Huyu mwandishi kijana ni bonge la kanjanja na kibaraka wa wakubwa na anatumika kisiasa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,440
2,000
Sababu:
1.Katika sakata la kulipuliwa kwa ofisi za IMMMA Advocates, Lissu anasimama kama mwanachama na kiongozi wa TLS na si mwanachama wa CHADEMA au mtu binafsi na kwa maana hiyo hawasilishi wala kusimamia maoni ya CHADEMA au ya Kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni au maoni yake binafsi

2.Inatambulika Tundu Lissu kama kiongozi wa TLS anawakikisha mawazo na msimamo wa TLS na wala si msimamo au mawazo ya CHADEMA kuhusu IMMM Advocates aliyoyawakikisha Bungeni mwaka 2012(kinachofanywa na mpambe huyu na wengineo ni upotoshaji wa makusudi kwa malengo ya kisiasa).

3.Mawakili wa IMMMA Advocates ni wanachama halali wa TLS hivyo baraza la uongozi wa TLS linawajibika kuwasemea katika hili kama wanachama wake vinginevyo baraza lisingetenda haki kama ambayo linashutumiwa kukaa kimya walipouwawa baadhi ya mawakili.

4.Ni uendawazimu na chuki za wazi kabisa kuwalaumu viongozi wa TLS ya sasa kwa makosa yaliyofanywa na uongozi wa TLS uliyopita kwa kutowasemea mawakili walioa pata na majanga wakati huo(kina Mvungi na wengineo)

5.IMMA Advocates kuwatetea waliochota mabilioni ya EPA hakuhalalishi ofisi zao kulipuliwa na homu hivyo ni uendawazimu wa hali ya juu kutegemea TLS ikae kimya pale mawakili ambao ni wanachama wao wanapopatwa na majanga kama haya.

6.TLS haikutamka moja kwa moja kuwa ni Polisi ndio waliovamia na kulipua jengo la ofisi za IMMMA Advocates bali walisema kuwa wamepwa taarifa/wanazo taarifa kuwa watu walioonekana kuvalia nguo za Jeshi la Polisi ndio waliohusika kulipua ofisi hizo(katika matamshi yao sijawasiki wakitamka kuthibitisha kuwa nguo hizo kweli zilikuwa ni sare za Jeshi la Polisi).

7.Ni mara ngapi watu wanakamatwa kwa kuvaa nguo za Jeshi la Polisi au zinazofanana na Jeshi la Polisi ili hali wao si Polisi halali wa Jeshi la Polisi Tanzania?

8.Katika mazingira haya,kulitaka Jeshi la Polisi kuchunguza tukio hili kuna kasoro gani ili hali hakuna mahali baraza la uongozi wa TLS limewatuhumu Polisi moja kwa moja kuhusika na tukio hili?

9.Kama kweli TLS ilitamka wazi kuwa waliovamia ofisi za mawakili wa IMMMA na kuzilipua walikuwa ni Polisi,mbona hatujaona Jeshi la Polisi likiwakamata viongozi hao wa TLS kwa kuchafua Jeshi hilo?

10.Ni kwanini kijana huyu asikamatwe kwa kupotosha tamko la TLS na zaidi kwa kumchafua IGP na Jeshi analoliongoza?

11.IMMMA Advocates kutetea wezi wa EPA si ndio kazi yao kama mawakili?

12.CHADEMA kupitia Tundu Lissu kuhoji IMMMA Advocates kuwatetea wezi wa EPA Bungeni walifanya vile kwasababu IMMMA Advocates walikuwa ni mawakili au walikuwa na sababu zingine?

13.TLS wangekaa kimya baada ya tukio hili la ofisi za IMMMA Advocates kulipuliwa ili hali walishatangaza rasimi kuwa shambulio dhidi ya wakili mmoja ni shambulio kwa mawakili wote,mngeacha kulaumu uongozi wa TLS kwa kushindwa hata kukemea na kulaani tukio hili?

Acheni unafiki na kujipendekeza huku mkitumika kisiasa!!
 

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,532
2,000
Ni mnafiki sana yule bwana!
Wakati wa kesi yake ya utapeli na utambulisho batili, huyo mwandishi alikuwa anazurula mkoa kwa mkoa kuomba huruma ya watu. Wakakasikia, wakakaonea huruma, kakawa huru. Sasa analipa fadhila za wahisani kutoka madhila ya kesi. Sishangai anavyojitumikisha ki-wendawazimu! They owe him something big!
 

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,532
2,000
huyo......anaacha kulalamiki wezi wa epa na wahujumu uchumi ccm kwa kuingia mikataba mibovu na kuipitisha bungeni kwa maslahi yao binafsi yeye anahangaika na watete wanyonge?.....
Ni aibu kubwa sana kuwa na watu wenye mawazo kama ya JM. Halafu kila agusacho hugeuka na kuwa rabsha kwake. Ajichunguze. Kuna kitu hakipo sawa kwenye approaches zake.
 

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,532
2,000
Watanzania kama tumepewa nafasi ya kuandika vitu bila kutoa majina yetu halafu bado tunaogopa kutaja majina ya watu tunaowaandika, tunaishia "muandishi kijana" na "JM", naweza kuelewa sababu mojawapo inayofanya tuwe masikini ni woga wa kijinga.

Sent from my Kimulimuli
Unaweza ukawa sawa kimtazamo kwa kiasi fulani. Nasisitiza kwa kiasi fulani. Ila kwa upande wangu, kila nikiliandika jina kamili la mlengwa hasa uzi ukiwa unafanana na huu hilo jina hufutwa na kubaki *****!
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,124
2,000
Jerry

Nimesikia sikia sikia siku hizi amekamatana sana na yule Mkuu wa Mkoa HARAMU..

Ameamua kuuza utu na heshima japo kidogo aliyokuwa amebaki nayo kwa kutetea upuuzi na wapuuzi..

Hana muda mrefu huyu, atafutika kabisa.
 

Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,921
2,000
Unaweza ukawa sawa kimtazamo kwa kiasi fulani. Nasisitiza kwa kiasi fulani. Ila kwa upande wangu, kila nikiliandika jina kamili la mlengwa hasa uzi ukiwa unafanana na huu hilo jina hufutwa na kubaki *****!
Jerry Muro.

Mbona mimi nimeliandika?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom