Huyu ndiye atakayeivusha Tanzania kwa Kasi zaidi

phillipinne

New Member
Jun 27, 2016
4
7
Tanzania ni kati ya nchi zilizojipatia uhuru wake mnamo miaka ya 1960's kutoka kwa mwingereza, hata hivyo Tanzania ilipata uhuru huo kwa njia ya amani pasipo umwagaji damu.
Nchi hii ilikwepa athari ambazo nchi zingine hupata kutokana na njia za vita katika kupata uhuru.
Pia Tanzania inaminika kuwa na raslimali nyingi za asili kama madini,misitu,Molina,mbuga za wanyama,mito,maziwa,bahari na aridhi yenye rutuba.
Hata hivyo baada ya uhuru Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani pasipo kuwepo vita wala ghasia za kutisha.
Vitu vyote hivi nilivyo vitaja ni mhimu sana kwa nchi kupiga hatua kwa Kasi katika maendeleo katika nyaja zote za maisha kiuchumi,kijamii na hata kisiasa.

Swali la kujiuliza je kuna wiano wa mda,kiasi cha maendeleo kilichofikiwa na raslimali zilizokwishatumika Tanzania mpaka sasa?

Jibu ni hapana.
Vitu hivi havina wiano kwa kuzingatia kiwango cha maendeleo na Kasi mpaka sasa hivilizishi huku kukiwa tayari raslimali nyingi zimekwisha tumika. Mfano elimu bado ni duni, huduma za afya ni duni, huduma za maji na umeme ni duni, barabara na reli ni duni.
Kwa hiyo unaweza kusema kila sehemu ni kama tumejalibu tu ila kuna kiasi kikubwa cha uduni pia umaskini bado upo kwa kiasi kikubwa sana.

Atakayeivusha Tanzania anapaswa kufanya yafatayo;
1. Tanzania itumie raslimali zake kwa maslahi ya watanzania wote.
2. Asimamie nchi pasipo kujali vyama au chama atokacho mtu katika kushughulikiwa na sheria
3. Aimalishe tasisi na sheria
4. Akubali mjadala huru wa kimaendeleo juu ya nchi
5. Siasa safi na utawala bora
6. Maadili kwa viongozi wa umma
 
Tatizo wanasiasa wengi huongea kwa midomo na matumbo yao badala ya midomo na mioyo yao!.Akili zao hufuata amri za tumbo kuliko za mioyo yao.
Naamini kuna siku huyo mtu atazaliwa!
 
Unakaanga mbuyu halafu unawaacha wenye meno wautafune. Kwani wewe ni kibogoyo? Anza wewe kumtaja mtu anayefaa kutokana na sifa ulizotaja. La sivyo huu ni uzushi wenye malengo machafu.
 
Serikali ambayo inakimbia jukumu la kuwa mdau nambari moja katika viwanda na kuweka sera mbadala itakayo mfanya mtanzania awajibike katika kuendesha viwanda.

Huku ikiachia wawekezaji kutoka nje ni njia moja wapo ya watanzania kuto faidi matunda ya nchi yao .
Lengo lao likiwa ni kutaka kuwa ridhisha wananchi wawapigie kura bila kuangalia madhara ya muda mrefu hii ni hatari sana
 
...tulienae ikulu sasa hivi ni 'mungu mtu' kazi yake kubwa ni kulazimisha watu wamwabudu...
"Sabung'ori" naamini wewe ni mtu mzima unajitegemea kimawazo pia, ndiyo maana umeweza kubandika hayo maneno humu JF. Vipi udhani kwamba tunalazimishwa na mtu! Labda kama umelazimishwa wewe kuandika hayo!!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Masahihisho

Tanzania haikupata Uhuru 1961
Tanganyika ndio ilipata Uhuru mwaka huo toka kwa mwingereza
 
...tulienae ikulu sasa hivi ni 'mungu mtu' kazi yake kubwa ni kulazimisha watu wamwabudu...

Hali hii imesababishwa na mfumo wa chama chao na kufanya watanzania wasio na dira. Watanzania wasio aminiana,watanzania wenyewe mawazo ya kuharibu pale wanapo kabidhiwa majukumu ya umma Huku roho ya ubinafsi ikishamiri.

Leo hii wao wenyewe wanashangaa kwanini watanzania wamekuwa hivyo.
Sasa wanachofanya nikutumia nguvu nyingi kutaka kuwarudisha kwenye mstari ndani ya muda mfupi wakati hizi tabia zilijijenga si chini ya miaka 40 iliyopita ni kitu ambacho hakiwezekani.
Lazima watachemka tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Aliyopo hana sifa hata moja.[/QUOTE

Hata kama raisi aliyepo ni mzuri Lakini kama hajapatikana kwa njia halali.
Hili ndio chimbuko la kukosekana kwa uzalendo hivyo kuwafanya watanzania kuwa na roho za chuki na kutoaminiana.

Huu ni ukweli kwani ukiaharibu mwanzo wa jambo lolote matokeo yake ni kutofanikiwa au kufanikiwa kidogo sana .
 
Tanzania ni kati ya nchi zilizojipatia uhuru wake mnamo miaka ya 1960's kutoka kwa mwingereza, hata hivyo Tanzania ilipata uhuru huo kwa njia ya amani pasipo umwagaji damu.
Nchi hii ilikwepa athari ambazo nchi zingine hupata kutokana na njia za vita katika kupata uhuru.
Pia Tanzania inaminika kuwa na raslimali nyingi za asili kama madini,misitu,Molina,mbuga za wanyama,mito,maziwa,bahari na aridhi yenye rutuba.
Hata hivyo baada ya uhuru Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani pasipo kuwepo vita wala ghasia za kutisha.
Vitu vyote hivi nilivyo vitaja ni mhimu sana kwa nchi kupiga hatua kwa Kasi katika maendeleo katika nyaja zote za maisha kiuchumi,kijamii na hata kisiasa.

Swali la kujiuliza je kuna wiano wa mda,kiasi cha maendeleo kilichofikiwa na raslimali zilizokwishatumika Tanzania mpaka sasa?

Jibu ni hapana.
Vitu hivi havina wiano kwa kuzingatia kiwango cha maendeleo na Kasi mpaka sasa hivilizishi huku kukiwa tayari raslimali nyingi zimekwisha tumika. Mfano elimu bado ni duni, huduma za afya ni duni, huduma za maji na umeme ni duni, barabara na reli ni duni.
Kwa hiyo unaweza kusema kila sehemu ni kama tumejalibu tu ila kuna kiasi kikubwa cha uduni pia umaskini bado upo kwa kiasi kikubwa sana.

Atakayeivusha Tanzania anapaswa kufanya yafatayo;
1. Tanzania itumie raslimali zake kwa maslahi ya watanzania wote.
2. Asimamie nchi pasipo kujali vyama au chama atokacho mtu katika kushughulikiwa na sheria
3. Aimalishe tasisi na sheria
4. Akubali mjadala huru wa kimaendeleo juu ya nchi
5. Siasa safi na utawala bora
6. Maadili kwa viongozi wa umma

Sidhani kama kuna usahihi katika para yako ya kwanza.

Nijuavyo Tanganyika haijapewa uhuru wake na Muingereza wala sidhani kama kulikuwa na sababu yoyote ya umwagaji damu katika kudai kwake kujitawala kwani Tanganyika ilidai uhuru wake wa kujitawala kutoka Umoja wa Mataifa na si Uingereza.

Tanganyika ilikuwa ni protectorate tu ya Uingereza na si koloni la Uingereza.

Huwa nnashangaa sana historia inapopotoshwa amma kwa makusudi amma kwa kutokuelewa amma kwa kusomea ujinga.
 
Kwa jinsi nionavyo mimi mtu wa kutuvusha na kutupeleka kwenye maendeleo labda atapatikana 2020, Kwa sasa acha tuendelee kuisoma namba tu Kwa sababu ndivyo walivyochagua ndugu zetu
 
Back
Top Bottom