Huyu mzazi mwenzangu nimuache aende zake au niendeleee kumbembeleza arudi nyumbani?

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
6,495
12,594
Habari wakuu?

Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 32,nilikuwa naishi na mzazi mwenzangu ambae tulibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka miwili sasa.mzazi mwenzangu ni mtu kutoka kabila la wahehe.

Mwaka jana mwezi wa saba nilipeleka barua ya posa nyumbani kwao na wakanipangia mahari, mipango yangu ilikuwa mwaka jana december ningeipeleka hiyo mahari huko kwao but mambo yakaingiliana hapo katikati yaliyopelekea mpaka leo bado sijaipeleka hiyo mahari.Huyu mwanamke kiukweli naweza sema ananipenda sana tu coz sijawahi kuona dosari yoyote kwake.so tatizo limeanza mwezi uliopita, ambapo alianza tabia ya kuwa anashika simu yangu hovyo akakutana na messages kutoka kwa wanawake wengine.

Well, ni kweli nilikuwa nacheat kipindi flani hivi, nilikiri kosa na kumuomba msamaha,alichosema ni kwamba amenisamehe but anahitaji nafasi kwanza ya kuwa mwenyewe coz anaona hana amani kuendelea kuishi na mimi kwa hayo yaliyojitokeza na mengine kadhaa yaliwahi kutokea siku za nyuma, nikamsihi asiondoke but ikashindikana, akaondoka na mtoto wakaenda kupanga mtaa jirani na kwangu..kiukweli sio kwamba simpendi huyu mwanamke,ila tu ni tamaa zetu wanaume ndizo zilizonifanya nikaanza kutoka nje.najua nimemuumiza sana moyo wake kwani alikuwa ni mtu mwenye matarajio makubwa sana na mimi.

Ombi langu kwenu wakuu ni kwamba,nawezaje kumrudisha huyu mwanamke ili maisha yetu yaendelee kama mwanzo?au kwa scenerio hii ya yeye kuondoka nyumbani kwa hasira na kwenda kupanga kwingine nimpotezee tu aendelee na maisha yake?na vipi nikiamua kumpotezea ile barua ya posa niliyopeleka kwao haitokuwa na madhara yoyote?

karibuni kwa mawazo yenu wakuu.
 
Muite mwambie ile mipango yangu imekaa sawa sasa nataka kupeleka mahari kwa wazee umsikie atasemaje. Na utumie nafasi hiyo kumuomba msamaha tena na ujutie kosa lako. Akikubali peleka mahari na umaanishe kutorudia tena kuchepuka na akikukataza kupeleka mahari jua imekula kwako hiyo Anza kumsahau maishani mwako

Sent from my Redmi Note 6 Pro using JamiiForums mobile app
 
Mimi naona ni vema umpe muda kama alivyokwambia usiache kumpelekea matunzo ya mtoto na kwenda kumjulia hali. Muombe sana Mungu akuongoze katika sala ya toba, na usirudie tena kosa. Naimani atakaa chini na kuona kweli ulifanya kosa hukudhamiria akikusamehe tu kamilisha ibada ya ndoa.
 
1. Kama mwanamke hapendi kuishi na wewe usimlazimishe. Kitendo cha yeye kwenda kupanga kwingine siyo cha kukichukulia poa. Lazima atakuwa kachezea mipini Kama njia ya kujifariji, kulipiza au kujihakikishia bado ni needed. Kama atakurudia cheki afya au uwezekano wa mimba ya mtu mwingine.

2. Mtoto wa kiume kulelewa na single mother siyo sawa hata kidogo, ndio sababu inayochangia uwepo wa wanaume mchele mchele. Pambana juu chini hata kama mtaachana lakini wewe ubaki na mwanao kama kweli ni damu yako.

3. Kama mwanamke hapendi kuishi na wewe unawazia mahari ya kazi gani?
 
Ni suala la muda tu huyo lazima akutafute. Endelea kuhudumia familia yako kama kawaida
Kipindi hiki inabidi utulie hata ile michepuko, inabidi uipige chini
 
Muite mukae muzungumze mana hakuna kosa ambalo alisameheki ndugu pia pindi utakapokutana nae jitaidi ujishushe sana alafu mchomekee inshu ya kupeleka mahali najua lazima atalegea but kitu kingine uyo lazima atakuelewa kwa nn? Coz ulishapeleka barua ya posa kwao na kwa mtoto wa kike barua ikishapelekwa kwao kinachofata mahali sasa shemeji hawezi kuona aibu iyoo itokee kamwe kitendo cha kupeleka barua alafu wazazi waone kimya kwa watoto wa kike ni udhaifu na fedhea kubwa sana so pambana mpka kieleweke
 
Muite mwambie ile mipango yangu imekaa sawa sasa nataka kupeleka mahari kwa wazee umsikie atasemaje. Na utumie nafasi hiyo kumuomba msamaha tena na ujutie kosa lako. Akikubali peleka mahari na umaanishe kutorudia tena kuchepuka na akikukataza kupeleka mahari jua imekula kwako hiyo Anza kumsahau maishani mwako

Sent from my Redmi Note 6 Pro using JamiiForums mobile app
Mada imeisha hapa.
Nakazia tu hapa.
Kwa kuongezea tu wakati huo unaishi naye uliwahi kumchunguza na kujua udhaifu wake ni nini?Kila mwanamke ana udhaifu wake fulani au kuna kitu fulani ambacho ukikifanya hicho hata awe amekasirika vipi utamchota na kumrudisha tena.
 
Muite mwambie ile mipango yangu imekaa sawa sasa nataka kupeleka mahari kwa wazee umsikie atasemaje. Na utumie nafasi hiyo kumuomba msamaha tena na ujutie kosa lako. Akikubali peleka mahari na umaanishe kutorudia tena kuchepuka na akikukataza kupeleka mahari jua imekula kwako hiyo Anza kumsahau maishani mwako

Sent from my Redmi Note 6 Pro using JamiiForums mobile app
sawa mkuu,,asante kwa ushauri
 
Mimi naona ni vema umpe muda kama alivyokwambia usiache kumpelekea matunzo ya mtoto na kwenda kumjulia hali. Muombe sana Mungu akuongoze katika sala ya toba, na usirudie tena kosa. Naimani atakaa chini na kuona kweli ulifanya kosa hukudhamiria akikusamehe tu kamilisha ibada ya ndoa.
asante kwa ushauri mkuu
 
Muite mukae muzungumze mana hakuna kosa ambalo alisameheki ndugu pia pindi utakapokutana nae jitaidi ujishushe sana alafu mchomekee inshu ya kupeleka mahali najua lazima atalegea but kitu kingine uyo lazima atakuelewa kwa nn? Coz ulishapeleka barua ya posa kwao na kwa mtoto wa kike barua ikishapelekwa kwao kinachofata mahali sasa shemeji hawezi kuona aibu iyoo itokee kamwe kitendo cha kupeleka barua alafu wazazi waone kimya kwa watoto wa kike ni udhaifu na fedhea kubwa sana so pambana mpka kieleweke
asante kwa ushauri mkuu
 
Na kuanzia Sasa ufunge zipu yako .

Kuna wanawake wengine hawana makando kando Ni wastaarabu sana

Tulia weka mipango utunze familia yako

Acha kutembeza rungu kitaaa waachie wachimbachumvi
sawa mkuu
 
Umewakosea sana wahehe hao binti hawanaga shida na mtu na hasira zao vinawatuma vibaya.

Ebu acha tuone mambo itakavyo kua usiache kuleta mrejesho tujifunze
kwa hiyo ushauri wako ni nini boss wangu?
 
Mzee yamenikuta just happened Kama yako na umri Kama wako

Sasa mie mke wangu mwezi June alienda kusalimia kwao Arusha,alikaa mwez alipo Rudi alikuja was tofaut Sasa na Mimi nikatia chumvi kwenye kidonda akakuta Rasta ya like kitandan .akamind so nikiwa mishe akauza sofa,tv,dek akasepa na mtoto wangu wa kiume

Mbaya Zaid badala ya kwenda kwao akaenda geita huko sijui kufanya Kaz ya bar au hotel au kujiuza akapanga na chumba mtoto akamtafutia mfanyakaz WAKAT huo mie ananiongopea kuwa yupo Moshi kwa ndugu

Nikambembeleza arud akakubali nikatuma nauli,hakuja..

Mala ya pili NIKAMMBELEZA akakubali nikasema Kama waja Basi nakutumia tiket ndio Hapo nikajua yupo geita mamaae

Nikatuma tiket akaja kabadilika sio yet akiwa njian anatuma sms za dharau mie nilijishusha tu afike nimchukue MWANANGU

Alipo fika kesho yake nikampeleka mtoto Kwan mama yangu mzazi NIKABAKI NIPO NA HUYU MAMA

MJUZ NIKAPIGA MISHE FLAN SASA HELA WALIHITAJI WATUME KUTOKA KWENYE CRDB BANK WATUME MPESA MIE NA HALOPESA NA HUYU MAMA ANA MPESA BASI NIKATAJA NAMBA YAKE

ikaiingia pesa Kama laki na nusu HV kwenye namba yake

Siku hiyo nilikuwa off na magu alikuja mbeya Sasa nilitoka kidogo KURUD nakuta mtu kapanga nguo zake kafunga kwenye mabag nikajifanya sijui nikaona analazimisha niende kumchek magu NIKAKUBALI NIKAOGA NIKATOKA

ILA SIKWENDA NIKAKAA BALABALAN MUDA UAKENDA AKAJA CHUKUA BAJAJI ILE ANABEBA MABEG NAMI NAIBUKA

ILI NIMSHUSHE HASIRA NDIO ZILIPANDA ***** nilipiga yule mwanamke nilitaka kuuuwa uso ulivimba aliiomba msamaha,akalala kesho yake nikamkatia tiket karud geita

NIMEBAKI SINGLE FATHER NA MTOTO WANGU WA KIUME

KAINGIA GEITA JANA

ILA NILIMPENDAA SANA SO NIMEUMIA SANAA HAWA WATU WA NDURUMA NA WEUPE WAO WANA DHARAU BALAAAAAA
 
Back
Top Bottom