Huyu ndiye Abdulrahman Kinana, nguli wa siasa nchini

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Kinana alizaliwa mwaka 1952 mkoani Arusha. Ni mwanasiasa aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini, zikiwemo; Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Naibu Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa kipindi cha miaka 10 na Spika wa Bunge la Afrika mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006. Pia, alishawahi kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha kwa muda wa miaka 10.

Kinana alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani. Pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006.

Kinana aliwahi kutumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa muda wa miaka 20 na hatimaye kustaafu kwa cheo cha ukanali.

Kinana aliteuliwa kushika ya Ukatibu Mkuu wa CCM mwaka 2012 kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Wilson Mukama.

Ni kiongozi ambaye aliyeleta uhai wa CCM. Kipindi chake cha uongozi cha miaka sita kiliwafanya wana-CCM watembee kifua mbele, wakati kabla ya hapo waliona hata aibu kuvaa sare za CCM mitaani. Kinana alipambana na viongozi wa Serikali wasiotimiza wajibu wao.

Kinana alifanya kazi kubwa ya kuzunguka mikoani kuangalia utekelezaji wa miradi ya Serikali, hakuwa na simile kwa watendaji wa Serikali walioonekana kukwamisha miradi ya maendeleo. Mfano, akiwa ziarani kwenye mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya, waliwataja wazi wazi mawaziri wane wa Serikali ya Awamu ya Nne kuwa wameshindwakutekeleza Ilani ya CCM.

Ziara za Kinana ziliinua uhai wa CCM nchi nzima na kuongeza kasi ya utekelezaji wa ilani na kutatua kero za wananchi kwenye maeneo yao, kiasi cha kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho tofauti na ilivyokuwa awali.

Utendaji kazi wa Kinana akiwa Katibu Mkuu wa CCM uliwavutia baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini na kuamua ‘’Kuunga mkono juhudi’’ kwa kuhamia CCM kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuwaletea maendeleo wananchi.

Hivyo, Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kumpendekeza jina Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ni jambo sahihi hivyo wana CCM na Wananchi kwa ujumla watarajie kilicho bora kutoka CCM katika nafasi aliyopendekezwa kwani Kinana ni mchapakazi, mweledi, mzalendo na anarekodi ya ufanisi katika mikakati ya kisiasa na uongozi wenye matokeo chanya ambayo yalionekana katika awamu zote serikali kuanzia Serikali ya Awamu ya Nne mpaka Awamu ya Tano.

Na;
Dkt. B.G. MATIKO
31/03/2022
 
Na Mwl Udadis

KUZALIWA

- Abdulrahman Omar Kinana alizaliwa mwezi October mwaka 1951 Mkoani Arusha.

TAALUMA

- Shahada ya sayansi ya siasa na uhusiano wa kimataifa kutoka katika Chuo kikuu cha Ljubljana nchini Yugoslavia.

- Shahada ya Uzamili katika Siasa, mikakati na Utawala wa Jamii kutoka katika Chuo Kikuu cha Havard

UZOEFU KATIKA SHUGHULI ZA UTUMISHI UMMA NA UONGOZI

- Afisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, TPDF kwa muda wa miaka 20 akikasimishwa majukumu mbalimbali na kuyatekeleza kwa weledi na hatimaye kustaafu kwa cheo cha ukanali.

- Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

- Naibu Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa.

- Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

-Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa kipindi cha miaka 10.

- Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi. Katika kipindi hiki Chama cha Mapinduzi kilipitia mabadiliko yaliyolenga kuhuisha ari, kasi na nguvu kubwa kiutendaji, Ndugu Kinana akiwa mtendaji Mkuu.

- Spika wa Bunge la Afrika mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006 akitumikia kwa weledi wa hali ya juu ya kuweka historia katika kuimarisha Jumuiya ya Afrika mashariki.

SIFA ZA KIPEKEE KATIKA KUMBUKUMBU ZA UTUMISHI NA UONGOZI WAKE

- Uchapakazi, weledi, uzalendo na kujituma

- Heshima na uamunifu katika jamii za kimataifa katika usuluhishi wa migogoro na utengamano wa Afrika mashariki.

- Rekodi ya ufanisi katika mikakati ya kisiasa na uongozi wenye matokeo

- Uzoefu wa kiuongozi katika bodi mbalimbali za masharika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yaliyofanya vizuri.

- Mwanazuoni na muumini wa umajumui wa Afrika.

00380034_d01bae0e1e681d6c198eeefce00a4d76_arc614x376_w735_us1.jpg
 
Anafaa Sana na anauzoefu na kazi mzee wetu mangula apumzike tu ametutumikia Sana katika wadhfa huu tunamshukuru kwakweli.
 
CCM tuna imani nae, ila yale mambo yake ya kashfa ya uwindaji tembo zifutike, wananchi hawapendi kusikia kiongozi unayemwamini, anasikika au kusemakana ana winda tembo. Hii inachafua sana Chama na hata imani yetu kwake inatoweka.
 
Kinana alizaliwa mwaka 1952 mkoani Arusha. Ni mwanasiasa aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini, zikiwemo; Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Naibu Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa kipindi cha miaka 10 na Spika wa Bunge la Afrika mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006. Pia, alishawahi kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha kwa muda wa miaka 10.

Kinana alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani. Pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006.

Kinana aliwahi kutumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa muda wa miaka 20 na hatimaye kustaafu kwa cheo cha ukanali.

Kinana aliteuliwa kushika ya Ukatibu Mkuu wa CCM mwaka 2012 kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Wilson Mukama.

Ni kiongozi ambaye aliyeleta uhai wa CCM. Kipindi chake cha uongozi cha miaka sita kiliwafanya wana-CCM watembee kifua mbele, wakati kabla ya hapo waliona hata aibu kuvaa sare za CCM mitaani. Kinana alipambana na viongozi wa Serikali wasiotimiza wajibu wao.

Kinana alifanya kazi kubwa ya kuzunguka mikoani kuangalia utekelezaji wa miradi ya Serikali, hakuwa na simile kwa watendaji wa Serikali walioonekana kukwamisha miradi ya maendeleo. Mfano, akiwa ziarani kwenye mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya, waliwataja wazi wazi mawaziri wane wa Serikali ya Awamu ya Nne kuwa wameshindwakutekeleza Ilani ya CCM.

Ziara za Kinana ziliinua uhai wa CCM nchi nzima na kuongeza kasi ya utekelezaji wa ilani na kutatua kero za wananchi kwenye maeneo yao, kiasi cha kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho tofauti na ilivyokuwa awali.

Utendaji kazi wa Kinana akiwa Katibu Mkuu wa CCM uliwavutia baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini na kuamua ‘’Kuunga mkono juhudi’’ kwa kuhamia CCM kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuwaletea maendeleo wananchi.

Hivyo, Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kumpendekeza jina Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ni jambo sahihi hivyo wana CCM na Wananchi kwa ujumla watarajie kilicho bora kutoka CCM katika nafasi aliyopendekezwa kwani Kinana ni mchapakazi, mweledi, mzalendo na anarekodi ya ufanisi katika mikakati ya kisiasa na uongozi wenye matokeo chanya ambayo yalionekana katika awamu zote serikali kuanzia Serikali ya Awamu ya Nne mpaka Awamu ya Tano.

Na;
Dkt. B.G. MATIKO
31/03/2022
Al shabab inarudi tena ni suala la muda tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom