Huyu Mwanamke hivi nimfanyeje jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu Mwanamke hivi nimfanyeje jamani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ab-Titchaz, Jul 13, 2009.

 1. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #1
  Jul 13, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wakuu wa maswala,

  kuna mwanamama nimeanza ufrendi naye lakini anakatabia ka kuingia
  kwenye simu yangu na kucheki nani kanipigia simu au nani kanitumia
  msg.

  nammaindi kinoma lakini hii tabia mimi sasa naona too much maana
  nimemkataza lakini bado hasikii. Leo asubuhi kaja na maswali ya
  kipuzi hata simuelewi.

  hebu nipeni wasia maana mwenzenu naona niachie ngazi mbele kwa
  mbele.

  P.S. Ni mmarekani

  Mwenzenu.
   
 2. fundiaminy

  fundiaminy JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 358
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  babu kweli wataka kuacha??sidhani.najua hako katabia kanakushinda,hiyo ni side a lakini ukigeuza tepu side b inacheza vizuri ama vp?
   
 3. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  simu zote kunakuwa na code ukiweka hiyo mtu hana uwezo wa kuifunguwa simu yako na kuona vilivyomo ndani sasa nashangaa kwa nini usichukuwe hatuwa kama hiyo ,hapo ndio atajuwa (ataelewa) kuwa hutaki achokonowe simu yako, kwani kugombana na mtu ni kutaka ukifanya hivyo itakuwa unamwambia (mueleza)indirect mtu kama huyo mara nyingi anakuwa na makubwa zaidi moyoni mwake yanayomsumbuwa zidi yako zaidi ya hilo la kuchokonowa simu .
   
 4. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sawa kabisa, kwa mfano kama simu ni aina ya Nokia kuna sehemu una-set KEYGUARD CODE ambayo hiyo utakuwa unaifahamu wewe tu. Au la sivyo mwone yeyote mwenye uzoefu na simu akusaidie
   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Kwani unampango naye wowote? If yes, unaficha nini? Au kicheche?
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Kama safari jiandae vizuri maana "Dalili za mvua mawingu", na kama mahusiano usambe hukuaswa "heri ya nusu shari kuliko shari kamili", kama ujenzi basi jua "usipoziba ufa utajenga ukuta" Fanya uamuzi wa maana mapema isije kuwa mambo ya "majuto mjukuu" . Pia yakhe kumbuka "ukicheza na mbwa atakufuata mpaka msikitini" na pia "mcheza na tope humrukia" kama kidume inabidi ujue "mchelea mwana kulia hulia yeye".

  Mimi nakwambia hivi kwa maana "adhabu ya kaburi aijuaye maiti" na "aisifiaye mvua imemnyea" ukiwa "bendera kufuata upepo" na kusema "chanda chema huvikwa pete" kwa kutaka ku "fuata nyuki ule asali" utajikuta butwaa kwa kujua "konzo ya maji haifumbatiki" baada ya kung'amua kwamba "lila na fila hazitangamani" na "mafahali wawili hawakai zizi moja"

  Lakini baada ya yote hayo, najua kuwa "kitanda nisokilala sikijui kunguniwe" na ujuwe kwamba"kila chombo na wimbile" na "kila ndege huruka na mbawa zake"
   
  Last edited: Jul 13, 2009
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  mkuu una familia...tunza ur family achana na kicheche hicho hata kama unalisaka karatasi.....
   
 8. b

  bnhai JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Inawezekana si KICHECHE labda yeye anamdanganya na binti wa watu yupo serious
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mpe straight kuwa haupendi tabia hiyo. Nimegundua watu wengi haswa mwanzoni mwa uhusiano wana penda kusugar coat kila kitu wasionekane wabaya. Bora umpe direct kuwa haupendi tabia hiyo na asipo change you will move on. Akiona anaweza kukupeleka kwenye jambo hili basi she will take advantage of you kila siku.
   
 10. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hebu twambie hii tabia ilianza lini?kama siku,miezi mingapi tangu uanze kum-mind!alot of times wen one is suspicious n insecure atataka kuinvestigate tumambo! Labda tutabia twako tumempush to that katabia. Tusimlaumu binti peke yake.i hop yeye pia anakumind kishenzi
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...duh, braza huyo ni G'friend au FBI unamfuga ndani :D? kwa uzoefu wangu, mwanamke kama huyo mukimuacha ndani anapekua masanduku na nyaraka zako zote, mbaya zaidi hata ukienda kukoga hachelewi kupitisha vidole ndani ya wallet!...

  Mbwage tu huyo bro, hafai! ...tabia haibadiliki, ukimchukua jumla jumla ujue siku za usoni utakuwa unapigwa body search...

  [​IMG]
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Samahani sana, hivi wewe ni Mwanamme? maana mimi siku zote nikiiona hiyo avatar yako najuwa u-mwanamke, samahani kama nimekosea. Au wewe ni mwanamke na huyo mwanamke wa ki merekani mna mahusiano ya jinsia moja? lesbians?
   
 13. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ufrendi wa aina gani?
   
 14. N

  Narumba Member

  #14
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mie siku zote huwa najua ni mwanamke huyu.
   
 15. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #15
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Narumba na Dar es salaam,

  Heshima mbele....mimi hapa ni mume tafadhali.
  Samahani kwa confusion ya avatar.

  One.
   
 16. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #16
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Asante kwa info hii and I will take up your advice.
   
 17. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #17
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mkuu,

  si kicheche bali ninampango naye..a future plan nd'o maana
  hii tabia yake inaniuzi kweli despite kumwambia I dont like it.
   
 18. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #18
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wewe bana eeeehhh!!!...haya basi.I''m planning my future
  with her...seriously!
   
 19. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #19
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  ...well said.Nuff respect to your words.
   
 20. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #20
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Si hivyo mkuu Yoyo,karatasi tayari ninalo.
  Huyu nd'o nataka nifanye kweli naye..hata kumleta Afrika.
  Lakini hii tabia inanitia wasiwasi.
   
Loading...