Huyu ndio mtumishi wa umma wa awamu hii

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
Miezi karibu sita kapita katika tanuru la uhakika,tanuru lenye mabonde, milima na miba maana zoezi hili lilikuwa na gharama zake kwa watumishi ikiwa ni pamoja na usumbufu mbalimbali ulioambatana na zoezi hili kama vile kushinda kwenye foleni,n.k.

Wako waliosafiri umbali mrefu kufuata vyeti,wako waliotoka vyuoni kurudi makazini kwa ajili ya kuhakikiwa,wako waliolazimika kwenda baraza la mitihani kwa ajili ya kusaka vyeti, wako waliolazimika kutangaza kupotelewa vyeti ili wapate vyeti vyao na wako waliolazimika kwenda polisi kuripoti kupotolewa vyeti vyao,n.k.

Pamoja na yote hayo,mtumishi huyu mpaka leo hii hajui kama kuna nyongeza ya mshahara na kibaya zaidi hata madai yake mbalimbali hajui atalipwa lini!Waliondolewa kazini nao hatima yao haijulikani.

Ukitaka kuchoka zaidi juu ya kazia hii inayowakabili watumishi, wasikilize wenye dhamana wanapohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu matatizo haya ya watumishi na majibu wanayoyatoa.

Utawasikia kila siku wanaongelea mambo yale yale yaani ni mipango na michakato isiyo na timeframe huku wakikwepa kujibu maswali ya msingi na kupiga siasa tu maana shida hizi wao haziwahusu.Yaani ni mwendo wa ku-buy time tu.

Cha ajabu na cha kushangaza ni jinsi mtumishi huyu anavyopelekeshwa wakati maslahi yake yamesahaulika.

Kwa mfano, hivi sasa wameibuka ma-RC ambao wamekuja na kauli za kuwabeza na kuwadharau kama vile kuwaita watumishi hawa mizigo, kuwadhalilisha mbele ya akadamnasi, n.k.

Kama hiyo haitoshi,baadhi ya watumishi hawa sasa wanakabiliwa na tishio jipya la makato ya asilimia 15 kwa ajili ya kulipia deni la bodi ya mikopo huku mshahara ukiwa ni ule ule.

Hivi katika hali ya kawaida mtumishi huyu morali ya kazi anaitoa wapi?

Kabla ya kuwaza kuwatimua na kuwasema hadharani huku miktaka kuona tija kutoka kwao, jiuluzeni kwanza kama nanyi mnatimuza wajibu wenu kama waajiri kwa watumishi hawa.

Jamani hata ng'ombe huwezi kumkamua kama huumpi majani hivyo acheni kujisahau kwani hawa nao ni binadamu kama nyie na wanahitaji kuthaminiwa na zaidi wanastahili kupewa incentives wawapo makazini

Msisahau kura mlizopewa nyinyi ni kura walizonyimwa wenzenu hivyo msijisahau na muwe considerate.
 
Miezi karibu sita kapita katika tanuru la uhakika,tanuru lenye mabonde, milima na miba maana zoezi hili lilikuwa na gharama zake kwa watumishi pamoja na usumbufu mbalimbali ulioambatana na zoezi hili kama vile kushinda kwenye foleni,n.k.

Wako waliosafiri umbali mrefu kufuata vyeti,wako waliotoka vyuoni kurudi makazini kwa ajili ya kuhakikiwa,wako waliolazimika kwenda baraza la mitihani kwa ajili ya kusaka vyeti, wako waliolazimika kutangaza kupotelewa vyeti ili wapate vyeti vyao na wako waliolazimika kwenda polisi kuripoti kupotolewa vyeti vyao,n.k.

Pamoja na yote hayo,mtumishi huyu mpaka leo hii hajui kama kuna nyongeza ya mshahara na kibaya zaidi hata madai yake mbalimbali hajui atalipwa lini!Waliondolewa kazini nao hatima yao haijulikani.

Ukitaka kuchoka zaidi juu ya kazia hii inayowakabili watumishi, wasikilize wenye dhamana wanapohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu matatizo haya ya watumishi na majibu wanayoyatoa.

Utawasikia kila siku wanaongelea mambo yale yale yaani ni mipango na michakato isiyo na timeframe huku wakikwepa kujibu maswali ya msingi na kupiga siasa tu maana shida hizi wao haziwahusu.Yaani ni mwendo wa ku-buy time tu.

Cha ajabu na cha kushangaza ni jinsi mtumishi huyu anavyopelekeshwa wakati maslahi yake yamesahaulika.

Kwa mfano, hivi sasa wameibuka ma-RC ambao wamekuja na kauli za kuwabeza na kuwadharau kama vile kuwaita watumishi hawa mizigo, kuwadhalilisha mbele ya akadamnasi, n.k.

Kama hiyo haitoshi,baadhi ya watumishi hawa sasa wanakabiliwa na tishio jipya la makato ya asilimia 15 kwa ajili ya kulipia deni la bodi ya mikopo huku mshahara ukiwa ni ule ule.

Hivi katika hali ya kawaida mtumishi huyu morali ya kazi anaitoa wapi?

Jamani hata ng'ombe huwezi kumkamua kama humpa majani hivyo acheni kujisahau kwani hawa nao ni binadamu kama nyie na wanahitaji kuthaminiwa na zaidi wanastahili kupewa incentives wawapo makazini.

Msisahau kura mlizopewa nyinyi ni kura walizonyimwa wenzenu hivyo msijisahau na muwe considerate.
Nadhani umejitahidi sana kuwakilisha kilio chao. Nimeenda zaidi hapa unaposema wasisahau kura walizopewa ni zile zile walizonyimwa wenzao wa upande wa pili. Hata hivyo labda mambo yataanza kufunguka soon maana wale waliosimamishwa tayari wameanza kurudisha kazini.
 
Kweli kuna walioanza kurudishwa kazini?
 
Ukiona mshahara mdogo acha kazi.
Kajiajiri ili upate kipato kikubwa.
Hakuna haja ya kulalamika kila wakati.
 
Ukiona mshahara mdogo acha kazi.
Kajiajiri ili upate kupato kikubwa.
Hakuna haja ya kulalamika kila wakati.
Wakati wa kampeni mpaka push up mnapiga na lugha za aina hii huwezi zisikia ila mkishachaguliwa mnaota mapembe.

Nawaambieni ipo siku kiburi na jeuri hii vitaisha na hamtoamini macho na masikioni yenu.

Mmejaa kiburi,dharau na majivuno kanakwamba hii dunia ni yenu na mmeongea na mungu na mnadharau historia ya mabadiliko katika mataifa mengine mkiwachukulia poa watanzania.

Mngekuwa ni watu wa kuona mbali mmeangalia idadi ya wabunge wa upinzani inavyoongezeka kwenye kila chaguzi na jinsi mnavyozidi kuvurunda badala ya kujirekebisha.
 
Nafikiri Kitulo amekuelewa. Udhalimu katika nchi hii hatimaye utafikia mwisho na kwa wadhalimu mwisho wao mbaya wa kutisha.
 
Hahahaaa ..kipindi cha danganya toto
kuna siku niliwaza nikafika mbali sana.Bila kupigiwa simu na mke wangu kunibadilisha uelekeo nafikiri mamboo yangekuwa mengine siku ile. Haiwezekani mtu nimekaa kwenye daraja moja miaka 10 halafu unapandishwa daraja mtu mjinga mmoja anazuia tusilipwe mshahara wa daraja jipya?
 
Kweli kuna walioanza kurudishwa kazini?
Ndiyo mkuu, mbona una mashaka? Mi sijawahi kuandika propaganda! Baadhi walirudishwa mwezi Novemba na kwa mujibu wa mikataba yao mipya, wanatambulika kuwa walianza kazi tarehe 1/11/2016. Mkataba wa mwanzo umefutwa, na hii inamaana kwamba hawawezi kudai arreas za mishahara kwa kipindi chote walichosimamishwa.

Amino niyasemayo mkuu Salary Slip!
 
bodi wakate tu maana ndo kuwahi kumaliza deni ili na wengine wenye uhitaji wakopeshwe
 
Ndiyo mkuu, mbona una mashaka? Mi sijawahi kuandika propaganda! Baadhi walirudishwa mwezi Novemba na kwa mujibu wa mikataba yao mipya, wanatambulika kuwa walianza kazi tarehe 1/11/2016. Mkataba wa mwanzo umefutwa, na hii inamaana kwamba hawawezi kudai arreas za mishahara kwa kipindi chote walichosimamishwa.

Amino niyasemayo mkuu Salary Slip!
Sasa Mtu kafanya kazi tangu 1996 halaf unakuja kumfuta kazi na kumrudisha kazini na kuanza mkataba mpya 1nov 2016,hii si dharau kabisa hii maana yke anaanza moja kabisaaa.
 
Ndiyo mkuu, mbona una mashaka? Mi sijawahi kuandika propaganda! Baadhi walirudishwa mwezi Novemba na kwa mujibu wa mikataba yao mipya, wanatambulika kuwa walianza kazi tarehe 1/11/2016. Mkataba wa mwanzo umefutwa, na hii inamaana kwamba hawawezi kudai arreas za mishahara kwa kipindi chote walichosimamishwa.

Amino niyasemayo mkuu Salary Slip!
Ngoja kwanza! Mfano mtu kafanya kazi kwa say, 18 years. Vipi kuhusu pension yake ambayo alikuwa anakatwa miaka yote siku akistaafu itakuwa considered? Au ndiyo kwamba hiyo miaka 18 aliyofanya kazi hakuwa ana-exist???

Sidhani kama ni sahihi na haki. Ngoja watu wa Human Resources Management waje watuambie.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom