Huyu naye mapenzi yanamtatiza!

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,553
11,316
Kuna kaka mmoja tuko wote ofisi moja ila mimi niko field,yeye ni mfanyakazi.Kwa mara ya kwanza nilipomwona nilimpenda ila siku zilivyozidi kwenda mapenzi juu yake yanapungua.Tatizo ni kwamba nimegundua kwamba huyu jamaa ni mbahili halafu anawivu kupindukia.Wenzie huenda lunch lakini yeye huagiza aletewe hapohapo ofisini halafu chakula chenyewe ni wali mbogamboga chakula ambacho ni cha bei ya chini kabisa tofauti na wenzie,mfano siku moja alinikuta nakoroga chai akaniuliza eti kwa nini natumia maziwa mengi wakati hanunui yeye.

Kingine kinachonikera ni kwamba huwa ananifuatilia sana nyendo zangu,mwanaume yeyote akinisemesha lazima aniulize tulikuwa tunaongea nini hata kama ni issue za kiofisi anataka kujua,kwa kweli ananiudhi kupita maelezo ila namheshimu kwa vile ni mtu mzima.Kichekesho zaidi kafanya juu chini hadi akapata namba yangu ya simu na kwa sasa ameanza kunitumia sms za mapenzi.

Kwa kweli mapenzi juu yake yameisha kwani naona hata nikiwa nae atanitesa kwani ikifika lunch time anajinunulia yeye msosi anakula mbele yangu bila hata karibu ya uongo tena haongei akishamaliza ndo anaanza kunisemesha tena sio kuuliza vipi mwenzangu mbona huendi lunch?Kazi yake ni kuniuliza kuhusu familia yangu eti tuko wangapi na je wazazi wanafanyakazi au la?Sa nyingine huniuliza kama nimejenga au nimepanga,jamani huyu ni mwanaume wa aina gani jamani nisaidieni.Mwenzenu niko njia panda manake nahisi huku tuendako kuna dalili za kugombana nae kama ataendelea kunifuatilia coz i already regard him as a careless and selfish one.
 
Hapa utatuwacha njiapanda,tufafanulie kwanza, 1.Ulimpenda lakini hamjaanza uhusiano? 2.mko kwenye uhusiano nae unataka kumpiga chini? 3.Mlikua kwenye uhusiano na hakua na namba ya simu yako?
 
huyo yaonekana kashamegwa ila kwasasa hali ni tete so kaona bure amwage mtama hapa jf.Kama vipi mwambie ajirekebishe au mpige chini
 
Ma-loves ni hiari ya mtu,kama ulivyompenda kwa hiari na ndivyo utakapommwaga kwa hiari yako, je hujachukua chake? tuanzie hapo.
 
Usipoteze muda wako dada! Huyu jamaa hakufai kabisa. Sasa hivi wakati wa kujenga mapenzi yenu ndiyo kipindi kizuri cha kuspend more time together ikiwa ni pamoja na kwenda lunch, music n.k. Kama anaweza kununua chakula chake bila kukufikiria wewe imagine kama mtakapokuja kuoana si ndiyo mambo yatakuwa mabaya sana. Mtolee uvivu na umwambie ukweli kwamba sasa penzi basi.
 
...yeye huagiza aletewe hapohapo ofisini halafu chakula chenyewe ni wali mbogamboga chakula ambacho ni cha bei ya chini kabisa tofauti na wenzie,mfano siku moja alinikuta nakoroga chai akaniuliza eti kwa nini natumia maziwa mengi wakati hanunui yeye.

...mambo ya Diet hayo, au huenda jamaa ni Vegetarian, kwanini humuulizi kuliko hivyo unavyo 'ass-u-me' bajeti ya mwenzio?

..huwa ananifuatilia sana nyendo zangu,mwanaume yeyote akinisemesha lazima aniulize tulikuwa tunaongea nini hata kama ni issue za kiofisi anataka kujua,kwa kweli ananiudhi kupita maelezo ila namheshimu kwa vile ni mtu mzima.

...kama nawe unavyomshangaa na kuudhika, naye anakushangaa hivyo hivyo, uzuri yeye anakuambia, nawe jitahidi umwambie kuwa anakuudhi!

...Kichekesho zaidi kafanya juu chini hadi akapata namba yangu ya simu na kwa sasa ameanza kunitumia sms za mapenzi.

:(...it is not funny!

Kwa kweli mapenzi juu yake yameisha kwani naona hata nikiwa nae atanitesa kwani ikifika lunch time anajinunulia yeye msosi anakula mbele yangu bila hata karibu ya uongo tena haongei akishamaliza ndo anaanza kunisemesha tena sio kuuliza vipi mwenzangu mbona huendi lunch?


...mambo ya 'table manners hayo' kula bila kuongea, ...hivi kuna ubaya gani wewe kumwambia muende Lunch nje ya ofisi? halafu atajuaje kama nawe unataka kula kama kila siku hutoki unamkodolea macho akila?


..Kazi yake ni kuniuliza kuhusu familia yangu eti tuko wangapi na je wazazi wanafanyakazi au la?Sa nyingine huniuliza kama nimejenga au nimepanga,jamani huyu ni mwanaume wa aina gani jamani nisaidieni.

...mbona ni maswali ya kawaida tu hayo?

...Mwenzenu niko njia panda manake nahisi huku tuendako kuna dalili za kugombana nae kama ataendelea kunifuatilia coz i already regard him as a careless and selfish one.

...Njia panda unajiweka mwenyewe, kama huna mahusiano naye ya nini kujichanganya 'T-Junction?', ...kama ni careless na selfish asingekuuliza maswali kuhusu familia yako, au kama umejenga/unapanga. The only option ya kujinasua ni face to face showdown na yeye na kumwambia haya yanayokuudhi kama ulivyoyaleta hapa jamvini.

...hizi zako ni dalili za kawaida mapenzi yakiisha.
 
Ndugu;
Sijakuelewa kabisa hebu fafanua zaidi. Kishakujua au bado? na je wewe ndio ulianza kumpenda au yeye?
 
Jamani mimi siyo mhusika wa huu mkasa bali nilivutiwa na malalamiko ya huyu Dada ndiyo maana nikayabandka humu jamvini ili tuweze kufumbuana macho kwa mambo yanayojitokeza kwenye jamii zetu hususani kuhusu mapenzi..

Na kuhusu wahusika kuwa na uhusiano wa kimapenzi, bado hawajawa wapenzi kwani mwanzoni kabisa huyu dada ametanabaisha kuwa alimpenda huyo jamaa siku ya kwanza pindi alipomuona tu, ila kadri alivyozidi kumwelewa ndiyo akagundua kuwa hawezi kumkubalia kuwa mpenziwe kutokana na tabia alizoziona kwa huyo jamaa na kama alivyoziorodhesha..
 
...mambo ya Diet hayo, au huenda jamaa ni Vegetarian, kwanini humuulizi kuliko hivyo unavyo 'ass-u-me' bajeti ya mwenzio?...kama nawe unavyomshangaa na kuudhika, naye anakushangaa hivyo hivyo, uzuri yeye anakuambia, nawe jitahidi umwambie kuwa anakuudhi!:(...it is not funny!
...mambo ya 'table manners hayo' kula bila kuongea, ...hivi kuna ubaya gani wewe kumwambia muende Lunch nje ya ofisi? halafu atajuaje kama nawe unataka kula kama kila siku hutoki unamkodolea macho akila?
...mbona ni maswali ya kawaida tu hayo?...Njia panda unajiweka mwenyewe, kama huna mahusiano naye ya nini kujichanganya 'T-Junction?', ...kama ni careless na selfish asingekuuliza maswali kuhusu familia yako, au kama umejenga/unapanga. The only option ya kujinasua ni face to face showdown na yeye na kumwambia haya yanayokuudhi kama ulivyoyaleta hapa jamvini.

...hizi zako ni dalili za kawaida mapenzi yakiisha.

Well put mchongoma,i like your analysis of the issue,table manners? ha ha ha
 
Jamani mimi siyo mhusika wa huu mkasa bali nilivutiwa na malalamiko ya huyu Dada ndiyo maana nikayabandka humu jamvini ili tuweze kufumbuana macho kwa mambo yanayojitokeza kwenye jamii zetu hususani kuhusu mapenzi..

Na kuhusu wahusika kuwa na uhusiano wa kimapenzi, bado hawajawa wapenzi kwani mwanzoni kabisa huyu dada ametanabaisha kuwa alimpenda huyo jamaa siku ya kwanza pindi alipomuona tu, ila kadri alivyozidi kumwelewa ndiyo akagundua kuwa hawezi kumkubalia kuwa mpenziwe kutokana na tabia alizoziona kwa huyo jamaa na kama alivyoziorodhesha..

Usome tena ujumbe ulioweka hapa ukumbini. Kwa jinsi ulivyoandika unaashiria kwamba wewe ndiye mhusika.
 
Wewe kama siyo mwenye hii story utawezaje kujibu maswali mengine ya ndani na pili jinsi ulivyo andika hakuna sehemu unayoonyesha kwamba wewe sio muhusika .
Ila kwa sisi tuliopata kuona picha kama "Analyse this" ya De Niro tunaweza kusema kama Dr .Sobel kuwa "what I think your freind is you".Wewe unaleta matatizo ya rafiki yako lakini inaonekana kam huyo rafiki yako ni wewe wenyewe kwa kuwa umeshindwa hata kuandika kwa nafsi ya tatu.

Kuhusu muhusika weka criteria za mtu unayemtaka kisha angalia kama anazo basi utakuwa na jibu kama unampenda au vipi.Unadai mwanzoni ulimpenda nadhani unamaanisha ulipenda wasifu wake wa nje ila sasa unaupata wasifu wake wa ndani unakupa shaka.Basi wawenga hawakukosea kusema usipende ugenini kwa hiyo taratibuni utajua mwenyewe kama unampenda au vp ruhusu muda upite.Just listen to yourself.
Halafu jaribu kuwa na positive mind anacho kula ni utaratibu wake ambao umeonekana kuwa mzuri tu ila ww huupendi.
 
ogopa mtu selfish....... Ingawa Mbu kamtetea kimtindo lakini mmmh hafai huyo
 
Last edited by a moderator:
kwi kwi kwi ukiomba laki ya saluni si atakufa huyo
kimbia murder case dear
 
Back
Top Bottom