana na huyu Mzee na alikuwa anapenda sana kueleza historia yake.

Alikuwa mwakilishi wa kwanza wa serikali ya tanu nchini Uingereza kama balozi.

Lakini alirudi Tanganyika 1962 akaanza kudai vyama vingi na kuanzisha NDP ndipo akapelekwa detention gereza la Uyui tabora huyu mzee alikuwa ni mfungwa wa kwanza kuwekwa katika Gereza la Uyui wakati huo bado jipya kabisa. Ina maana ni mfungwa namba moja.

Kuanzia hapo akaitupa kadi yake ya TANU akawa mpinzani bila chama na hakuwahi kurudi tena TANU wala kuwa mwanachama wa CCM.

Alisema kuna siku alikuwa analima shambani kwake akawa anasikiliza taarifa ya habari saa 7 mchana kwenye redio yake akasikia Nyerere anatangaza kuwa Tanzania tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

Akarudi nyumbani kwake haraka sana akamwambia mke wake ampangie vitu viwili vitatu kwenye begi lake safari ikawa moja kwa moja Dar es salaam na akakutana na akina Chief Fundikira na kuanzisha UMD.

Alikuwa kiongozi mpinzani wa kweli na kwenye historia ya wakati ule ni kiongozi wa upinzani pekee ambaye hakuwahi kuwa mwanachama wa CCM.

Wengine wote walishawahi kuwa wanachama wa CCM kwa namna moja au nyingine. Sababu kubwa ilikuwa huwezi kupata kazi bila kuwa mwanachama wa CCM kwa maana nyingine uanachama ulikuwa lazima
.
Maelezo yako Yana walakini aliporudi alianzisha chama, Nyerere akamweka ndani , akatupa Kadi ya Tanu. Aliwezaje kuanzisha chama cha siasa huku anamiliki Kadi ya Tanu?
 
Licha ya kusema alipewa fedha kupindua serikali, Kasanga Tumbo (ni mara chache tulikuwa tunasikia jina lake la kwanza, Christopher, ingawa nalo lilijulikana) alikuwa na uhusiano na viongozi wa maasi ya jeshi, Colito Barracks, 1964. Victor Mkello pia alikuwa na uhusiano huo. Kuna mengi bado yamefichwa lakini Kasanga Tumbo na Mkello walikuwa wanatafuta njia ya kutumia maasi hayo kumuondoa Nyerere madarakani na kuunda serikali yao. Kulikuwa na viongozi wengine katika shirika la wafanyakazi na nje ya shirika hilo waliotegemea kuwa viongozi katika serikali ya Kasanga Tumbo na Victor Mkello viongozi hao wawili wangefanikiwa kumuondoa Nyerere. Inasemekana hata Nyerere aliamini kulikuwa na uhusiano kati ya waasi na viongozi hao wa wafanyakazi. Walikuwa siyo viongozi wa kuaminika.


Kwahiyo tofauti kati ya Nyerere na Kasanga Tumbo haikuwa ni ya mfumo wa vyama tu: tuwe na chama kimoja au vyama vingi vya siasa.


Jaribuni kumshawishi Mzee Lusinde atuambie yaliyotokea wakati ule wa maasi. Anajua mengi. Wengine waliojua nini kilitokea - Kawawa, Kambona na Bomani - wameisha tuondoka. Lakini kuna wengine ambao bado ni hai. Kuna mambo mengi pia ambayo Sarakikya anayajua kwa undani. Mwingine ni Mzee Kahama.


Kuhusu Kasanga Tumbo na vitisho vyake kwamba alipewa fedha Uingereza kumpindua Nyerere, pamoja na uhusiano wake na waasi wa jeshi na kujaribu kutumia maasi hayo kuunda serikali yake pamoja na Victor Mkello na viongozi wengine, amshukuru Nyerere hakuwa kama viongozi wengine. Katika nchi zingine za Kiafrika na hata nje ya bara letu, ungekuwa ndiyo mwisho wake wakati ule. Hata kaburi lake msigejua liko wapi.


Ni muhimu tujue historia yetu. Lakini mara nyingi maswali ya aina hii yanapoulizwa, kuna wale ambao wanajaribu kupindua ukweli au kutumia historia hiyo kumshambulia na kumlaumu Nyerere bila kuangalia upande mwingine kwa nini aliamua alivyoamua kuhusu mambo mbali mbali pamoja na yale yanayohusu usalama na umoja wa taifa letu. Alikuwa na mapungufu yake. Alifanya makosa kama binadamu wengine. But he shouldn't be blamed for everything that has gone wrong in our country since independence. Apportion guilt accordingly.
Chukua maua yako.
 
Swali dogo tu, chama kilikuwa na uhai wa miaka 2, uliwezaje kukipima na kusema kilikuwa na nguvu saaana, wakati hata hakikushiriki kwenye uchaguzi? Hivi kipimo cha nguvu ni watu kufika mkutanoni? Kumbuka katika nchi zetu, ambazo watu kazi zao ni za msimu kama wakulima, mikutano, ni moja pa mahala kwenda kutoa stress, na kuona vimwana kama ngomani.

I really doubt your analysis
Kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 1960,katanga tumbo hakuwa sehemu ya upinzani.
 
Kafa maskini kazikwa kienyeji; kaburi la udongo; just thinking kama wanafamilia watanikubalia basi nitalijengea. Huyu ndie balozi wetu wa kwanza nchini ui geleza baada tu ya uhuru wa nchi yetu 1961.Sidhani kama watanzania wengi wanajua h5istiria hii.
Yeye mwenyewe anasema aliwahi kuitwa na Nyerere kuongoza shirika la reli lakini akakataa. So sahihi kuhusisha umasikini wake na mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom