Huyu ndio Faru Fausta wa Ngorongoro,atimiza miaka 54,aishi chini ya ulinzi wa kijeshi masaa 24

Hiyo picha ni fotoshop, ama ni ya maktaba kutoka maeneo mengine katika Afrika.
Hakuna hapa Tz jeshi la taifa kulinda kitu kiitwacho faru. Kazi hiyo hufanywa na askari wa wanyama pori na sikuhizi wanapewa mafunzo maalumu ya kijeshi-usu(para military).
Huyo askari alivyokaakaa ni kama askari wa Kenya kutokana na mavazi aliyovaa pamoja na aina ya bunduki aliyoshikilia mikononi mwake.
Ili mradi walindwe. ..
 
Una ushahidi? Unafikiri majangili wana bahatisha ama kukurupuka? Wana network kubwa mno hadi game rangers, maofisa wa wizara, idara ya wanyamapori, hifadhi na mapori ya akiba. Wanafahamu nini wanakifanya.

Ndiyo maana kuna kipindi South Africa walianza kuwakata faru pembe zao katika kupunguza kasi ya wao kuuliwa. Lakini watu wa haki za wanyama wakipigia kelele hilo, na likasitishwa.

Hayo nayokwambia yanatokea south africa ambako takwimu zao kila siku wanauawa faru wawili ndio wakaamua kuwatoa pembe lkn bado wakaendelea kuawa
 
Hayo nayokwambia yanatokea south africa ambako takwimu zao kila siku wanauawa faru wawili ndio wakaamua kuwatoa pembe lkn bado wakaendelea kuawa
Weka source kaka. Mbona maneno matupu?
NB: ujangili wa ZA na TZ haufanani hata kidogo. Mimi nilikupa mfano wa faru kukatwa pembe kukuonyesha best practice. Lakini dynamics za ujangili na hata za uhifadhi Tanzania na ZA hazifanani hata kidogo.
 
View attachment 465022

FARU FAUSTA WA NGORONGORO ATIMIZA MIAKA 54
Ndio faru mzee duniani,sasa haoni
.Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi

FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54.
Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona.
Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo.
Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba.
Hivi sasa gharama inayotumika kumlinda Faru Fausta ni kubwa,hivyo uongozi wa Mamlaka umeishauri wizara kuchukua
hatua juu ya Faru Fausta
Uyo Mwanajeshi Ameshika Aina Gani Ya Silaha???
 
Back
Top Bottom