jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,687
- 1,780
Leo ni siku ya kuzaliwa binti yangu wa pekee (mpaka sasa) mpendwa sana!
Kwa mpaka sasa katika maisha yangu, huyu kiumbe ndio kitu kikubwa sana cha mafanikio yangu, na ndio sababu pekee inayonifanya napambana na ndio msingi wa furaha na mafanikio mengine.
Anatimiza miaka mitatu (3), nipo mimi na yeye tu!
Ilianza hivi.....!
Miaka minne iliyopita.
Kuna maeneo hapa mjini dar, unaweza kupata muono wa bahari ya hindi vizuri sana, hapo ndio utatambua utamu na uzuri wa bahari hiyo vilevile maisha.
Golden Tulip Hotel ni miongoni mwa maeneo hayo, najua yapo mengi na wewe unayajua!
Ilikuwa ni ratiba ya mimi na vijana wenzangu wa uswazi, kwamba kila mwisho wa mwezi tunachagua kiwanja kimoja ambapo tunaenda kubadili mandhari (kusafisha macho)
Wakati tupo hapa, eneo la "Maasai pub" stori za hapa na pale huku tuk-enjoy mawimbi yanavyopiga.... haikuchukua mda mwingi kabla sijajua kuwa huo muonekano wa bahari ya hindi na uzuri wake havikuwa na maana tena mbele ya huyu binti aliyepita hapa mbele yetu mda si mrefu.
Ni cashier. Toka nilivyomuona, akili ikawa ishanihama wala sikutaka kupoteza tena muda na kushangaa uzuri wa-view ya bahari ya hindi.
Wakati tunaondoka, nilimpitia pale counter nikamuuliza kama anaujua wimbo wa "All 4 One" unaitwa "As beatiful as You"
Akasema anaujua! Nikamwambia walimtungia yeye...... akacheka, nikachukua namba yake ya simu, mahusiano yakaanza.
Nyuma ya msichana mzuri sana, kuna tabia usiyoitarajia na itakushangaza (nzuri au mbaya)
Ilichukua miezi miwili nikawa nje ya Dar, then akawa ana mimba ya "Malaika"
Kwa bahati mbaya sana, mahusiano hayakudumu (stori nyingine) ila tulichoumba kilidumu.
Akajifungua "Baby girl".... Kabinti kangu ka kike my first born, raha sana!
Sababu sikuwa dar, hivyo baada ya kumuona tu nilirudi huko na mawasiliano ya mara kwa mara pia nilimuunganisha na familia yangu.
Baada ya miezi 6 ya umri wa mtoto, sikuamini nilivyomkuta mwanangu.... mtoto kama katoka Somalia ati ndio "kabemendwa" hivyo. Na alikuwa kishamuachisha ziwa.
Basi bibi yake hapa (Mama yangu) akasema inabidi mtoto abaki naye ili amshughurikie LISHE.
Inaonekana hiyo ndio ilikuwa ahueni ya huyo "shosti" maana toka siku hiyo binti (Mama mtoto) hadi leo hii wala hajatia pua yake hapa! Kamuacha mtoto.
Leo anatimiza miaka 3.
Mtoto lazima awe na mtu wa kumuita Mama, kadiri anavyokuwa shangazi yake mkubwa (dada yangu) ndio amemchagua kama Mama yake.
Tumeamua kumuacha tu aendelee hivyo sababu kwake aunt ndio anaziba pengo la Mama kimalezi, japo anachanganya na sisi tunavyomuita Bibi yake (Mama yetu) Mama, so na yeye anamwitaga Mama kwa kukosea.
Kiukweli sitamani Mama yake arudi kwa mda huu sababu nadhani itamchangnya zaidi mwanangu.
Nachukua wasaha huu kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa, Mungu ambariki sana na amzidishie hekima, akili na azidi kuwa mtoto mzuri.
Sanasana Mungu awabariki wakina Baba wote. (Kwa niaba yangu binafsi)
Pia awabariki wakina Mama wote (kwa niaba ya bibi yake na shangazi zake)
Mungu awabriki watoto wote wa Tanzania