Huyu Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara anafanya haya kwa makusudi ama hajui maana ziara ya Waziri (Serikali) mikoani/majimboni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Nimeshuhudia ziara yake akiwa huko kata ya Sirari na kata zingine ndani ya jimbo la Tarime Vijijini, inatia huruma kwa Waziri kufanya haya.

Hotuba ina dakika (60) yaani saa moja.
-Anatumia dakika (10) kuelezea kwanini ametoka CHADEMA kwenda CCM.
- Anatumia dakika (20) kumtukana na kumkashifu Mbunge wa Tarime Vijijini mhe. John Heche pamoja na madiwani wa CHADEMA.
-Anatumia dakika (10) kukiponda chama cha CHADEMA na viongozi wake Kitaifa
- Anatumia dakika (15) kumsifia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mhe. John Pombe Magufuli
- Anatumia dakika (5) kuwaomba wananchi wachangie ujenzi wa shule (kwa harambee) na mwisho anachanga shilingi laki tano.

Hii ni ziara ya kisiasa wala siyo ziara ya serikali. Serikali inatumia kodi za Wananchi ndivyo sivyo, yaani Waziri anazunguka majimboni kutukana wapinzani na kukejeli vyama vya upinzani.
This is bad!!!
Nchi hii inaudhi isivyo kawaida!!
 
Back
Top Bottom