Huyu mwanamke nilimtongoza akanikataa. Alichonifanyia leo ni ishara ya kunipenda au amenichukulia kama rafiki?

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Si mpenzi wa wanawake waliojazia lakini kwa huyu nilikwama ana kila kitu yani anavutia kiukweli tulizoeana kiasi, nilimtongoza akanambia hawezi kabisa kuwa na mimi lakini hakunipa sababu alinisumbua sana.

Nilifuta namba yake maisha yakaendelea, kuna siku alinitafuta nikamjibu ovyo nilipomuuliza mwenzangu nani akajitambulisha huo ndio ulikuwa mwisho, tulipotezana kama miezi 4.

Leo nikiwa nimetoka kazini asubuhi nilikuwa shift ya usiku, sina hata pesa ya nauli nikadoea gari ya ofisi nirudi nyumbani nipumzike.

Nikiwa napita mahali flani nikaitwa na mtoto mkali sana amejiremba amependeza sana alivyovaa sasa acha kabisa kwa haraka sikumjua ikanibidi nisimamishe gari nishuke nikamjue ni nani huyu ananiita asubuhi yote hii.

Nikamkuta mrembo akitabasamu yupo kwenye biashara yake akiudumia wateja, anafanya biashara ya kuuza maziwa fresh, mtindi, chapati, maandazi na mikate, baada ya kusalimia akaniuliza maswali kadhaa yanahusu kazi na ninapokaa nikamjibu vizuri tu, akaniomba nimuungishe nikamjibu siku nyingine leo sina pesa yoyote hapa.

Akanambia basi kaa nikuudumie nakununulie mimi, nikaona hizi dharau nikapotezea kwa stori kadhaa akawa yupo busy nikajisahaulisha nikamuaga niondoke zangu, lakini yeye alisisitiza ni lazima ninywe chai angalau nipashe tumbo moto alafu niondoke vizuri.

Aisee! Ilinilazimu nilihudumiwa kama wateja wengine, wakati naendelea kunywa chai simu nimeweka mezani ikaingia SMS aliichukua simu aliisoma akaniangalia usoni akatabasamu akaendelea na kazi zake.

Nilipomaliza nilimshukuru nilimuaga niliondoka zangu,sasa nawaza hapa nikumbushie tena ombi langu nimiliki mtoto mzuri au amenichukulia kama rafiki tu na niwe mteja wake wa kawaida kwa siku zinazoendelea?

Mitazamo yenu ina maana kubwa sana hapa nitapitia mojamoja.
 
Usimtokee tena, maana ulishamtokea.... inatakiwa umalize kiutuuzima, mle kimasihara... endeleza urafiki wa karibu sana... siku mualike kwako, akija tu anza kutomasa piga mzigo...
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚kilichobaki ni kula kimasihara tu.
 
Kama ingekuwa ni mimi, hata sijisumbui kumkumbushia. Mimi nikisharusha ndoano ikachomolewa huwa sirudii tena hata iweje, siwezi kufanya kazi ile ile mara mbili.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ kwaiyo unafanyaje?
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ kwaiyo unafanyaje?
Kutesa kwa zamu, kama yeye alinitolea nje kwa kunijaribu ilhali ananielewa basi huwa ni nafasi yake ya kupambania penzi lake. Yaani huwa ni zamu yake kunivuta mimi kwake, nikiridhika fresh naruka nae na nisiporidhika basi ni suala ya Mungu kumtia yeye nguvu kuyakabili maumivu.
 
Kutesa kwa zamu, kama yeye alinitolea nje kwa kunijaribu ilhali ananielewa basi huwa ni nafasi yake ya kupambania penzi lake. Yaani huwa ni zamu yake kunivuta mimi kwake, nikiridhika fresh naruka nae na nisiporidhika basi ni suala ya Mungu kumtia yeye nguvu kuyakabili maumivu.
Nimekupa barabara
 
Back
Top Bottom