Huyu ndio Camilius Wambura, Inspekta wa Polisi - Mpenda haki

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Nimejawa na furaha kuona mtu makini ndani ya Jeshi la Polisi mwenye uzoefu na weledi anakabidhiwa majukumu makubwa ya kuliongoza Jeshi letu la Polisi. Hakika CAMILIUS WAMBURA ni mtu sahihi mno.

Wengi wetu tunaofuatilia utendaji wa Jeshi la Polisi nchini tulitegemea mabadiliko kufanywa hususani katika nafasi hii muhimu ili kupatikana mtu anayeendana na kasi na dira ya serikali ya awamu ya sita.

Baadhi ya nyadhifa na majukumu ndani ya Jeshi la Polisi yaliyowahi kufanywa na IGP CAMILIUS WAMBURA ni pamoja na;

1. Kamanda wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi - KINONDONI
2. Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi- Makao Makuu
3. Mkurugenzi wa Operesheni- Makao makuu DODOMA
4. Kamanda wa Polisi -Kanda Maalum-DAR ES SALAAM
5. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
6. Na sasa INSPEKTA JENERALI WA POLISI (IGP)

BAADHI YA SIFA ZA KIPEKEE ZA IGP WAMBURA KATIKA UTUMISHI

1. Mpenda haki na muwajibikaji
2. Msomi na mwanataaluma mbobezi ndani ya Jeshi la Polisi
3. Kamanda wa Polisi anayependa kujihusisha na mambo ya kijamii.
4. Mzalendo na mchapakazi katika majukumu mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi
5. Kamanda wa Polisi asiye na makuu na mwenye weledi katika nafasi anazo aminiwa.

UZOEFU KATIKA MAJUKUMU MAKUBWA

-Kamanda wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi - KINONDONI
  • Mkurugenzi wa Operesheni- Makao makuu DODOMA
  • Kamanda wa Polisi -Kanda Maalum-DAR ES SALAAM
  • Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
UMARIDADI NA HISTORIA
  • Utumishi uliotukuka katika medani
  • Uzalendo na uchapakazi katika majukumu mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi
  • Ushiriki katika masula mbalimbali ya kijamii
  • Mwanazuoni aliyefanya vizuri katika masomo na tafiti za kitaaluma
  • Mwakilishi wa Tanzania katika mijadala ya Usalama ya Kimataifa
  • Kachero mwenye uweledi katika kutekeleza Operesheni zenye maslahi kwa nchi yake.
-Kamanda wa Polisi aliyejipambanua katika kutetea haki na kulinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Pamoja na mambo mengine, ajue mtihani wake Mkubwa kabisa pamoja na mingine ni uchaguzi ujao.

Tunamtakia Kila la kheri kwenye majukumu yake.
Hivi watu mnadhani kuna mtu atakae simamishwa na CCM kisha aende kinyume na misingi yao ya miaka yote? HILO SAHAUNI.

Mwaka jana nilisema humu, wanaotegemea unafuuu kwasababu JPM katoka kaingia mwingine ilhali ruling party bado ni ileile wanajidanganya, haya sasa hata miaka haijapita Mama yenu kangia line.

TEGEMEENI YALEYALE KWENYE UCHAGUZI.
 
Hope's nitaishi na kushuhudia mauteuzi haya yanakwisha,hizi nafasi zinatakiwa watu waombe na kufanyiwa usaili SIO kutegemea fadhilia za politicians, ebu angalia candidates wanafanyiwa usaili na kamati ya Bunge, Rais anapelekewa majina 4-6 na yeye amateur Jina moja na anaapishwa na CJ
 
Mbona unatuelezea matukio badala ya sifa? Amelifanyia nini taifa ktk majukumu mbali mbali aliyopewa awali?
Lete na sifa za Kingai tafadhari!

Yaani unamtuhumu Sabaya na kumuweka ndani halafu unamteua Kingai.

Double standard
 
Leo Julai 20,2022 Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi ya Polisi kwa kumteua aliyekua Kamishna wa Polisi Camillus Wambura kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP).

IGP Wambura kitaaluma na kiutendaji ni mpelelezi aliyebobea, mwenye weledi katika nyanja ya upelelezi. Alianza kuonekana tangu enzi za Alfred Tibaigana akiwa Kamanda wa Polisi Dar Es Salaam ambapo kila alipoingia katika jukumu alifanikiwa kudhibiti matukio ya uhalifu kwa asilimia kubwa.
Kabla uteuzi huu, IGP Wambura alishika nyadhifa zifuatazo ndani ya Jeshi hilo.

  • Amekua Mkuu wa Upelelezi (ZCO) Kanda Maalum ya Dar es Salaam
  • Kamanda Wa Jeshi La Polisi, Mkoa Wa Kipolisi Kinondoni
  • Afisa Mwandamizi Wa Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi.
  • Mkuu Wa Oparesheni Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi
  • Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Dar Es Salaam
  • Mkurugenzi wa Operesheni- Makao makuu DODOMA
  • na Mkurugenzi Wa Mashtaka Na Makosa Ya Jinai (DCI).

Mambo mengine yaliyotajwa katika Utendaji kazi wa IGP WAMBURA ni – UADILIFU, MPENDA HAKI, ANAYECHUKIA RUSHWA na MCHAPA KAZI.

Umaridadi wa IGP WAMBURA umeonekana katika
-Utumishi uliotukuka katika medani,
-Ushiriki katika masula mbalimbali ya kijamii,
-Mwanazuoni aliyefanya vizuri katika masomo na tafiti za kitaaluma,
-Mwakilishi wa Tanzania katika mijadala ya Usalama ya Kimataifa,
-Kachero mwenye uweledi katika kutekeleza Operesheni zenye maslahi kwa nchi yake.
-Kamanda wa Polisi aliyejipambanua katika kutetea haki na kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
CAMILLIUS M. WAMBURA.png
 
Hizo sifa ni kama zile za form two za factors affecting weather.

Hujatwambia ni mpenda haki kwa mifano ipi.

Ila nachokumbuka ni kuwa baada ya uchaguzi Mh Freeman Mbowe na Jacob Meya wa zamani walikamatwa na kufichwa kusikojulikana.

Kamanda huyu inasemekana ndiye aliyemruhusu Mbowe kusafiri kwenda Nairobi then South Afrika then Dubai wakati ule wa zama za giza.
 
Akifanya kazi na wanasiasa wa tanzania hawa walamba asali..uadilifu wake lazima utiliwe shaka.

Mbaya zaidi wateuliwa wengi huwajibika zaidi kwa aliyewateua na wala sio kufuata misingi ya katiba sheria n taratibu za nchi.

Katiba ya warioba iweke mezani..

#MaendeleoHayanaChama
 
Leo Julai 20,2022 Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi ya Polisi kwa kumteua aliyekua Kamishna wa Polisi Camillus Wambura kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP).

IGP Wambura kitaaluma na kiutendaji ni mpelelezi aliyebobea, mwenye weledi katika nyanja ya upelelezi. Alianza kuonekana tangu enzi za Alfred Tibaigana akiwa Kamanda wa Polisi Dar Es Salaam ambapo kila alipoingia katika jukumu alifanikiwa kudhibiti matukio ya uhalifu kwa asilimia kubwa.
Kabla uteuzi huu, IGP Wambura alishika nyadhifa zifuatazo ndani ya Jeshi hilo.

  • Amekuwa Mkuu wa Upelelezi (ZCO) Kanda Maalum ya Dar es Salaam
  • Kamanda Wa Jeshi La Polisi, Mkoa Wa Kipolisi Kinondoni
  • Afisa Mwandamizi Wa Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi.
  • Mkuu Wa Oparesheni Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi
  • Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Wa Dar Es Salaam
  • Mkurugenzi wa Operesheni- Makao makuu DODOMA
  • na Mkurugenzi Wa Mashtaka Na Makosa Ya Jinai (DCI).

Mambo mengine yaliyotajwa katika Utendaji kazi wa IGP WAMBURA ni – UADILIFU, MPENDA HAKI, ANAYECHUKIA RUSHWA na MCHAPA KAZI.

Umaridadi wa IGP WAMBURA umeonekana katika
-Utumishi uliotukuka katika medani,
-Ushiriki katika masula mbalimbali ya kijamii,
-Mwanazuoni aliyefanya vizuri katika masomo na tafiti za kitaaluma,
-Mwakilishi wa Tanzania katika mijadala ya Usalama ya Kimataifa,
-Kachero mwenye uweledi katika kutekeleza Operesheni zenye maslahi kwa nchi yake.
-Kamanda wa Polisi aliyejipambanua katika kutetea haki na kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Nimejawa na furaha kuona mtu makini ndani ya Jeshi la Polisi mwenye uzoefu na weledi anakabidhiwa majukumu makubwa ya kuliongoza Jeshi letu la Polisi. Hakika CAMILIUS WAMBURA ni mtu sahihi mno.

Wengi wetu tunaofuatilia utendaji wa Jeshi la Polisi nchini tulitegemea mabadiliko kufanywa hususani katika nafasi hii muhimu ili kupatikana mtu anayeendana na kasi na dira ya serikali ya awamu ya sita.

Baadhi ya nyadhifa na majukumu ndani ya Jeshi la Polisi yaliyowahi kufanywa na IGP CAMILIUS WAMBURA ni pamoja na;

1. Kamanda wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi - KINONDONI
2. Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi- Makao Makuu
3. Mkurugenzi wa Operesheni- Makao makuu DODOMA
4. Kamanda wa Polisi -Kanda Maalum-DAR ES SALAAM
5. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
6. Na sasa INSPEKTA JENERALI WA POLISI (IGP)

BAADHI YA SIFA ZA KIPEKEE ZA IGP WAMBURA KATIKA UTUMISHI

1. Mpenda haki na muwajibikaji
2. Msomi na mwanataaluma mbobezi ndani ya Jeshi la Polisi
3. Kamanda wa Polisi anayependa kujihusisha na mambo ya kijamii.
4. Mzalendo na mchapakazi katika majukumu mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi
5. Kamanda wa Polisi asiye na makuu na mwenye weledi katika nafasi anazo aminiwa.

UZOEFU KATIKA MAJUKUMU MAKUBWA

-Kamanda wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi - KINONDONI
  • Mkurugenzi wa Operesheni- Makao makuu DODOMA
  • Kamanda wa Polisi -Kanda Maalum-DAR ES SALAAM
  • Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
UMARIDADI NA HISTORIA
  • Utumishi uliotukuka katika medani
  • Uzalendo na uchapakazi katika majukumu mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi
  • Ushiriki katika masula mbalimbali ya kijamii
  • Mwanazuoni aliyefanya vizuri katika masomo na tafiti za kitaaluma
  • Mwakilishi wa Tanzania katika mijadala ya Usalama ya Kimataifa
  • Kachero mwenye uweledi katika kutekeleza Operesheni zenye maslahi kwa nchi yake.
-Kamanda wa Polisi aliyejipambanua katika kutetea haki na kulinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata mwendazake anaitwa "mtakatifu" na kwa sasa eti yupo na watakatifu mbinguni!!!
 
Back
Top Bottom