Huyu ndiye bwana mdogo Kalulu aliyeasiliwa na Sir Henry Stanley na kuzunguka naye Afrika,Ulaya na Amerika

BoManganese

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
979
2,670
Kalulu.PNG

Kalulu alikuwa ni kijana wa miaka 12 ambaye alinunuliwa kama mtumwa kutoka kwa waarabu huko Zanzibar na mwingereza aitwae Sir Henry Morton Stanley. Mwingereza huyu alikuja kama mpelelezi kwa ajili ya kuipeleleza Afrika na kuiandaa kuja kutawaliwa na wakoloni.

Kijana huyu jina lake halisi alikuwa anaitwa Ndugu Mhali lakini Sir Henry Stanley hakulipenda jina hilo hivyo akambatiza kijana huyo jina akamwita Kalulu.

Hivyo Kalulu alikuwa ni mfanyakazi wa Sir Henry Stanley kati ya miaka ya 1872 mpaka 1873 Kalulu alifanikiwa kuwa mfanyakazi wa karibu wa Sir Henry Stanley walizunguka wote huko mabara ya Amerika na Ulaya.

Sir Henry Stanley alimpeleka shule Kalulu huko Wandsworth, South west London mwalimu wa Kalulu aligundua kuwa Kalulu ni mjanja sana na alikuwa anajifunza vyema lugha ya kiingereza.

Lakini Kalulu hakufanikiwa kusoma kwa muda mrefu shuleni hapo kwasababu ilipo fika mwaka 1874 Dr David Livingstone alifariki akiwa nchini Zambia hivyo Sir Henry Stanley alitakiwa kurudi Afrika kushika nafasi iliyoachwa na Dr Livingstone katika shughuli za upelelezi. Hivyo Sir Henry Stanley alimwachisha shule Kalulu huko london wakarudi Afrika.

Ilipofika mwaka 1877 Kalulu akiwa kama mfanyakazi wa Sir Henry Stanley walisafiri pamoja katika mto Congo kutafuta chanzo cha mto huo lakini kwa bahati mbaya sana mtumbwi aliokuwa amepanda Kalulu ulikumbwa na dhoruba na kupelekea Kalulu kudondoka katika maporomoko ya maji na kufariki dunia na huo ndio ulikuwa mwisho wa kijana Kalulu.
Hivyo maporomoko hayo yalipewa jina la kalulu ili kumuenzi kijana huyu

Nawasilisha
_IMG_15738228514694033.jpeg
_IMG_15738228423208789.jpeg
_IMG_15738228469179089.jpeg
 
Back
Top Bottom