Huyu Ndiye Anayetakiwa Kumlipa Dalali Kwenye Uwekezaji Wa Ardhi Na Majengo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Dalali anatoa huduma ya kuunganisha huduma zinazohusiana na ardhi na majengo kati ya makundi yafuatayo;-

✓ Wapangaji na wenye nyumba.

✓ Wauzaji na wanunuzi.

✓ Watoa mikopo na wapokeaji mikopo ya majengo.

Haya ndiyo makundi makuu (3) ambayo huhusika na gharama za kumlipa dalali kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo.

Somo hili limelenga kwa ajili ya huduma za udalali wa ardhi na majengo. Maarifa sahihi na uzoefu kuhusu udalali wa vitu au mali za aina nyingine unaweza usiipate kwenye makala hii.

Sababu Kuu Ya Uwepo Wa Udalali.

Huduma ya dalali ipo kwa sababu kuu ya kutoa taarifa kwenye upande ambao una uhitaji mkubwa wa huduma husika. Dalali anaweza kuhusika kutoa taarifa za huduma zifuatazo;-

✓ Huduma ya upatikanaji wa vyumba au nyumba za kupangishwa.

✓ Huduma ya upatikanaji mikopo ya ardhi na majengo.

✓ Huduma ya upatikanaji wa ardhi au nyumba zinazouzwa.

Kwa sababu hii ya uwepo wa dalali ni vigumu sana kufanikisha kulamisha upande mmoja uhusike kumlipa dalali wa ardhi na majengo.

Uhitaji Wa Chumba Kwa Mpangaji.

Kwenye eneo ambapo kuna hali nzuri ya soko mahalia la nyumba za kupangisha, wenye nyumba hata asipomtafuta dalali ataendelea kuwa na wapangaji kwenye nyumba yake miezi yote 12 ya mwaka.

Wakati huohuo wapangaji watakuwa na ugumu wa kupata taarifa sehemu ambapo vyumba vinapatikana.

Kwenye mazingira haya, mpangaji atamlipa dalali ili aweze kumjulisha sehemu ambapo nyumba hupatikana.

Mpangaji asipokuwa tayari ataendelea kukosa chumba au nyumba kwa ajili ya biashara au kuishi.

Uhitaji Wa Mkopo Kwa Mwekezaji.

Mwekezaji anapohitaji mkopo na taarifa sahihi kuhusu mikopo unaomfaa atatakiwa kufahamu vyanzo vingi vya watoaji wa mikopo ya ardhi na majengo.

Kwenye mazingira ambayo upatikanaji wa mikopo ya majengo ni shida, mwekezaji analazimika kumtafuta dalali wa mikopo.

Dalali huyu atahusika kutafuta vyanzo vingi vya aina ya mkopo unaohitajika na mteja wake.

Dalali atawasilisha taarifa sahihi za vyanzo ambavyo anaona vinaweza kumfaa mteja wake.

Kisha, mwekezaji na dalali wake wa mikopo watachagua chanzo ambacho kinawafaa wao.

Kwa mazingira haya, hata iweje benki au chanzo cha mikopo ya majengo hakiwezi kumlipa dalali wa mikopo ya majengo.

Kwenye mazingira ambayo chanzo cha mikopo kimekosa wawekezaji wa kuomba mikopo ya ardhi na majengo, watoaji wa mikopo watalazimika kumtafuta dalali wa ardhi na majengo.

Kwa mazingira haya, dalali atalipwa na chanzo husika cha mikopo ya ardhi na majengo.

Uhitaji Wa Wapangaji Kwa Mwenye Nyumba.

Kwenye hali baya ya soko mahalia na uchumi mahalia wa eneo husika, mwenye nyumba ni lazima atangaze kuwa anahitaji wapangaji wa nyumba yake.

Kwa mazingira haya, njia mojawapo anayoweza kuitumia kuwafikia wapangaji watarajiwa ni kumtafuta dalali wa nyumba za kupangisha.

Mwenye nyumba atalazimika kumlipa dalali wake kwa sababu anamuondolea chanagamoto ya kukosa kipato endelevu kutoka kwenye nyumba zake za kupangisha.

Uhitaji Wa Kununua Ardhi Au Nyumba Kwa Mwekezaji.

Kuna mbinu nyingi ambazo dalali wa ardhi na majengo ni muhimu sana kuwa naye kwa mnunuzi wa nyumba kuliko hata muuzaji wa nyumba.

Mbinu zinazohitaji uwe na dalali wa ardhi au nyumba zinazouzwa ni kama ifuatavyo;-

✓ Kununua na kuuza nyumba ndani ya miaka miwili (2).

✓ Kununua na kuuza viwanja na mashamba ndani ya miaka miwili (2).

✓ Kuwekeza kwenye ardhi na majengo ukiwa mbali na mji unapoishi (long-distance real estate investing).

✓ Kununua na kuuza mikataba ya ardhi na nyumba.

✓ Kununua na kuuza mikopo inayofanya kazi na mikopo isiyofanya kazi (performing and non-performing notes).

Je mwenye nyumba atakuwa tayari kumlipa dalali wa nyumba za kupangisha bila ya yeye kuwa na uhitaji wa wapangaji?.

Makundi Sita (6) Ya Watu Wanaotakiwa Kumlipa Dalali.

Moja.

Wapangaji wa nyumba, viwanja au mashamba (tenant's agent).

Hawa watatakiwa kumlipa dalali wa kiwanja au shamba au nyumba ikiwa kwao ilikuwa chanagamoto na wanahitaji utatuzi wa chanagamoto yao.

Mbili.

Mwenye nyumba (Landlord's agent).

Wenye nyumba za kupangisha (nyumba za kuishi, fremu za biashara, hoteli, apatimenti kubwa na kadhalika).

Hawa watatakiwa kumlipa dalali ikiwa wamekuwa na changamoto ya kupata wapangaji na wana uhitaji wa kumtumia dalali kama njia yao ya kujitangaza.

Mwenye nyumba ambaye hana chanagamoto na ashikiwe kisu kuwa anatakiwa kumlipa dalali itakuwa sio biashara tena.

Tatu.

Mnunuzi wa ardhi na majengo (buyer's agent).

Huyu anatakiwa kumlipa dalali ikiwa ana chanagamoto ya kuhitaji ardhi au nyumba inayouzwa ndani ya siku za mategemeo yake.

Hapa sina maana gharama za kutembelea eneo au nyumba. Gharama za kutembelea eneo linalouzwa au nyumba inayouzwa zinaweza kupangwa na dalali kwa sababu ya kupunguza idadi wanunuzi wababaishaji.

Nne.

Muuzaji wa ardhi au nyumba (Seller's agent).

Muuzaji huyu anaweza kutumia dalali kuwafikia aina ya wanunuzi anaowahitaji kwa muda husika.

Kwa mazingira haya, tunategemea kabisa kuwa muuzaji wa ardhi au nyumba anatakiwa kumlipa dalali wake.

Tano.

Mkopeshwaji.

Huyu ni mwekezaji kwenye ardhi na majengo ambaye ana uhitaji wa huduma za udalali ili aweze kupata aina ya mikopo ya majengo ambayo inamfaa yeye na mbinu anayotumia kuwekeza.

Mkopeshwaji atatakiwa kumlipa dalali wa mikopo ya majengo kwa sababu yeye ndiye ana chanagamoto na dalali ametatua chanagamoto.

Kwenye mazingira haya, mkopeshaji kumlipa dalali wa mikopo itakuwa ni kujipendekeza na upotevu wa fedha za masoko ya huduma zake za mikopo.

Sita.

Mkopeshaji.

Huyu ni chanzo cha mikopo ya majengo ambayo hutolewa kwa wawekezaji kwenye ardhi na majengo.

Wakopeshaji ambayo wana chanagamoto ya kupata wakopaji kwa muda wanaotegemea wanaweza kuwatumia madalali wa mikopo ya majengo kuwafikia waombaji wa mikopo.

Kwa mazingira haya, wakopeshaji wa mikopo ya majengo watatakiwa kuwalipa madalali wao kwa sababu chanagamoto yao imetatuliwa.

Sababu Kuu Mbili (2) Za Uwepo Wa Utofauti Wa Uhitaji.

Moja.

Hali ya uchumi mahalia wa ardhi na majengo.

Kuna maeneo ambayo huwapendelea wapangaji kuliko wenye nyumba kama nilivyo eleza hapo juu.

Kuna maeneo ambayo wenye nyumba hupendelea na hawalazumiki kujitangaza kwa kutumia madalali ili kupata wapangaji bora kwenye nyumba zao.

Hali ya uchumi mahalia ndiyo huathiri upatikanaji wa mikopo ya majengo na upatikanaji wa viwanja vinavyo ongezeka thamani kwa haraka zaidi.

Mbili.

Hali ya soko mahalia la ardhi na majengo.

Vipindi vya anguko la soko la ardhi na majengo linakuwa na uhitaji mdogo sana wa nyumba na viwanja kiasi kwamba matumizi ya madalali yanakuwa makubwa sana.

Kwa mazingira haya, wamiliki wa ardhi na nyumba huhitajika kuwalipa madalali ili kuwafikia wapangaji au wanunuzi wa nyumba.

Makundi Mkuu Mawili (2) Ya Madalali.

MOJA.

Dalali wa upande mmoja (seller's agent, buyer's agent, tenant's agent, landlord's agent).

Hawa ni madalali ambao hutoa huduma za udalali kwa upande mmoja tu. Na kwa kawaida hulipwa na upande unaohudumia.

MBILI.

Dalali wa pande zote mbili (Dual real estate agent).

Hawa ni madalali wa pande zote mbili. Hawa hutoa huduma za udalali wa ardhi na majengo kwa pande zote mbili. Kwa lugha nyingine, dalali hawa hutatua chanagamoto za pande zote mbili kwa wakati mmoja.

Kwa kawaida, mdalali hawa hulipwa na pande zote mbili. Muuzaji na mnunuzi wa ardhi au nyumba humlipa dalali kwa wakati mmoja.

Mkopaji na mkopeshwaji humlipa dalali kwa wakati mmoja. Mpangaji na mwenye nyumba humlipa dalali kwa wakati mmoja.

Kuwekeza Kwenye Ardhi Na Majengo Bila Dalali (For Sale By Owner, FSBO).

Hii ni mbinu inayotumiwa na wawekezaji ambapo huweza kuuza nyumba au kiwanja bila kumtumia dalali.

Haijalishi mnunuzi amemtumia dalali au hajamtumia dalali. Haiwezekani kumlazimisha muuzaji wa nyumba kumlipa dalali ambaye hana mpango wa kumtumia.

Mbinu hii hutumiwa na wawekezaji kwenye ardhi na majengo ikiwa ni njia ya kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo.

Mbinu hii pia nimeileza kwenye kitabu changu kiitwacho NJIA 120 ZA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE ARDHI NA MAJENGO.

Kiasi Cha Gharama Za Udalali.

Udalali ni huduma kama zilivyo huduma nyingine. Haiwezekani na haitawezekana kumpangia mtu kiasi cha huduma zake.

Kama ilivyo kwenye huduma nyingine. Leo ninaweza kuandika kitabu na kukiuza laki moja na asiwepo wa kunipangia bei ya kuuzia.

Leo ninaweza kujenga hoteli na nikapanga kiasi cha kodi ya siku kulingana na ubora huduma zangu.

Kwenye huduma za udalali pia, vifuatavyo vinaweza kuamua kiasi sahihi cha gharama za kumlipa dalali;-

✓ Makubaliano ya pande zote mbili.

✓ Uhitaji wa huduma yenyewe.

✓ Ubora wa huduma ya dalali mwenyewe.

Ushauri Kutoka Kwangu.

Kwakuwa nimekushirikisha makundi makuu mawili ya madalali; dalali wa upande mmoja na dalali wa pande mbili.

Ili kuondoa sintofahamu, inatakiwa kuwe na uwazi kati ya pande tatu ili kuonyesha wazi nani anatakiwa kumlipa dalali anayehusika kwenye dili husika.

Pande tatu zinaweza kuwa ni kama ifuatavyo;-

✓ Dalali wa mikopo, mkopeshaji na mkopaji. Hawa wanatakiwa kuwekana wazi nani anatakiwa kumlipa dalali bila kuficha.

✓ Dalali wa ardhi na majengo, mwenye nyumba na mpangaji. Hawa wanatakiwa kuweka wazi wakati wa mazungumzo kuwa nani anatakiwa kumlipa dalali anayehusika kwenye dili hiyo.

✓ Dalali wa majengo, muuzaji wa ardhi au nyumba na mnunuzi wa ardhi/nyumba. Hawa nao wanatakiwa kuweka wazi bila kificho kuwa gharama za udalali zipo muuzaji au mnunuzi au wote wawili.

Je ni nani hasa anatakiwa kumlipa dalali kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo?. Tafadhali nishirikishe jibu lako kwenye kisanduku cha maoni cha hapo chini.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi Wa Ardhi Na Majengo.

WhatsApp/calls; +255 752 413 711
 
*Fursa ya biashara kwa ubia (joint venture)
*
Abraar Bricks Nyumba kwa wote,

Kumejitojeza fursa ya kibiashara ambayo inahitaji active partners wa kuingia nao makubaliano ya kibiashara (joint ventures).

Yeyote kati ya hawa hapa chini wanaokidhi vigezo tuwasiliane;

1) Upo kwenye fani ya ujenzi kwa zaidi ya miaka 5.

2) Civil Engineers or Architects.

3) Mwekezaji kibiashara mwenye mtaji wa kutosha.

Tutaingia ubia na wewe kwa mtaji wako kikazi au mtaji wako kifedha, muhimu uwepo karibu. Hii project ni ya muda mrefu.

Kwa maelezo zaidi pitia uzi huu: Fursa ya Ubia kwenye Real Estate Development na Construction. au wasiliana na Abdul Ghafur +255625249605

Sambazia na wengine.
 
Back
Top Bottom