Huyu mwanaume ni zaidi ya kichomi, ungekuwa wewe ungefanyaje katika ndoa kama hii?

Kwanini haondoki?
Jibu linabaki kwa mtu binafsi, na sababu zinaweza kuwa ngumu sana. Ukweli ni kwamba, kuondoka kunaweza kuwa vigumu hata wakati unajua ni jambo sahihi. Wengi wetu tunaweza kujaribu kuondoka mara nyingi kabla ya kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya mwisho.

Sababu nyingine zinaweza kuwa, hapati ushirikiano/msaada kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki au hata serikali za mitaa.
Kushindwa kujikimu kifedha, hapa kama mumewe hampatii fedha ni ngumu kuweka akiba itakayomsaidia kuondoka pale nyumbani.

Pengine akiondoka mumewe atamnyanganya watoto wake, kama mama asingependa kuondoka kuwaacha watoto nyuma.

Akifikiria kazi atapata wapi? ni mda sasa tokea kamaliza chuo na hakupata work experience yoyote, itamchukua muda kupata kazi yenye kipato.

Na kama hajawahi kuishi mwenyewe ataanzia wapi kuanza kuishi mwenyewe na kujitegemea?
Pengine familia aliyokulia au kwenye jamii yake wanawake hawaruhusiwi kuachika/kuacha ndoa zao, anaogopa kuleta aibu na fedhea.

Sababu nyingine, anaweza kujihisi yeye ndio mwenye matatizo/makosa na anastahili hizo adhabu akaona sawa tu, kumbe sisi tulioko nje tunaona tofauti.

Kama mleta mada alivyosema, mwanamme akiwa nje ya nyumbani ni mcheshi huwezi dhania ndio anamnyanyasa mkewe, pengine akishampa vibano anambembeleza na kuhaidi hatorudia tena, hapa huyo dada anaona jamaa atabadilika anaona abakie kusubiria siku atakayobadilika.
Hizo siku anazoenda kwao halafu anarudi inawezekana mumewe anamtisha asiporudi atakuja mpiga zaidi ya mara ya mwisho, mdada anaona bora arudi nyumbani Kwake.

Mnisamehe kwa maelezo mengi ila unyanyasaji kwenye ndoa/mahusiano yapo sana hata wanaume wananyanyaswa.

Wale wanao pitia haya manyanyaso poleni sana.
 
Ndo maana ya uwepo wa vyombo vya dola. Kama yyy na nyingi nyote mlitambua uwepo wake mwanzo sasa mmesahau nn msongesheni mpaka atie adabu.
 
Acheni kufuatilia maisha ya watu.

Hivi wewe unajua uchungu wa kumlipia mtu Ada!? Na mapungufu ya huyo msichana mbona hamyasemi
 
Amefungwa na pingu au minyororo

Anawezaje kuwa weak kiasi hicho

Small minded people will never understand
 
Acheni kufuatilia maisha ya watu.

Hivi wewe unajua uchungu wa kumlipia mtu Ada!? Na mapungufu ya huyo msichana mbona hamyasemi

Kwahiyo kumlipia ndo umnyanyase kiasi hiko???
Wewe kama dadako/ mamako anafanyiwa hivi utajisikiaje??
 
Wanaume acheni huu ni Unyanyasaji uliotukuka. ..

Kuna mwanaume mmoja amemuharibia masomo binti alikua form 5,, ndugu wa binti wakachachamaa msomeshe na umuoe lasivo sheria inachukua mkondo wake. Hatukuelewiiiiii
Mwanaume akasema Ahaaa kusomeshaaa tu owkeyyyy kumuoaaa tu wazee sawa huyu mbona tayari ni mke wangu Aalelelelelelelele!
Binti katafutiwa chuo. Chuoni binti akikodolewa macho tu akirudi lazima ajibu yule aliekuwa anakuangalia Ninani?? mtaani yaleyale ulikua unaongea nayule mna biashara gani?! Atapigwa mpaka basi.

Binti kamaliza chuo mwanaume cheti kakichukua kakificha tena kakipeleka kwingine kabisa huko kwa ndugu wake mwanaume . Mwanaume hataki mke afanye kazi eti atamkimbia atamdharau as long as yeye ndo kamsomesha ataleta nyodo.
Mwanaume mwenyewe mwalimu tu mdada alisomea nursing ila hataki dada wawatu afanye kazi. Hapo dada anashinda Pori huko kumwagilia vitalu vya miti mara kulima kulingana na msimu. Hapohapo asubuhi shamba saa sita nyumbani kupika then urudi shamba nikukute huko nikitoka kazini Jioni ntakupitia

Chuo ilikua akifeli atapigwa mpaka basi finywa kwenye mapaja chapwa fimbo mpaka huruma.. Maneno kibao mara awamu hii ukifeli utanirudishia hela yangu boya wewe huna akili wala nini unafeli feli tu unamaliza pesa zangu bure.
Majuzi Kati ilikua usiku. Majirani wanashangaa wanasikia kilio kikubwa sana mwanamke analia. Ila hawasikii kelele labda za makofi yale ya paaa paaaa au kusema kusikia selekaseleka zozote hakunaaa. Ni kimyaa ila kilio cha machungu makali mmamaaaa mamaaa mungu wanguuuueeeeeee uwiiiiiiiiiiii uwiiiiiiiiiiii yoooooooooooooooooo!!
Asubuhi kuulizwa mwanamke ndo kuonesha wamama fulani watu mapajani bisibisi ilichomfanya. Siku nyingine alimpigisha magoti dada wawatu na mimba kubwaaa yani tumbo liko kuleeeee haijajalisha.

Acha sasa nyumbani akikosa analo. Wee mi nisingekupa ujauzito walaa nisingekuoa. Hata hivo nilipoteza hela zangu tu. Atapewa adhabu kama wanafunziiii. Anaeza ambiwa apige magoti hapo mume akienda aendako akirudi akukute ole wako unyanyuke... Ataambiwa ainame apitishe mikono nyuma ya miguu itokezee mbele na kushika masikio fimbo iko ndani jamani walimu vibaya hivooo!!'
Ole wako nikukute umekaa na sijui mwanamke jirani sijui mdudu gani hapa kwangu. Nitakunyonyoa. Hao watakuletea maneno ya umbea umbea make wanawake wa mtaani sio kabisa. Ni wambea wambea wanaofatilia yasiyowahusu ole wako nisikie upuuzi sijui nani Kaniambia hivi mara vile. Ukome.
Mwanamke kamuomba basi walau amfungulie hata ka biashara kadogo hapo nyumbani auze hata nyanya hakuna mume kagoma katakata.
wanaume acheni huu unyanyasaji. Haya siyo maisha kabisa. Sawa wanawake tunavumilia ila this is too much. Acheni wivu wa kijinga kwa ustawi na afya ya maisha yenu wenyewe. Mnapowavua chupi huwa mnawaza what next kweli???

Huwa mnajaribu hata kuwauliza kama siku ni salama kweli?? Wapo wanaume wanaotamani walau wake zao wangekua wafanyakazi kwa namna moja ama nyingine. Wewe unachezea.

Just imagine wewe kama ndugu yako anafanyiwa haya utajisikiaje??!
Ungekuwa wewe ndo huyo dada how would you react to such kind of a man???
Ewe mwanaume mwenye roho kama hii huwa unajisikiaje kumfanyia mtoto wa mwanaume mwezio hivi??

mahondaw wa Smart911
Hyio ndiyo faida ya mapenzi shuleni
 
Mpenzi mahondaw sijawahi na sikutegemea itatokea siku nitakupinga. Kwa leo naomba unisamehe NASEMA hii stori ya kijiweni. Nadhani utunzi huu umefundishwa na Smart911 na yeye usimuonee alifundishwa na Kasie.

Hahahaahhahahaahahahahaha
Sina hiko kipaji hata. Halafu nitunge story yanini?? Sio hobi yangu.

Halafu kadada ka watu ni kazuri kwakweli ila ndoivo matesooo tu
 
Dahhh! Huyo dada kashushwa na MUNGU,mm maneno na masimango yalinifanya niiage ndoa kila siku matusi tena mazito na ubinafsi vilinitosha,ndugu zake wachukue hatua la sivyo watamkosa ndugu yao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upande wa pili mbona hujatupa story yake ili tuweze kuhukumu kiuhalali, huoni kama story yako Ipo biased
Upande wa pili ni Mpole sana yani very decent hana makuu ila ndoivo anayofanyiwa na huyo mwanaume ndokama hayo
 
Mpenzi mahondaw sijawahi na sikutegemea itatokea siku nitakupinga. Kwa leo naomba unisamehe NASEMA hii stori ya kijiweni. Nadhani utunzi huu umefundishwa na Smart911 na yeye usimuonee alifundishwa na Kasie.

Hahahaahhahahaahahahahaha
Sina hiko kipaji hata. Halafu nitunge story yanini?? Sio hobi yangu.

Halafu kadada ka watu ni kazuri kwakweli ila ndoivo matesooo tu
 
Back
Top Bottom