Huyu mzungu anataka nini?

Wewe mwenyewe unaonekana ndo unaendeleza conversation. Yani inaonekana yeye ndo anakujibu maswali unayomuuliza, sasa huelewi nini afu unatuuliza sisi '' huyu mzungu anataka nini ". But ukisoma hizo emails sisi ndo inabidi tukuulize wewe " unataka nini kwa huyo mzungu? " .
 
Mimi Kuna moja alijidai ni mrusi amekosa bwana huko anataka kuja akapanda ndege eti alivyofika nauli ikamwishia akaomba nimtumie 900$ nikamwambia ndege gani anatarajia kupanda akasema Ethiopian nikamwambia hapa agent yupo ngoja nikalipie utumiwe tiketi ,kimyaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie ninae anaedai ni mjerumani anaishi marekani nachati nae Kila siku uku akihaidi mambo lukuki nikakwambia naitaji nikuone muda huo huo akapiga WhatsApp call tukaonana na Kila nikiwa na shaka nae ananipigia ata kwa call WhatsApp au kawaida nami namchungulia kwa mbaliiii! Akitamka pesa tuuu mie nduki

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kakubali kuonesha sura na ni mzungu basi huyo sio tapel
 
We contact nae tu sema ukimuona anaingia kwenye anga sijui nimepungukiwa na kiasi fulani niongezee ndio ushtuke,Lakini sumtime mbona wazungu kibao wanazubaa mitandaoni wanatafuta mahusiano.
Hiyo ndio biography yake mkuu
Screenshot_20200308-222657.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaanzaga taratibu mwisho wa siku anaingiza habari za pesa.
Endelea kuwasiliana nae lakini akikuletea habari za pesa toka nduki.
 
Zungumzeni yoteee mnayoyajua sijua ekari za ardhi ,kuku,nyumba ,watoto ila akileta habari za hela kimbia usigeuke nyuma utakua jiwe la chumvi.
 
Nnavyo wajua wazungu si wepesi kutoa maelezo yake ya ndani saaana mapema hivo but tusimuhukumu wewe chat nae akiongea kuhusu hela kimbia pia wazungu huwa hawajib mail ontime ukiona yupo ontime saaaan huyo tapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna huyo alinichek ivo ivo akaniambia ni mjeda wa US yupo Afghanistan war on terrorism,,,baada ya kuchat sana na kuniambia kila kitu kuhusu yeye...mwishon akaniambia kipindi wanafanya patrol ya makambi ya ISIS wamekutana na sanduku lina mali,,lina SAA za gold na diamonds roughly kama $10M...sasa akaniambia huko kambini amepanga yeyr na OC wake wazigawane ila wakionwa nazo watachukuliwa kama traitors... Kwahiyo akawa anafanya mchakato wa kunitumia hizo mali ...hapo ndo kupigwa kukaingia nkashtuka.
Maelezo kma hayo Mimi nishakutana nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom