Huyu ndio Shujaa wetu hayati John Pombe Magufuli - Rais wa Watanzania na kimbilio la wanyonge

Tuache unafiki, ametuachia Ukabila, ametuchia chuki, ametuachia deni kubwa sana la Haifa, ametuachia umaskini uliotamalaki. Alikua na mema machache
Kwa kifupi amelirudisha taifa nyuma mara mia moja, ameacha mikosi na mabalaa ya kila aina
 
Mbn mnatumia Nguvu kubwa ?
The passed one he had did nothing the issue of an assassination attempt it unforgettably , Lissu is prophet Alive.
Ze Inglishi izi camu wiz ze shipu. Tupende Kiswahili jamani unaweza kutukana pasipo kukusudia.
 
Mods Moderator naomba msiunganishe huu uzi🙏

Tumshukuru sana Mungu kwa zawadi ya uhai wa John Pombe Joseph Magufuli kwa nchi yetu. Ametutoa pagumu sana, ametuthubitishia yaliyoambiwa hayawezekani yanawezekana kwa vitendo

Ametuachia viongozi makini aliowapika kuwa wazalendo kama yeye mwenyewe na ameacha wananchi wengi walio maskini wakiwa na cha kujivunia kwa nchi yao

Ameiheshimisha Tanzania duniani kote kwa kuondoa uhuru wa bendera na kurudisha misingi ya uhuru halisi

Ametuachia serikali makini chini ya aliyekua msaidizi wake makini Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote

Ametuachia jamhuri ya muungano wa Tanzania iliyo imara, bunge imara, mahakama imara na jeshi imara.

Hotuba ya Samia siku ya kuapishwa waziri mkuu, waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje. Hii ni baada ya Samia kuteiliwa na Magufuli kuwa makamu wa rais kwa mara ya pili. Samia alimhakikishia rais amenyooka na kumshukuru sana. Aliahidi kufanya kazi na rais apumzike akifanya mambo makubwa


Hotuba ya rais Magufuli siku ya kuapishwa waziri mkuu, waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje.



🙏🙏🙏


Pole tanzania yangu



Tumuombe Rais wetu Samia Suluhu Hassan aendeleze yale waliyoyaanza pamoja, na Mungu aendelee kumjaza hekma, ampe afya ya mwili, roho na akili katika kulitumikia taifa hili

Rest well our hero President John Pombe Magufuli 💔😭🙏

Asante kwa uzi mwanana! You are genius!
 
Nadhani Mbelgiji atakuwa amepata somo la kutosha kutokana na msiba wa mpendwa wetu, viatu vya marehemu Magufuli ni vikubwa sana na nashukuru JF kwa kumuenzi kwa kuweka rangi nyeusi kuashiria kwamba tupo kwenye msiba,wema,uadilifu na mapenzi aliyokuwa Raisi Magufuli kwa nchi hii ndio unaotutoa machozi na hatuamini kama hatutamuona tena, ni matarajio yetu kwamba ambao watashika hatamu watafuata nyayo za Magufuli, Magufuli ametufanya tutembee vifua mbele ,tujiamini ,tuipende nchi yetu na zaidi ya yote heshima kwa aliyenacho na asiyenacho,tunaamini yale mambo ya '' unanijua mimi nani" au kusimamisha gari katikati ya barabara na kutoa bastola kutishia watu hayatarudi tena. Wakati namlilia raisi wangu mpendwa Magufuli yafaa tu kumuombea kwa Mungu ili ampe pumziko la milele,kwa heri Magufuli hakika ulikuwa mzalendo wa kweli na msalimie Mwalimu Nyerere,ulikuwa mwanafunzi mzuri wa falsafa ya mwalimu pamoja na kuwa hukuwahi kufanya nae kazi au kuwa mwananfunzi wake.
 
Back
Top Bottom