Huyu ndio "kijana" wa Dr Mwakyembe,aliyemsaidia 99% katika vita ya madawa ya kulevya

Mkuu sijui kama tumeelewana

Hakuna mahali mimi nimesema jamaa ana makosa au hana makosa,wala hakuna sehemu nimemshutumu huyo Jingu.Nilichokiweka ni ukweli wa wapi alipo na kwa sababu gani,pili ni kumsihi Waziri ajiridhishe na kutumia nafasi yake kumuokoa,na tatu ni kumsihi waziri awe na koo/kifua.

Hayo mengine sijajua umeyatoa wapi mkuu wangu Dr
Tunachosema udadisi au utafiti wako ulifanya upande mmoja tu (wa wanaomshikilia huyo kijana gerezani). Udadisi/ utafiti wako huo ulitakiwa ufanyike pia upande wa pili ( wa wakina Mwakyembe) unaoona kuwa kijana huyo kaonewa kushikiliwa gerezani. Kwa kufanya hivyo habari yako ingekuwa balanced. Tunachosema ni kuwa habari yo yote ambayo haiko balanced, hata kama ni nzuri kiasi gani na ina mvuto kiasi gani, inabaki kuwa ni majungu au udaku kwa kiswahili cha sasa.
 
images-172.jpeg
 
Isije ikawa waziri mwenyewe anatuchezea 'keusi kekundu',akijifanya anapambana na madawa ya kulevya seriously kabisa huku akitupiga kwenye tembo.
 
Mwakyembe hamna kitu ndio wale wale, kapiga dili za mabehewa y tren mpaka basi, then anakuja anajifanya kama anauuchuuuunguu vile, alafu awa jamaa bado wanajua kama waTZ hatuna kumbukumbu sijui, yani kuna wakati nakaaaa najiulizaaa awa jamaa wanatuchukuliaje nakosa majibu
 
Hujakosea mejaTz. Kumbuka pia kugawiana nyumba za serikali na mv Dar. Leo hii ndio wanatutangazia kuwa wazalendo zaidi na wapinzani ni maadui wa taifa hili. Hawa watu Mungu atawachoma hapa hapa duniani.
 
Inawezekana kuna mchezo Jingu kachezewa.
Alikua anatumiwa tu kwa kupokea vimemo nae anafanya tu kulinda kibarua.
 
View attachment 472029
View attachment 472030

Juzi kati Waziri wa Katiba na Sheria Dr.Mwakyembe alisikika kupitia kipindi kimoja cha "East Africa Tv/Radio" akilalamika jinsi alivyomshindwa Masogange katika vita vya madawa ya kulevya.Dr Mwakyembe anasema hata baada ya ushahidi wote kuonyesha kuwa "mzigo" ulipitishwa hapa Dsm kuelekea J'burg,lakini bado Masogange alimponyoka.

Anasema,baada ya muda,alihamishwa ktk Wizara hiyo na kupelekwa sehemu nyingine,kitu kilichomfanya ashindwe kuendeleza harakati za vita hiyo.Sisi tutamuamini Dr kwa yale anayoyasema,wengi wanaomfahamu wanasita kumuamini.

Lakini haya yote,hayaondoi ukweli kuwa,Dr Mwakyembe,daktari wa sheria,mwanazuoni,wakili,Waziri na Mbunge wa Jimbo la Kyela,alielemewa na Masogange mpaka akawa anamletea "nyodo".

Mjadala mkubwa aliouibua Dr Mwakyembe,ni huyo "kijana" wake aliyekuwa "anamsaidia" katika vita hivi,bahati nzuri au mbaya,licha ya kusema "kijana" wake anatakiwa alindwe huko gerezani,bado Dr aliamua kumtaja kwa jina moja la JINGU,hivyo aliotoa mwanya wa kudadisi;Huyo "kijana wake Jingu ni nani haswa?"

Dr Mwakyembe hajasema huyo "kijana" wake alifungwa kwa kosa gani hasa,yeye kama mwanasheria na waziri,ametumia njia gani za kisheria kuhakikisha huyo "kijana" wake anatoka huko gerezani?Na je Mwakyembe ana uhakika kuwa huyo "kijana" wake aliomsaidia kwa 99% ni kweli yupo huko gerezani kwa "kubambikiwa" au ni stahili yake.

Na je,kukamatwa kwake huyo "kijana" kuna uhusiano wowote na "msaada" kwa Dr Mwakyembe?Au kukamatwa kwake "kunahusishwa" tu,lakini kuna jambo lingine tofauti na "msaada" huo kwa Dr?

Clemence Jingu Mbaruck (bila shaka ndio huyu "kijana" wa Dr Mwakyembe) alikuwa Meneja wa Usalama (Manager Security) wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania.Alihudumu kwa nafasi andamizi kabla ya cheo hicho katika kitengo cha Usalama katika uwanja wa Julius Nyerere kwa muda mrefu.

Kwa maelezo ya Kamishna Rogers Sianga,moja ya mbinu kubwa ya "drug lords" ni ku-recruit watu ktk kila kitengo wanachopita ili iwe rahisi kwao kupitisha mizigo yao,kitengo cha usalama ktk viwanja vya ndege,ni moja ya "waajiliwa" wa mitandao hii.Hivyo hawa huwa na "details" za lini,saa ngapi,nani,na ndege gani itapitisha mzigo kuingia au kutoka nje ya nchi.

July 2015,mzigo wa kilo 262 wa pembe za ndovu ambao ni sawa na tembo 50 ulikamatwa katika uwanja wa ndege wa Zurich Uswis,ukiwa umetoka Dsm kuelekea China.

Mzigo huo ulikamatwa ukiwa ndani ya begi za raia wa China.Begi hizo zilipita bila kuonekana Tanzania, iwe kwa macho au kwa "Screening machine".
Soma Nyara za Serikali zawafikisha kizimbani Maafisa 4 wa TAA

Watuhumiwa wanne ambao ni wafanyakazi wa Kitengo cha Usalama wakiwemo wanajeshi watatu wa JWTZ (ambao huwa wapo attached ktk kitengo cha usalama wa kiwanja) na Manager Security Jingu walitiwa kizuizini kwa tuhuma za kuhisika kufanikisha mzigo huo kupita bila kukamatwa.

Clemence Jingu (kijana wa Mwakyembe) na wenzake waliwekwa mahabusu kwa tuhuma ya Uhujumu uchumi,na kesi yao kusomwa mahakama ya Kisutu na baadae kurudishwa rumande sbb kesi hii haina dhamana.

Mpaka leo,Jingu yupo ndani akiendelea kusota kutokana na kesi hii.Ni kesi inayotambulika kama ya "Uhujumu Uchumi" ambayo haina dhamana.Kukamatwa kwa Jingu kulitokana na nafasi yake kama "Manager Security" ambaye inaonekana (sababu mahakama haijathibitisha) alishiriki kufanikisha mzigo huo kupita bila kizuizi.

Huwezi kupita na mzigo wa kilo 262 wa meno ya tembo bila kuonekana kwa macho wala kwa mashine.Ni lazima uwe na mtandao wa maana utakaorambishwa "asali".Mtandao huu wa kuramba "asali" hauishii kwa "security officers" wanaokagua mizigo magetini tu,ni lazima ufike mpaka kwa "boss".Na pengine swali lilikuwa,"mzigo mkubwa kama huu unaweza kupita bila Manager Security kujua?"

Leo Dr Mwakyembe,wakili,Waziri na Mbunge,bila kujali usiri wa taarifa za mtoa taarifa kaamua kututajia hadharani mtu aliyekuwa anamsaidia kwa 99%.Tena kwa kumtaja ktk chombo cha habari.Lakini sidhani kama amejiridhisha kuwa kuwekwa ndani kwa "mtoa taarifa" wake ni kweli kwa sbb ya vita ya madawa ya kulevya?

Na hata kama ni hivyo,Je Dr hana namna ya kisheria iwe kwa kumuwekea mawakili au msaada wowote wa kisheria kuhakikisha "kijana" wake anatoka!?Na ana uhakika kuwekwa ndani kwa Jingu ni sbb ya "uadui wa kutoa ushirikiano wa 99%?".

Zaidi ya hapo,Dr ametuonyesha kuwa hana "kifua",inawezakana huyo "kijana" wake alikuwa anampa habari hizo sbb ni Waziri na bosi wake,sasa inakuwaje leo aamue kutaja chanzo chake cha habari kwa jina na mahali alipo?Alipoamua kumtaja Jingu hadharani,alitupa nafasi ya kudadisi;huyo Jingu "kijana" wa Mwakyembe ni nani?

Leo Masogange na washirika wake na wote waliokamatwa enzi za Mwakyembe kupitia uwanja wa JNIA,wanajua Jingu ndio aliowachoma.Hali hii ya kukosa "kifua" cha kutunza siri unazopewa ktk uwajibikaji,haiwezi kuwakatisha tamaa maafisa wengine wa JNIA katika vita hivi vya sasa?

Maana kwa kauli hii ya Dr,ni wazi kuwa hata maafisa wengine wa usalama JNIA wanaweza kuogopa kutoa taarifa kwa kuhofia siku moja huko mbele ya safari mtu atakuja kutaja chanzo chake cha habari.

Wakati tukimkumbusha Dr Mwakyembe,wakili,mbunge na waziri kufuatilia kwa kina kukaa mahabusu kwa "kijana" wake Jingu kulisababishwa na nini haswaa,pia tumkumbushe kuwa awe na tabia ya kuwa na "kifua".Kifua cha kiume hutunza siri,kifua cha kiume hakiropoki,kifua cha kiume huundwa na mifupa imara ya kustahimili kuhifadhi hata maneno ya kimbea.

Ndio maana,ni nadra sana kukuta wanaume wanasutana kwa maneno ya uwongo na umbea,sababu jadi ya wanaume wa kiafrika ni kukaaa na kufunika siri za jamii na za familia katika kifua.Dr Mwakyembe,zaidi ya udaktari wake,uanazuoni,ubunge na uwaziri;Yeye ni MWANAUME wa kiafrika.
Safi uchambuz mzuri kabisa
 
naunga mkono 1 kwa 1 hii thread, sababu
1. Waziri wa sheria na katiba anatakiwa kuheshimu sheria, ni kosa alilofanya kuelezea jinsi alivyohangaika kumtoa hii ni dhahiri ilikuwa nia ya kupindisha sheria isiyokubalika kikatiba... kuna maswali ya ziada anatakiwa kujibu juu ya hili
2. kwa madudu yaliyotokea alitakiwa kujiudhuru sababu hao yawezekana walikuwa mabosi au security managers walipopatikana wanahatia yeye kama waziri ndiyo bosi mkuu kitengo hicho
3. Nadhani alihusika na dili zilizokuwa zikiendelea ktk utawala uliopita
 
barafu wakati mwingine huwa tunaandika mambo utadhani hatujui utawala wa JK uliakuaje

Enzi ya JK waziri ulikua mshenzi tu mbele ya wenye pesa zao, waziri alikua ni mtu wa kupokea maamrisho na si wakutoa

Si mtetei Dr Mwakyembe lakini siwezi kuidanganya nafsi yangu kwqmba Dr ni moja ya Waziri angalau wanatia moyo kulinganisha na vilaza wengine

Tunaweza kujitia uchizi na kutokutaka kuujua ukweli kwamba enzi za JK wauza ngada walikua untouchable na takataka yeyote achilia mbali Dr

Melezo ya Dr yapo wazi kabisa, pamoja na mamlaka yake yote alishindwa kumkamata Masogange na kijana wake akaangushiwa gunia la mavi........... Huundio ukweli ambao Dr hakua na sababu ya kuukana

Kama kuna mawaziri ambao hawaku fit utawala wa JK Dr Mwakyembe ni mmoja wao
Haku fit kwasababu angalau alikua na uthubutu fulani kugusa pasipo gusika ktk kujaribu kuondoa kero kadhaa
Dr Mwakyembe ana mengi moyoni ambayo anashindwa kuyasema kutokana na viroja alivyokumbana navyo wakati wa JK
Angalau amelisema hili ni kwasababu nafsi yake inamshtaki kwa kuwa yeye ni sababu ya kijana wake kuwa matatizoni

Kimsingi kijana wa Dr sio kusema ni mtakatifu sana...... Hapana
Isipokua kwasababu alikua ameamua kufuata maelekezo ya waziri badala ya waliomuweka basi ilikua hakua budi wamuadabishe
Dr analijua hilo, nafsi inamshtaki kwasababu alidhani ataweza kumlinda lakini enzi za JK wenye nazo ndio waamuzi na walikwisha kuamua kuwa Kijana aadabishwe na Dr aondolewe wizarani

Dr ni mwanasheria anatambua issue ikiwa mahakamani hawezi kuiongelea kwa mapana yake na ndio maana alitoa hints tu

Mkuu barafu nakuomba fanya uchunguzi wako utakuja kujua figisu alilofanyiwa kijana wa mwakyembe, na najua unajua ila hukutaka kuliandika

TANZANIA BILA MADAWA INAWEZEKANA
 
Mkuu Au Wewe ndio Dr.Mwakyembe maana ulivyo jibu tuhuma.Naona unajitetea
 
Waziri wa katiba na sheria kulalamika kwenye vyombo vya habari ni kukosa maadili ya kazi. Nadhani anamjulisha mteuzi wake kuwa amechoka kazi, anataka kurudi kwenye uanaharakati wake. Mkuu yapasa amsikie
 
Badala ya kumtaja msiri wake ni vyema Mwakyembe angeelezea Masogange alimponyoka vipi.?

Sasa kama waziri analialia pamoja na mamlaka zote alizopewa .......vipi akina sie tutakuwa na uthubutu gani wa kupambana na maovu ya nchi hii?
Pengine sumu haijaisha kwenye ubongo
 
barafu wakati mwingine huwa tunaandika mambo utadhani hatujui utawala wa JK uliakuaje

Enzi ya JK waziri ulikua mshenzi tu mbele ya wenye pesa zao, waziri alikua ni mtu wa kupokea maamrisho na si wakutoa

Si mtetei Dr Mwakyembe lakini siwezi kuidanganya nafsi yangu kwqmba Dr ni moja ya Waziri angalau wanatia moyo kulinganisha na vilaza wengine

Tunaweza kujitia uchizi na kutokutaka kuujua ukweli kwamba enzi za JK wauza ngada walikua untouchable na takataka yeyote achilia mbali Dr

Melezo ya Dr yapo wazi kabisa, pamoja na mamlaka yake yote alishindwa kumkamata Masogange na kijana wake akaangushiwa gunia la mavi........... Huundio ukweli ambao Dr hakua na sababu ya kuukana

Kama kuna mawaziri ambao hawaku fit utawala wa JK Dr Mwakyembe ni mmoja wao
Haku fit kwasababu angalau alikua na uthubutu fulani kugusa pasipo gusika ktk kujaribu kuondoa kero kadhaa
Dr Mwakyembe ana mengi moyoni ambayo anashindwa kuyasema kutokana na viroja alivyokumbana navyo wakati wa JK
Angalau amelisema hili ni kwasababu nafsi yake inamshtaki kwa kuwa yeye ni sababu ya kijana wake kuwa matatizoni

Kimsingi kijana wa Dr sio kusema ni mtakatifu sana...... Hapana
Isipokua kwasababu alikua ameamua kufuata maelekezo ya waziri badala ya waliomuweka basi ilikua hakua budi wamuadabishe
Dr analijua hilo, nafsi inamshtaki kwasababu alidhani ataweza kumlinda lakini enzi za JK wenye nazo ndio waamuzi na walikwisha kuamua kuwa Kijana aadabishwe na Dr aondolewe wizarani

Dr ni mwanasheria anatambua issue ikiwa mahakamani hawezi kuiongelea kwa mapana yake na ndio maana alitoa hints tu

Mkuu barafu nakuomba fanya uchunguzi wako utakuja kujua figisu alilofanyiwa kijana wa mwakyembe, na najua unajua ila hukutaka kuliandika

TANZANIA BILA MADAWA INAWEZEKANA
toa upuuzi hapa kama Dr.mwakyembe ni MTU safi kwani asiujiudhuru. au kwanini asijitoe kwernye chama fisadi?? na Je? kwanini anakubali nafasi za uteuzi?? kwenye serlikari ovu??
 
Kama Mwakyembe amekaa kimya miaka miwili leo baada ya Makonda kuwataja wabwia na wauza mihadarati ndiyo anaanza kulia kulia na kumtaja hadharani msiri wake anatoa picha gani.

Kama waziri mzima hana kifua cha kumhifadhi msiri wake je sisi tunaotoa siri kwa askari wa kawaida tutakuwa na usalama gani? Hivi askari hao nao wakitutaja watalaumiwa?

Kama hata IGP yuko chini ya waziri maana humpigia saluti ni nani katika wizara ya mambo ya ndani aliyemzidi waziri kete akamweka Jingu magereza na kisha akamhamisha Mwakyembe wizara kama hapa hamlengi Rais aliyemteua?

Mbona Mwakyembe anakuwa kiongozi popo awke mambo hadharani tutamwelewa?
 
Back
Top Bottom