Huyu ndie Rais wetu asiekuwa na muda wa kupoteza.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu ndie Rais wetu asiekuwa na muda wa kupoteza....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtoboasiri, May 11, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Rais Kikwete ataka mawaziri wajiengue
  Na Sharon Sauwa  10th May 2011
  [​IMG] Ni wanaokiuka maadili, uwajibikaji
  [​IMG] Agusia wizi, uzinzi, ubabe, dhuluma  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa viongozi wakuu wa serikali mjini Dodoma jana. Wengine ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto) na Jaji Mkuu, Othman Chande (kulia).  Rais Jakaya Kikwete amewataka mawaziri na makatibu wakuu ambao watashindwa kuzingatia uwajibikaji wa pamoja wajiondoe wenyewe kwenye nafasi zao.
  Akifungua semina elekezi kwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu jana mjini Dodoma, Rais alisema kupingana hadharani kwa viongozi hao, mbele ya wafanyakazi au hata kwenye vyombo vya habari kunawapata tabu ya kuwajibia maswali.
  "Lazima ieleweke kuwa tukishaamua jambo kwa pamoja Wizarani au katika Baraza la Mawaziri ni uamuzi wetu sote hata kama wewe ulikuwa na mawazo tofauti. Wote tunao wajibu wa kuunga mkono na kuutetea. Kamwe hatutegemewi kuendelea kuupinga baada ya hapo, " alisema na kuongeza:
  "Kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya uongozi na uwajibikaji wa pamoja. Kama unaona vigumu sana kuuafiki ni bora kutoka. Hairuhusiwi kupinga taasisi ambayo wewe umo ndani kama mmoja wa viongozi wake. Ni vyema hili likaeleweka vyema. Msitupe tabu ya kuulizana maswali na kuwasemea."
  Vile vile, amesema kumezuka tabia ya baadhi ya mawaziri kupinga maamuzi ya Baraza la Mawaziri hivyo amewataka wasiokubaliana nayo wajindowe wenyewe.
  Rais Kikwete alielezea kutofurahishwa kwake na malumbano ya viongozi hadharani na aliita jambo hilo kuwa ni fedheha ya hali ya juu.
  “Haifurahishi kuona Waziri na Katibu Mkuu, au Waziri na Naibu Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu au Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu hawaelewani, wanasemana na hata wakipingana hadharani na baya zaidi pale wanapopingana katika vyombo vya habari kuhusu maamuzi au utendaji wa Wizara au Serikali kwa ujumla hayo si maadili mema katika taasisi yoyote,” alisema.
  Alisema uzoefu unaonyesha kuwa jambo hilo hutokea pale kunapokuwa na kuingiliana katika majukumu au kwa kutozingatiwa kwa taratibu na maadili ya uongozi.
  “Lazima ieleweke kuwa tukishaamua jambo kwa pamoja Wizarani au katika Baraza la Mawaziri ni uamuzi wetu sote hata kama wewe ulikuwa na mawazo tofauti. Wote tunao wajibu wa kuunga mkono na kuutetea. Kamwe hatutegemewi kuendelea kuupinga baada ya hapo. Kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya uongozi na uwajibikaji wa pamoja.
  Alisema uwajibikaji wa pamoja unahusu pia shughuli za Serikali Bungeni kwani Miswada ya Serikali ni ya Mawaziri wote mmoja mmoja na kwa umoja wao.
  “Mswada wa Sheria ukiletwa na Waziri mmoja, kila Waziri anao wajibu wa kuunga mkono na kuutetea. Haitarajiwi na ni kinyume cha maadili cha hali juu kwa Waziri kupinga mswada wa Waziri mwenzake…Kwa kweli, tabia hii haivumiliki na anayetenda hayo amejitenga mwenyewe na Serikali,” alisema.
  Katiba semina hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othmani; Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya na viongozi wakuu wa vyombo vya usalama, Rais Kikwete aliwataka mawaziri wasiwe mangimeza na badala yake wawe wanawatembelea wananchi kujua shida zao na kisha kuzitatua. Alisema wanatakiwa kuyajua kwa kina mambo yote yanayohusu Wizara wanazoziongoza la sivyo hawataongoza vizuri na watakuwa wababaishaji.
  “Mawaziri na Makatibu Wakuu lazima mtoke... Hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kujua mambo yahusuyo Wizara zenu na ndiyo njia bora ya kuongoza: kuona wenyewe na kutenda. Itawafanya mjiamini kuelekeza na pia mnaposimama mbele za watu na kusema. Msiwe mangimeza. Tokeni, tembeeni kuona shughuli zenu. Tembeleeni wananchi muwafahamu, wawafahamu, mjue shida zao muwatatulie.
  Aliowataka kujielimisha kuhusu katiba, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi katika sehemu zao za kazi na kwamba uhalali wa maamuzi watakayoyafanya hupimwa na sheria.
  “Ukifanya maamuzi yanayokinzana na sheria utahojiwa wewe binafsi, lakini pia utaibebesha Serikali mzigo wa hasara na fedheha itakayotokana na maamuzi hayo... maamuzi yasiyofuata sheria yanaweza kuwa na madhara kwa wananchi hivyo heshimuni Katiba na fuateni sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yenu,” alisema.


  Alisema Mawaziri wanapaswa kutambua kuwa kuhudhuria vikao vya Bunge ni jambo la lazima kama ilivyo kwa vikao vya Baraza la Mawaziri na si jambo la hiari. Alisema ni lazima Waziri ahudhurie vikao vya Bunge bila ya kukosa labda awe na sababu kubwa inayoelezeka na kukubalika. Alisema ingawa kutembelea jimbo la uchaguzi ni jambo la lazima, lakini siyo sababu ya kuwafanya wakose vikao vya Bunge au Baraza la Mawaziri.

  UWAJIBIKAJI NA KIMAADILI
  Alisema Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu ni viongozi wakubwa sana Wizarani, Serikalini na katika jamii hivyo kiongozi anatakiwa kuwa mfano mwema kwa watu anaowaongoza.
  Alisema watu watatamani kuwa kama yeye au kuishi kama yeye na watatamani kumuiga kwa uchapakazi wake, kwa tabia njema na matendo mema. Alisema Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Mkuu wasinyooshewe kidole kwa uvivu, uzembe, wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, vitendo vya utovu wa uadilifu kama vile wizi, ulevi wa kupindukia, uzinzi, majigambo, ubabe na uonevu na dhuluma. Kuwa hivyo ni kupungukiwa sifa za msingi za uongozi.
  Alisema wananchi wanapenda kuona Serikali yao ina viongozi na watumishi waadilifu, wachapakazi hodari, wanaowasikiliza, wanaojali shida zao na wepesi wa kushughulikia na kutekeleza maamuzi mbalimbali ya Serikali.
  Kuhusu kuisemea serikali, Rais Kikwete alisema hilo ni jambo ambalo kuna udhaifu mkubwa.
  “Sijui kwanini hatuwi wepesi kuyasemea mafanikio mengi tuliyoyapata tukaacha wasiotutakia heri wanaosema hatukufanya kitu wasikike mpaka waonekane wanasema kweli… Mwanazuoni mmoja bingwa wa habari aliwahi kusema kuwa “kufanya kitu bila kuufahamisha umma ni sawa kama kitu hicho hakijafanyika… Mwingine anasema kuwa uongo ukisemwa mara nyingi hugeuka kuwa ukweli,” alisema.


  Alisema serikali imefanya mengi lakini wananchi hawakuelezwa ipasavyo na kwamba viongozi wameacha upotoshaji kufanywa bila ya kusahihishwa au kuchelewa sana kusahihishwa.
  Aliwataka viongozi na watendaji wakuu wa Serikali, kuwa mfano kwa wafanyakazi wanaowaongoza kwa kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.
  Aliwataka kuhakikisha bajeti hazikiukwi, fedha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sheria na kanuni za fedha zinaheshimiwa.


  “Niliagiza Kamati za Fedha ziundwe katika kila Wizara na Idara za Serikali zinayojitegemea. Je, zimeundwa? Je, zinafanya kazi? Hakikisheni zipo hai na zinatimiza wajibu wake. Zitasaidia sana kwa upande wa kuongeza mapato na kudhibiti matumizi katika Wizara,” alisema.  CHANZO: NIPASHE

  Kakiri mwenyewe kuwa:

  • Hawezi kuwadhibiti aliowateua
  • Aliowateua hawajui shida za watu na hawafanyi kazi kama timu (kupingana hadharani kwa mambo waliyoamua pamoja)
  • maagizo yake hayazingatiwi
  • Na mengine mengi.
  Hatujui tunakokwenda sasa tutafikaje? Alisema bwana mmoja (ambae sasa hivi sikumbuki jina lake): If you aim at nothing you are sure to hit it!
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Akili zake ovyo
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  kubwa zaidi alisisitiza yy ndo mwenye uamuzi wa nani ashike wapi.nilimshangaa akisema ww waziri unakasirika nn kuwa katibu mkuu wako kaenda mahali kufanya kitu flani.uwaziri nimekupa mie,na ukatibu mkuu nimempa mie!na kuna siku tu utaona kwenye media 'rais amafanya mabadiliko'...very unproffessional advise!wakati huo huo anasisitiza kuwasiliana watu wajue wenzao wanafanya nn!
   
Loading...