Huyu mwanaume simwelewi kabisa

Anna pita

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
227
425
Jamani naombeni ushauri wenu ndugu zangu nilikua na rafiki wa kiume close friend yaani tulikua marafiki hasa kiasi kwamba haiwezi pita Masaa 2 hatuwasiliani usiku tunaongea mpaka SAA 5 usiku.

Kuna siku alienda kazini akachelewa kutoka akanipigia best ndio nafika alafu gesi imeisha kwakua ni rafiki sikuona ajabu nikamwambia njoo ule huku akaja kula Sijui kilitokea nini tukajikuta tupo katika mahusiano ya kimapenzi kweli mi nilikua nampenda sana before nadhani hata yeye.

Sasa kilichofanya niombe ushauri ni tabia ya jamaa kifupi tumepanga kufikia December tuwe tumesha tambulishana kwa wazazi lengo tuje tuishi pamoja ambacho simuelewi jamaa anaweza piga simu pika nakuja kula kweli najipinda napika anakula anaondoka au anaweza pata mgeni akaniambia piga ninamgeni tunakuja kula nawapikia jamaa hanunui hata mboga wala tu kujiongeza angalau alete hata nyanya tu hapana

Yeye ana kazi nzuri analipwa karibia 1million per month mimi mbangaizaji tu lakini hata huruma hana nashindwa nimuelewe juzi aliniambia njoo uninunulie lunch nikamwambia sina hela basi.

Jana kaja nimekuja kula ikabidi niandae chakula akala akaondoka jamani nashindwa kumuelewa ni mtu wa aina gani mi sio muongeaji sana nashindwa kumuambia nataka niachane nae je naanzaje? maana ukweli nampenda Jamaa ana 36 mimi nina 30.
Naombeni ushauri wenu
 
Usipoteze bahati kwa vitu vidogo kama ivyo.Mpe mda na pia inabidi uwe muwazi kwake kwamba inabidi kufanyike cost sharing.Kama Marioo utajua ukimwambia ukweli na atajiengua mwenyewe.Lakini swala la kumpiga chini wakati hujamfungukia utakuwa umepoteza wewe.Kama unampenda mwambie ukweli hupendi iyo tabia yake ya kula na kutochangia chochote.Kwani kwako Msikitini
 
Kama shida ni msosi tu na unataka kujua kama jamaa ni bahiri au huchukulia kawaida tu hali kama hiyo maana mwenye mamlaka na maamuzi ya hapo kwako ni wewe pia jamaa huenda kajiridhisha kuwa huna shida ndogo ndogo, mtembelee na wewe, nenda kwake akikuomba hela ya mboga achana naye.

_ where ever you are remember me_
 
Endelea kumlea inaonekana una roho nzuri sana weye. Hizo ni dalili za one side love. Mshikaji hakupendi ila anakutumia tuu kurahisisha ugumu wa maisha na ukizingatia hali kiuchumi siyo salama sana
Huitaji ushauri mwingine zaidi ya huu... Hawa wanaitwa mario... Kila kona kambi ila zote kupunguza ukali wa maisha kusave za kumpa baby wake.... Upooooooooooooooooooooo
 
Jaman naombeni ushauri wenu ndugu zangu
Nilikua na rafiki wa kiume close friend...yaan tulikua marafiki hasa kiasi kwamba haiwezi pita Masaa 2 hatuwasiliana. Usiku tunaongea mpaka SAA 5 usiku...
Kuna siku alienda kazini akachelewa kutoka akanipigia best ndio nafika alafu ges imeisha kwakua ni rafiki sikuona ajabu nikamwambia njoo ule huku akaja kula Sijui kilitokea nn tukajikuta tupo ktk mahusiano ya kimapenz
Kwel mi nilikua nampenda sana before nadhan hata yeye.

Sasa kilichofanya niombe ushauri ni tabia ya jamaa kifupi tumepanga kufikia December tuwe tumesha tambulishana kwa wazazi lengo tuje tuishi pamoja
Ambacho simuelew jamaa anaweza piga cm pika nakuja kula kweli najipinda napika anakula anaondoka au anaweza pata mgen akaniambia piga ninamgen tunakuja kula nawapikia jamaa hanunui hata mboga wala tu kujiongeza angalau alete hata nyanya tu hapana...yeye ana kazi nzuri analipwa karibia 1million per month..Mimi mbangaizaji tu lkn hata huruma hana nashindwa nimueleweje
Juz aliniambia njoo uninunulie lunch nikamwambia sina hela basi
Jana kaja nimekuja kula ikabidi niandae Chakula akala akaondoka .jmn nashindwa kumuelewa ni mtu wa aina gani mi sio muongeaji sana nashindwa kumuambia...nataka niachane nae je naanzaje??? Maana ukwel nampenda.....
Jamaa ana 36 Mimi Nina 30..
Naomben ushauri wenu
Soma nyakat mapema, yupo kimaslah zaid, yan ukikosea ukapata na mimba hapo ushatelekezwa, chakula hawez kuchangia au kukujal kama MKE mtarajiwa unadhani kuna ndoa hapo ,kua makin wanaume weng c wastarabu, u eat u ran ndio walioweng

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa umri huo sikushauri kuachana naye... Jikaze tu uipate ndoa, at least kama hujatongozwa na wanaume angalau watatu zaidi ya three months, sikushauri kabisa kumuacha... Ukiingia ndani ya ndoa atakoma maana itabidi ayabebe hayo majukumu. Vumilia tu bado siku kidogo umalize la saba!
 
Back
Top Bottom