Huyu mwanamke sio mwaminifu

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Hiki ni kisa cha mume na mke kuachana.

Watu hawa walifunga ndoa mapema. Mke alianza kumfahamu mume baada ya kuolewa tu,hakuwahi kukutana na mwanaume awaye yote.

Wamejenga familia pamoja,wamezaa watoto na kulea . Wameishi pamoja kama familia,wakiwakosoa majirani kwa kushindwa kuwa na familia imara nk.

Bahati mbaya sana,mwanamke alianza urafiki na mke wa jirani ambaye mume wake ana ukwasi.

Familia ya huyu mwanamke iliyumba baada ya mwanaume kutambua kuwa urafiki huo haukuwa wa dhati zaidi ya kutafutaiana wanaume. Basi,yule bwana alikasirika na hatimaye aliwafukuza watoto baada ya kupima DNA kuwa wamezaliwa nje ya ndoa na yule jamaa(mwenye mahusiano na mke wa jamaa)

Alimuonya mke wake kuwa,mke wangu achana urafiki na huyo mwanamke,maana nahisi una mahusiano na mwanaume karibu nyumba ya rafiki yako na mchakato mzima unafanywa na rafiki yako. Baadae yule jamaa aliamua kumfukuza mke wake kwa kuhisi kuwa anatoka nje ya ndoa.

Baada ya kusikia hivyo mwanamke alilia sana na kukimbilia kwa balozi kupata suluhu akidhani kuwa ameonewa na kunyimwa haki yake ya ndoa. Baada ya balozi kutoa uamuzi,yule mwanamke aliwaaga maswaiba zake rasmi ili kuwaandaa kisaikolojia kuwa anaondoka na achana na mume wake wa zamani.

Na baada siku moja,alikutwa na mume wake akifunga ndoa na mume aliyekuwa anakataa kuwa hana mahusiano naye. Huku watoto wakiwa wandaaji wa misosi,wapambaji nk

Je,kama huyu mwanamke alikataa kuwa hana mahusiano na huyu mwanaume,mbona kafunga ndoa naye? Mahusinao yalianza lini?

Je,kwa nini watoto wake waliohisiwa na mume wake kuwa inawezekana walizaliwa nje ya ndoa wako kwa jamaa huyu aliyefunga ndoa baada ya siku moja kuwaaga majirani?

Je,huyu mwanamke aliwezaje kumuacha mume wake wa kwanza aliyemzindua usichana wake? Sababu ni nini?. Je,sababu ya pesa au tamaa ya mwili?

Tusemezane.
 
Mkuu.......haya maswali unatuuliza sisi........?.......tunawafahamu hao watu........?.......au ni nani wetu labda.........?.....

na wewe.......nini kinakufanya usifuatilie maisha yako uhangaike na maisha ya watu........?......huoni huo ni umbea.........?..

Soree.......ila naona.......yote haya ungewauliza wahusika.......huenda wana majibu mazuri zaidi yetu..........
 
Duu fasihi imekula kwake, napenda kufikirisha kichwa namna hii. Mke kaolewa siku moja tu baada ya kuachika na kufukuzwa na mme bora
 
Huyu demi alikuwa "anobomolewa mipango" kwa siri na jamaa mmoja anafahamika kwa jina LA green network
 
Ndo ujue huyo mume hana sifa za kuwa mume bora ndo maana hata ‘alivyotishia kumuacha mke’, mke akaona afadhali amesaidiwa kutua ‘limzigo’
 
Ndo ujue huyo mume hana sifa za kuwa mume bora ndo maana hata ‘alivyotishia kumuacha mke’, mke akaona afadhali amesaidiwa kutua ‘limzigo’

ha ha ha,mwanamke ma...la..ya huyo,kwa nini aanze mahusiano na mwanaume kabla ya kuachana na aliyemuondolea usichana wake? Alipoamua kuolewa na mume huyo tena akiwa mdogo hakuliona hili la kuwa sio mwanaume bora? Ana jini mahaba.
 
si useme ni wewe mkeo kakuvuruga,sie hatuna ushauri zaidi ya pole,utapona tu.....afu wacha kuwa Mmbea..... ' 'kuchapiwa siri ya ndani'- Rich Mavoko LOL :biggrin:
 
si useme ni wewe mkeo kakuvuruga,sie hatuna ushauri zaidi ya pole,utapona tu.....afu wacha kuwa Mmbea..... ' 'kuchapiwa siri ya ndani'- Rich Mavoko LOL :biggrin:

Naona umeachwa. Jamaa katumia philosophy kuwakilisha message yake. Jiongeze utaelewa
 
Naona umeachwa. Jamaa katumia philosophy kuwakilisha message yake. Jiongeze utaelewa

duh thanks,:embarrassed1::embarrassed1::embarrassed1::embarrassed1::embarrassed1::embarrassed1::embarrassed1::embarrassed1::biggrin::biggrin::biggrin:
 
Yaani hapa mpaka div 5 za Mulugo waelewe kilichozungumzwa itakua mwaka umeisha
 
ha ha ha,mwanamke ma...la..ya huyo,kwa nini aanze mahusiano na mwanaume kabla ya kuachana na aliyemuondolea usichana wake? Alipoamua kuolewa na mume huyo tena akiwa mdogo hakuliona hili la kuwa sio mwanaume bora? Ana jini mahaba.

Kwani huyo mwanaume nae kawaondolea usichana wanawake wangapi? Ni wengi ‘kawatoa huo usichana’ na walimsaliti vile vile kinachomuuma sana kwa huyu ni nini? Atafute wengine ‘awatoe usichana watulie nae’.

Hapo tatizo kubwa mume hana vigezo na ‘wake anaowafukuza’ wakimkosoa ili awe sawa anakimbilia kuwafukuza sasa hii ndo imemuuma sana. Na wewe una undugu na ‘mume wake’? Maana unatetea sana
 
Back
Top Bottom