Wasifu wa Ally Salum Hapi

Peres

Member
Aug 15, 2011
7
7
Ally Salum Hapi ni kijana mzaliwa wa Nzega mkoani Tabora. Kijana huyu anayetoka katika familia ya kawaida kabisa (si ya kitajiri au uwezo wa kifedha) alipata elimu yake ya shule ya Msingi humo humo Mkoani Tabora. Baadae alichaguliwa Kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya Ufundi ya Wavulana Bwiru iliyoko jijini Mwanza. Akiwa Bwiru Boys aliweza kuchaguliwa kuwa Kiranja Mkuu (Head Prefect) akiwa kidato cha pili tu. Hii ilichangiwa na uwezo wake wa ushawishi na ujenzi wa hoja kama alivyokuwa amejitanabaisha miongoni mwa wanafunzi. Ni katika Uongozi wake aliwashawishi wanafunzi wenzake kugoma na wao pasipo kujua nia yake walifanya hivyo. Katika mgomo huo aliwasaliti wenzake na akapelekea wanafunzi 15 wakifukuzwa shule ilihali yeye akibaki na hivyo kufanikiwa kumaliza shule japo hakufanya vizuri katika masomo ya ufundi (Technical subjects) hasa Fizikia lililokuwa kiungo kwa machaguo yote na hivyo kutopata chaguo la Serikali.

Kijana huyu alijiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule moja ya binafsi jijini Dar es Salaam huku akiamua kusoma masomo HKL (History, Kiswahili and Language). Ikumbukwe kuwa hakuwa kusoma somo la Historia akiwa ‘O’ level lakini alilazimika kulisoma akiwa ‘A’ level. Mungu si Athumani Kijana huyu alifaulu kwa Kupata Daraja la Kwanza pointi 4, na hivyo kujiunga na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Kitivo Cha Sheria mwaka wa masomo 2007/2008. Akiwa mwaka wa kwanza alijaribu kujitangaza vya kutosha na hata Kufikishwa katika Kamati ya Maadili na Akina Owawa Stephen na David Silinde (Mbunge wa Mbozi Magharibi kupitia Chadema). Cha ajabu katika kamati hiyo aliwasingizia kina Silinde, Owawa na Selemani Ally kuwa ndio wahusika wakuu, hivyo aliwasaliti katika makubaliano yao ya mwanzo na ya pamoja. Akiwa Chuoni alifanya harakati ili awe Rais wa serikali ya wanafunzi –DARUSO. Katika harakati zake alikutana na vigogo wa CCM katika Hotel ya Travertine iliyoko Magomeni na kupatiwa fedha za kampeni na kuhonga wenyeviti wa Vitivo ili wampitishe. Baada ya hapo alikwenda kwa M/Kiti wa Kamati ya Bunge Mashirika ya Umma (wa Bunge la Tisa) na kuomba laki sita (Tsh 600,000/-) ili afanyie maandalizi ya kuwa mgombea (awahonge wenyeviti).

Baada ya harakati zake zote mwisho wa siku wakambwaga chini maana wanachuo wa UDSM si wakuchezea na alidhani kuwa atawahonga na fedha za mafisadi na kisha atapita. Hela walikula na bado wakamtosa. Hapo ndipo raha ya siasa. Alikuja kuambulia Ubunge wa kuteuliwa kutoka kwenye Kitivo chake cha Sheria. Akiwa Mbunge, Bunge la DARUSO kwa kauli moja lilimwamini na kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ya DARUSO mwezi Machi 2010. Bajeti kwa ajili ya kamati hii ilipitishwa na yeye kama Mwenyekiti wa Kamati alichukua Tsh 1,000,000 kwa ajili ya kazi mbali za Kamati katika kushughulikia Mabadiliko ya Katiba kwa maana ya Kuratibu mapendekezo na maoni ya wanafunzi chuoni. Cha ajabu hakuitisha hata kikao kimoja na wajumbe wake, pesa akala na hakuna mapendekezo yoyote aliyowasilisha. Bunge la wanafunzi lilipotaka kujua sababu za kutokuwepo mapendekezo ya katiba, lilivunjwa eti muda wake umeisha.

Hivi karibuni alipitishwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa –UVCCM. Sina shaka na siasa zake za jukwaani maana anajenga hoja ipasavyo na anajiamini na hutetea kile anachokiamini hata kama ni cha kiusaliti/kinafiki au kifisadi. Shaka yangu iko katika Uadilifu wake, na Uzalendo wake kwa Vijana wenzake na taifa kwa Ujumla.

Kijana huyu si Mwadilifu na si Mzalendo na anaweza kununuliwa kwa bei rahisi sana kiasi cha kuuza uzalendo kwa wenye pesa. Kwa sasa anafanya kazi “Crest Attorneys” ofisi ambazo ziko jingo la Coronation, mtaa wa Samora/Azikiwe. Ukitaka kuwaona utawapata katika jengo hilo ghorofa ya pili. Pamoja na kufanya kazi pale, Salum Ally Hapi amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu sana na ofisi za Ridhiwani Kikwete za GRK Advocates.

Ni uwazi usioshaka kuwa kijana huyu ana nguvu ya Riz1 katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Umakamu Mwenyekiti Taifa-UVCCM. Huyu ndiye Salumu Ally Hapi anayeonekana kupererusha vyema nafasi hiyo katika masikio ya walio wengi, huku ikiwa ni Kinyago kilichochongwa na wenye Pesa kuwakilisha maslahi yao ndani ya Umoja!

Huyu ndiye Ally Salum Hapi. Kila la Heri!

Salumu.jpg
 
Ally Salum Hapi, CCM, Wa Tabora na mpenda short cut, kila kitu kipo pema kabisa.

Infact kwa dini yake na hiyo tabia ana kila sababu ya kufaulu na kwenda mbali sana kisiasa.

Wa Tabora mwenzangu, changamka ule mapema maana ikifika mwaka 2015 unaweza ujikute huna pa kwenda.

Sasa Mwana sheria mzima anajipendekeza, si ndiyo hawa anawasakama Mchungaji Msigwa?

 
Last edited by a moderator:
Mhhhh yetu macho wanaweka watu wao bana si unajua 2015 watakuwa hawako madarakani lazima waweke mizizi
 
Sikonge,

Mchungaji mwenyewe povu linamtoka akisikia Mwakalebela 2015 ndo mwisho wake kuitwa Mheshimiwa Mark my word
 
Last edited by a moderator:
HUYU ANAPANGA MIKAKATI YAKE PALE BRAKE POINT MJINI NILIMWONA 1DAY hafai
 
Pamoja na kuwa ni mtumishi wa magamba, kuna kitu kimenivutia kwenye historia yake.
Jamaa alitoka shule ya Tech O-level, akasoma HKL Advance including History ambayo hakuwahi soma O level lakini bado akasukumia mabanda mawili na B moja, yaani div 1 point 4. Basi jamaa ni mkali sana!
 
Duuu siasa za kupandikizwa mbaya sana kwa vijana,unafiki ni sumu mbaya zaidi ya yoote!acha wachaguane wafu kwa wafu!!
 
Kwa CCM iliyopo sasa huyu ndiye anaye wafaa sana, maana anahistoria nzuri sana ya rushwa, ufisadi na fitina, vitu ambavyo ndio ''Operating System'' ya CCM kwa sasa.

Na kwa kuwa anafadhiliwa na mtoto wa Sultani(Ridhwani) basi uwezekano wa kushinda ni mkubwa sana.

Najua huyu Hapi anaungwa mkono na kundi la urais la USULTANI(Membe group) akipambana na Paul Makonda Kutoka kundi la urais la ZILIPENDWA(Sitta group). Bado sijajua mgombea wa kundi la UFISADI (Lowassa group) ni nani.

Ni mambo yaliyo wazi sana kuwa hakuna lolote la maana kwenye uchaguzi wa UVCCM zaidi ya kupigana viti(Mara), kushinikiza kupewa chai(Morogoro), kuhamasishwa kuvuta bangi(Mara), Fujo na matusi(Dar), Kuhongwa chai na vitumbua(Nzega), Maombolezo ya kifo cha CCM(Tanga) nk.
 
Pamoja na kuwa ni mtumishi wa magamba, kuna kitu kimenivutia kwenye historia yake.
Jamaa alitoka shule ya Tech O-level, akasoma HKL Advance including History ambayo hakuwahi soma O level lakini bado akasukumia mabanda mawili na B moja, yaani div 1 point 4. Basi jamaa ni mkali sana!

hiyo mbona ipo tu,kuna kijana wangu mmoja alilamba zero form six PCB akarudia mwaka shule combination ya HKL akalamba one ya tano.alisoma mazengo o level na alikuwa hajawahi kusoma history.
 
Ana akili sana km alisoma masomo ya sayansi akahama kabisa na kwenda kufaulu arts kwa div one kali kichwa kizima kile.hayo mengine ni majungu tu
 
Hapi wapige mboko za mgongo hao,tunajua unawakimbiza ndio mana hawalali wanaishia kukuchafua
 
Wenye uwezo huwa hawakosi maadui,hawa wanaokesha mtandaoni kuchafua wenzao ni njaa zinawasumbua
 
Kiukweli huyu kijana ni mpambanaji na ana akili ya ubunifu sana.ukiwa na roho ya kwa nini lazima umchukie mana ana uwezo wa kufanikiwa mahali ambapo wewe huwezi.he can make things hapen
 
Ana akili sana km alisoma masomo ya sayansi akahama kabisa na kwenda kufaulu arts kwa div one kali kichwa kizima kile.hayo mengine ni majungu tu

Mtu wa Sayansi kufaulu arts with flying colours jambo la kawaida sana, wala sio ajabu. Wangapi wanapiga PCM/PCB, chuo wanasoma B. Com/ Law na kufaulu vema sana?
Hakuna la ajabu hapo.
Kuna wenye MD(MADAKTARI) wamesoma MBA na kutoka na ma "Suma cum Laude"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom