Huyu ndio mbunge aliemtaja kweka kushirikina na wahalifu.

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

  • Wednesday, July 18, 2012

Mbunge Joshua Nassari na Kangi Lugola.
Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola kupitia CCM bungeni july 17 2012 amesema polisi wamtafute Fadhili Kweka mwenye mtandao wa uhalifu ndani ya jeshi la polisi.

Amesema "kuna mtandao mkubwa wa uhalifu ndani ya jeshi la polisi na ushahidi ninao, wanatoa kwa wahalifu taarifa za wananchi wanaomiliki silaha ili wahalifu wajue wananchi wana uwezo kiasi gani wa kujihami ili waende kufanya uhalifu, IGP unaenisikiliza naomba anza na mtumishi wenu anaitwa Fadhili Kweka anaomtandao wa uhalifu ndani ya jeshi la polisi, hainiingii akilini anapata wapi taarifa za wananchi wanaomiliki silaha alafu anawapa wahalifu, anzeni na huyo na nitawapa ushahidi wa kutosha"

Hiyo ndio kauli ya Mbunge Kangi Lugola ambae alikua akitoa hiyo mistari wakati wa kuchangia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi…. unaweza kumsikiliza zaidi hapo chini ufahamu yote aliyosema….


4.jpg










 

Madame Speaker kwanini hakumtaka alete Ushahidi wake BUNGENI kama anavyofanya kwa wa CHADEMA?

Au ni UKWELI sababu inatoka ndani ya mtu wa SERIKALI tawala?

Nchi yetu sasa imekuwa, kama KANU ya Kenya kupoteapotea kwa Viongozi Maarufu na Wananchi Maarufu na Mwisho

Wake ni KUPOTEA kabisa kwa chama cha KANU...
 
Speaker hili halihitaji ushahidi? Au hukusikia hizo tuhuma maana ni nzito kwa taasisi yetu hii ya ulinzi - kuwa na mtandao ndani ya jeshi la ulinzi ni hatari ndio maana wananchi wengi tunasema hatuna imani na jeshi la polisi.
 
Kila wakati watendaji utawasikia wakisema jeshi letu ni zuri isipokuwa wachache. Hao wabaya wamebaki wachache kila siku, mwaka hadi miaka. Leo hii naamini askali wabaya ni wnegi kuliko wazuri ingawa watendaji wa Serikali hawataki kusema hilo.

Mbunge huyu naamini anasema kweli kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa polisi. Anawafahamu polisi wetu vizuri.
 
spika tunaomba umwambie mheshimiwa afute kauli hiyo au alete ushahidi
 
mbona lukuvi haombi mwongozo?hauhitajiki ushahidi hapo?spika mwoga na mkandamizaji..mbona tumesahau uspika alipewa na akina chenge?
 
Back
Top Bottom