Huyu ndiye atakayemuondoa bungeni Nimrod Mkono2015...

Hongera sana kwa kutangaza nia kwa style ya uwoga hivi. Ila kabla ya kumtoa Mkono utatakiwa kufanya kazi ya kunitoa mimi kwanza katika ngazi ya chama (CHADEMA) kama utataka kugombea kwa chama chetu makini. Ni mimi kijana wa Mmazami Makutano ya juu. Fisadi Mkono lazima aondoke 2015.

Nimeipenda hii, uzuri wa mchezo ni lazima kukabana na mwisho wa siku CDM ichukue Jimbo. Kongi, hebu na wewe weka wasifu wako tuone.
 
Kumtoa Mhe Mkono hizo ni ndoto labda huyu anataka kukatiwa pesa. Mhe. Mkono amefanya maendeleo mengi sana kwenye Jimbo lake njoo muone sio siri. Namtakia Maisha mema adumu kwenye Ubunge mpaka achoke mwenyewe.
 
Magesaaaaaaaa! kweli umemua bro.komaaa kaka,mwanzo mzuri ila jiandae kwa vita kali kwani sidhani kama atauachia kirahisi rahisi.
Ushauri: weka mikakati rahisi na sahihi....!
 
Nani anaota mimi au wewe??

Mimi niko Musoma, nafahamu nini kinaendelea!

Maeneo ya Majita, Mugango na kwingineko kuna madiwani hadi wa CHAUSTA, UPDP, CUF n. k

Maeneo ya kwao ndio hakubaliki kama unadhani nakudanganya uliza. Watu mko blinded na Shule alizojenga ambazo asilimia kubwa ya watoto wanaosoma hapo si kutoka jamii zinazozunguka hapo.

BTW, Mkono si mwanasiasa kabisa, na hata Familia ya Mwalimu hawamkubali kiivyo akiwemo pia Chief Japhet Wanzagi...

Wanasiasa wote unaosikia wanapita bila kupingwa si wanasiasa wanaoweza himili mikiki mikiki ya majukwaani ndio maana wanategemea rushwa ili kufanikisha malengo yao wakiwemo Anna Makinda, J. Makamba, Mkono & Co.
Hayo mengine sijui, lakini ninajua kuwa kampuni ya Mkono ndio walikuwa wanasheria wa Mwl Nyerere Foundation mwalimu mwenyewe akiwa hai. Ni familia gani hiyo isiyomkubali? Kwa taarifa yako, huyu ni mmoja wa watu walio karibu sana na hiyo familia, na ameisaidia sana.
 
Magesaaaaaaaa! kweli umemua bro.komaaa kaka,mwanzo mzuri ila jiandae kwa vita kali kwani sidhani kama atauachia kirahisi rahisi.
Ushauri: weka mikakati rahisi na sahihi....!
Wewe ndugu sema unataka jimbo gani cose MKONO ataenda kugombea wilaya mpya BUTIAMA kama jimbo jipya 2015. Au hujajua musoma vj itakuwa na majimbo mawili. Kama unabaki na w....a wenzanko ili upambane nao huko. huyu mzee hamtamweza muacheni aendelee mpaka atakapo sema anapumzika. Huna jipya sana kajikite kwa wasira.
 
Basi kwa hali hii uchachuzi wa kura za maoni 2015 ndani ya CDM patachimbika so inabidi chama kije kiruhusu demokrasia iliyo wazi na pana kwani kwa utafiti wangu mdogo niliofanya na wanafunzi wenzangu wa hapa UDOM wasiopungua 56 wamesema wote 2015 lazima watagombea kupitia CDM. Sasa kwa hali hii nina imani bado tu watu wapo wengi vyuo vingine na wengine makizini ambao watataka wagombe. Alafu kikubwa kuna watu 5 wanampango wa kwenda kugombea kupitia jimbo la Mbowe (hai)
2015 ITAKUWA NI KAZI KWELI KWELI .
 
Mie pia ni mdau wa Musoma ,Mkono ni fisadi wa maendeleo ya wananchi na amekuwa akitumia fedha kama fimbo kupigia maskini kwa ajili ya kuua demokrasia.Naamin katika uchaguzi wa 2015 Mkono hatoki amekuwa msumbufu kupita kiasi mfano ujenzi wa makao makuu pale Kiabakari ame lobby viongozi wa kitaifa amepeleka makao makuu karibu na kwao ili aweze kupangisha nyumba zake na ndugu zake kwa watumishi wapya wa Halmashauri na serikali kuu ,huu ni uhuni.Jambo zuri tumekwisha juu mbinu zake za porini na sisi lazima tumuondoe.David mie kwetu Musoma pia naona tumemaliza mwaka mmoja UDSM ingawa tulikuwa wengi sijakupata vizuri mie nilikuwa B.COM ,CPA and Msc.Economics & Fin.Weka mipango vizuri na baadaye hadharini nitakusupport na bahati nzuri watumishi wengi rika letu wamepanga kutoa ushirikiano wa nguvu kuhakikisha jimbo lina tua kwa mtu mwenye vision kuliko hivi sasa Mkono anafanya kama NGO.
 
David anatambua kuwa hadi sasa kuna wagombea zaidi ya 30 waliojitokeza kugombea Musoma vijijini 2015 kupitia chadema (aliambiwa na vincent nyerere wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo arumeru mashariki pale ngomeni)..David sio muoga ndio maana alipambana na goliath na kumshinda..anawasubiri uwanjani kwenye kura za maoni..yuko tayari kwa kila idara..tayari ameshaanza survey musoma vijijini kutambua mti wa matatizo (problem tree) then atafute mti wa kuondoa matatizo (solution tree),aje na objective, output na finally activities..hivi vyote vitaongozwa na strategies.David anasema bado ndo kwanza yuko kwenye preliminary stage.kabla ya survey kuanza,alianza na jografia ya musoma vijijini,distances from one kijiji to another,idadi ya watu,wanafanya nini,akina mama ni wangapi,akina baba..vijana watakaopiga kura 2015 ni wangapi na pia kufahamiana na uongozi wa chadema wilayani,wajumbe wa kamati tendaji ya wilaya na mkoa n.k...DAVID AMEJIANDAA..KAJIANDAA HASA SIO KIDOGO..

Hongera kaka...i know you can talk the talk and definetly walk the talk....tupo pamoja
 
naifaha musoma vijini vyema kuanzia bwasi bwai kiabakari hadi kiagata. kwanza aliyegombea CHADEMA 2010 Yuko Udom mwaka 3. na ndani ya chama kunamgogoro na hata mjumbe wa baraza kuu kutoka musoma vijini hakuhudulia mkutano wa tarehe 29/4 kwa hiyo uyo david kama anawapenda watu wa msoma aende kujenga chama kwanza.
 
David anatambua kuwa hadi sasa kuna wagombea zaidi ya 30 waliojitokeza kugombea Musoma vijijini 2015 kupitia chadema (aliambiwa na vincent nyerere wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo arumeru mashariki pale ngomeni)..David sio muoga ndio maana alipambana na goliath na kumshinda..anawasubiri uwanjani kwenye kura za maoni..yuko tayari kwa kila idara..tayari ameshaanza survey musoma vijijini kutambua mti wa matatizo (problem tree) then atafute mti wa kuondoa matatizo (solution tree),aje na objective, output na finally activities..hivi vyote vitaongozwa na strategies.David anasema bado ndo kwanza yuko kwenye preliminary stage.kabla ya survey kuanza,alianza na jografia ya musoma vijijini,distances from one kijiji to another,idadi ya watu,wanafanya nini,akina mama ni wangapi,akina baba..vijana watakaopiga kura 2015 ni wangapi na pia kufahamiana na uongozi wa chadema wilayani,wajumbe wa kamati tendaji ya wilaya na mkoa n.k...DAVID AMEJIANDAA..KAJIANDAA HASA SIO KIDOGO..

Hapa nina wasiwasi anieleze umbali uliopo toka Bugoji hadi Suguti na aseme idadi ya wakazi walioko katika kijiji cha Saragana.
 
Nani anaota mimi au wewe??

Mimi niko Musoma, nafahamu nini kinaendelea!

Maeneo ya Majita, Mugango na kwingineko kuna madiwani hadi wa CHAUSTA, UPDP, CUF n. k

Maeneo ya kwao ndio hakubaliki kama unadhani nakudanganya uliza. Watu mko blinded na Shule alizojenga ambazo asilimia kubwa ya watoto wanaosoma hapo si kutoka jamii zinazozunguka hapo.

BTW, Mkono si mwanasiasa kabisa, na hata Familia ya Mwalimu hawamkubali kiivyo akiwemo pia Chief Japhet Wanzagi...

Wanasiasa wote unaosikia wanapita bila kupingwa si wanasiasa wanaoweza himili mikiki mikiki ya majukwaani ndio maana wanategemea rushwa ili kufanikisha malengo yao wakiwemo Anna Makinda, J. Makamba, Mkono & Co.

uko sawa. naongezea tu katika uchaguzi wa 2010 hakukua na mawakala wa CHADEMA katika vituo karibia vyote na ni kutokana na kutokuwepo na wagombea wa udiwani ktk kata nnyingi na ubunge. sambamba na uongozi dhaifu pia dk slaa hakutua jimboni kwa campein wala kiongozi yoyote zaidi ya CCM lakini matokeo ya urais dk aliongoza.
 
Hongera sana kwa kutangaza nia kwa style ya uwoga hivi. Ila kabla ya kumtoa Mkono utatakiwa kufanya kazi ya kunitoa mimi kwanza katika ngazi ya chama (CHADEMA) kama utataka kugombea kwa chama chetu makini. Ni mimi kijana wa Mmazami Makutano ya juu. Fisadi Mkono lazima aondoke 2015.

wa mazami juu. msalimie choge katbu wa wilaya CHADEMA. PIA Kwa jicho la kidemokrasia kila mtu anahaki hiyo iwe akutoe au ubaki usishangae wewe mwenyewe ukamkubali af ukampigia kura.
 
Nyie Muraa mna bahati sana ya kupendwa na upinzani tofauti na hapa Tanga.tatizo huyo mzee ananunuaga wagombea anapita b ila kupingwa
wa mazami juu. msalimie choge katbu wa wilaya CHADEMA. PIA Kwa jicho la kidemokrasia kila mtu anahaki hiyo iwe akutoe au ubaki usishangae wewe mwenyewe ukamkubali af ukampigia kura.
 
bandugu,david haongeki.pesa za mkono zinanuka.hamjawahi kusoma riwaya ya 'pesa zako zinanuka' ya elvis musiba?!,david haongeki.ni mtumishi wa Mungu wa kweli

Mkuu Magessa78,
Sahihisho; ni Pesa Zako Zinanuka (Give Me Money, kilivyotafsiriwa kwa kiingereza) cha ambacho kilitungwa na Benedict Rashid Mtobwa (RIP) na kuchapwa na Heko Publishers Limited.Maudhui yake yalikuwa juu Magendo, Uhujumu uchumi na Azimio la Arusha(UJENZI WA JAMII MPYA).
Setting yake ni Arusha mjini na wahusika wake ni Kandili Maulana, Ben Kolo, Dora na Idrisa Kalulu! Njoo PM tutete na kujadili riwaya zote za zamani!
 
Dah! kazi mnayo Magwanda maana huyo mzee hasubiri bajeti za serikali yeye shule, zahanati anajenga mwenyewe!

Huyu mkono ndo yule alieshirikiana na wenzake kuiba fedha pale BOT na badae wakaichoma moto na wenzake. Akakimbia nchini, Nyerere alimpiga marufuku kurudi Tanzanian na wale wanaofatiliaMkono alirudi Tanzania baad ya Nyerere kufa.
Hata hizo shule anazojenga anapiga picha mazingira halafu anapelekea wafadhiri wanampa hela, ila anapokuja huku anajidai kama anatoa pesa zake mfukoni.
Kiukweli huyu hata kama angetoa misaad bado inatakiwa tu ihesabike kama sehemu ya hela yetu aliokwapua Bot.

Hana lolote.
 
david karibu ulingoni.nikikushinda usihame chama ukaenda ccm.ukinishinda nitakuunga mkono
 
Kweli kabisa. Huyu kijana namfahamu, machachari sana. Anaitwa magessa, atamuondoa mkono kama jimbo halitagawika maana nasiki kutakuwa na majimbo mawili, jimbo la butima na jimbo la nyanja..
Hata hivyo tuko vizuri...
Asihongwe tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom