Huyu ndiye anafaa kuvaa kiatu cha Mwl Nyerere

Mimi naona askofu yupo vizuri zaidi kuliko padre (slaa)! Au nyie mnaonaje wadau?
 
Hicho kiatu kipo wapi, ni namba ngapi? na ni cha ngozi au Sandals maana Mwalimu mara nyingi nilimuona na Sandals!

Je tunaruhusiwa kukipima na sisi? kama kitatu-fit! na kwanini kiatu cha Mwl. mnakinadi kwani wanafamilia hawakitaki?

Anyway kwanini mnajadili kuwapa wanasiasa hicho kiatu cha Mzee wetu? na nadhani kitunzwe kiwe kumbukumbu hasa pale kwenye makumbusho ya Butihama mwaka juzi nilipatembelea pana faa kutunza hicho kiatu.
 
Nyerere alifanya a few good things, kama kuleta umoja wa kitaifa.Ila kwa wale wanao ona mbali hii nayo ilikuwa na a wider agenda .Mwalimu ali-mismanage sana uchumi wa taifa letu.No, his ideas were too utopian and idealistic, hasa ukizingatia the nature of the human being.Sasa ametulea vipi kiroho na kimwili bwana?No, I simply don't agree with you. Obviously kiroho hapana, because he wasn't a pastor,sheikh or even farther.Kimwili pia no, kwasababu alituingiza kwenye mparaganyiko mkubwa sana wa kiuchumi na kuleta matatizo makubwa katika jamii yetu.Sina haja ya kuyataja matatizo hayo, tuliokuwepo tunayajua. Kumbuka uchumi ndio mhimili mkuu wa taifa,uchumi ukiharibika everything else ceases to exist.Sitasahau,nilifulia majani ya mpapai,nilipiga foleni siku nzima bila kuambulia hata robo kilo ya sukari,wewe leo utaniambiaje Nyerere amenilea kimwili?You are joking.To me his was just another style of an evil dictatorship.Watanzania tuko wajinga sana,tumeamini kwamba hawa watu ni tofauti,no, they are not.Wanachofanya ni kupokezana vijiti.They have the same father.
 
Tatizo bado lipo palepale na linajionyesha wazi miongoni mwetu kila siku. Tatizo la fikra finyu kwa sababu ya kutopenda kuongeza maarifa hasa kwa kusoma vitu mbalimbali na kutopenda hata kujua historia za familia zetu wenyewe achilia mbali kabila labda na nchi. Tanzania haimuhitaji Nyerere kwa sasa na haimuhitaju mtu yeyote wa mfano wa Nyerere. Tanzania inahitaji watu haihitaji mtu. Tanzania ilifika pale ilipokuwa sababu ya watu. Watu hao ndio waliomuibua Nyerere, Nyerere hakuibuka tu. Nyerere ndiye aliyetuletea matatizo yota haya. Alipopata nguvu akawafanya wananchi waamini kuwa ni Nyerere tu, jambo ambalo si kweli, ameondoka watu wanafikiri ni Nyerere tu. Nguvu alizokuwa nazo amezitumia kujijengea himaya yake na amewajengea watanzania namna ya kufikiria. Hata yeye aliiona hatari hiyo baadae lakini akawa amechelewa kuvunja himaya yake. Watanzania wanahitaji sio wanataka maana walio wengi hawajui wanachokitaka, wanataka mfumo wenye kuwapa wananchi madaraka ya kuwawajibisha waliowapa dhamana ya kuwaongoza. Hawahitaji tena mtu kama Nyerere wa kumuabudu. Zama hizi na zile ni tofauti sana. Ujanja ujanja wa Nyerere wa kudanganya watu kuwa wamarekani ni adui zake wakati yeye ni agent wake umepita. Wakati wa viongozi kufoka na kutoa amri si huu, ni wakati wa wananchi wenye maarifa kutambua vipaumbele vyao na kuwatuma waliowajiri wavitekeleze. Wananchi wa Tanzania wantakiwa wahangaike kutafuta maarifa kwanza na waachane na uvivu wa kufikiri ambao hata humu JF watu wanauonyesha hata bila ya kuona aibu. Sio Membe, sio Slaa, Lowasa wala jina lolote liwalo linaloweza kubadilisha maisha ya watanzania bali watanzania wenyewe. Tuache kuchangia mamilioni kwenye vikao vya harusi tuwanunulie watoto wetu vitabu. Tuache kujaza mikono yetu simu kibao za mikononi wakati nyumbani kwetu hata kitabu kimoja cha kusoma hatuna. Tuache kuongeza cholestol katika miili yetu kwa nyama nyoma badala yake tujenge tamaduni za kununua vitabu. Tutafute maarifa kwanza kabla ya kutaja majina wala chama. Tofauti kubwa iliyopo kati ya mataifa yaliyoendelea na yasiyoendelea si utofauti wa rasilimali bali ni utofauti wa maarifa. Hata uwe na rasilimali ngapi kama huna maarifa ni bure. Hata uwe na wagombea waliotumwa na Mungu kama huna maarifa ya kuwatambua kamwe hutaweza kufanya uamuzi sahihi. Tutafute maarifa kwanza tuondokane na uvivu wa kufikiri
 
Back
Top Bottom