Huyu ndio Rais wa watu aliyeinuliwa kwa ajili ya watu; kisa cha teja part II

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Moja ya sifa kubwa iliyowafanya Wamalaysia tuliokuwa nao sawa kiuchumi miaka 50 iliyopita kutuacha nyuma ni utendaji kazi wa kukunja ndita.

Wamalaysia na hata Wachina walipoamua Kazi tu leo sote tunataka kwenda kufaidi matunda yao na kufaidi katika nchi zao; ndio maana naendelea kumsihi yule swahiba wangu teja katika kisa kilichopita aachane na mawazo ya kuzamia meli kwenda nje.

Tanzania hii hii itakuwa Kuala Lumpur au Beijing ya Afrika kama sote tutaamua kwenda katika fasafa moja.

Ukiacha rafiki yangu teja kuna waliopata kulalamika sana kuhusu uzembe na rushwa katika utumishi wa umma ingawa sasa wanasaka vijisababu lakini ukweli ni kwamba sasa maradhi hayo yote yamepata mtaalamu bingwa wa upasuaji.

Kuna watu walilalama sana kuhusu madini kuwa tunaibiwa, ingawa sasa wataanza kugeuka kuwa upande wa wazungu (kwa kuwa wanaugua maradhi yaitwayo saddisim) lakini sasa wao wanajua na dunia inajua kuwa hatutaibiwa tena kirahisi katika Madini.

Waliwahi kubeza kuwa tunauongozi legelege na unatakiwa wa kukunja ndita.Amekuja wa kukunja ndita na ndita imeshakunjwa na mashambulizi yanaendelea nasikia wameanza kuitamani jana.

Katika dunia inayohaha kuwa na viongozi thabiti na wanaoishi kuyaenzi matendo mema- msingi wa maisha bora kwa watanzania naomba mniruhusu nitoke nje kifua wazi na nitembee kwa kujigamba kuwa Tanzania tunaye Dkt. JPM na hakuna wa kumfananisha naye.

Analeta matumaini palipo na shaka, analeta furaha penye huzuni na zaidi analeta mageuzi penye mageresho.

Hivi watanzania tunataka nini zaidi??

*Political Jurist, UDOM*
 
Back
Top Bottom