Huyu Mwana jf mwenzangu kama bado yupo hai or mahututi mwenyezi mungu akupiganie

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,145
11,191
Ni member ambae nilifahamiana nae miezi minne iliyopita na nlifahamiana nae kupitia jf doctor kuna kipindi nliweka ushuhuda wa acid reflux ilivyonisumbua na njia nlizotumia kupambana nazo basi ndio akanitafuta nimpe mawili matatu kwani nae alikuwa na tatizo kama hilo bas tukawa tunawasiliana mdogo mdogo

Baada ya mda kupita mwezi uliopita wa pili mwanzoni kama tarehe 4 nakumbuka,akanipigia sim ya gafla mda huo nlikuwa kwenye piki piki, nikashindwa kupokea baada ya kushuka akapiga tena akiwa ana jazba akitaka nimsaidie kumpa mawili matatu huhusu changamoto mpya aliyokuwa anapitia

Akaniambia kuwa anachangamoto ya upumuaji na anapitia kipindi kigumi sana ikiwemo baadhi ya sehem kuanzia mkononi kufa ganzi hadi mguuni na kifua kubana, akaniomba kama nna ufaham nimshauri afanye nini, kwa upande wangu yale yale tuliyokuwa tunaambiwa na wataalam wetu ndio nliyokuwa namuelekeza, kama kula vyakula vyenye vitami kwa wingi, mazoezi ,mchanganyo wetu ule wa nimri na nikamuhusia asisahau kusali mara kwa mar

Nikawa namjulia hali , kuanzia kipindi hicho akawa anasema haoni dalili ya kupona nikazidi kumpa moyo kuwa asikate tamaa , azidi kupambana na amuombe mungu

Lakini kitu kinachonipa wasi wasi ni kuanzia tarehe kumi na sita mwezi wa pili 16/02/2021 ndio mara ya mwisho kuwasiliana nae na kunijibu text ya mwisho saa kumi jioni
Screenshot_20210301-155812_Messages.jpg

hadi leo namba yake nikipiga inaita tu haipokelewi na si kawaida , kama yupo mahututi or something else sijui kwa kweli, laiti ningefahamiana na mtu mwingine wa karibu yake ningeweza kujua hali yake or nini kimemkuta

Nasikikita but kama bado yupo hai mola ampiganie na wote tumuombee

NOTE

Nilijaribu kutumia namba nyingine ya dada yangu ambayo sikuwahi kuitumia kuwasiliana nae alivyopiga haikupokelewa hadi leo..

Tumuombee...
 
Juzi nimempigia mmoja simu (sio member humu) ikapokelewa na kaka yake baada ya mazungumzo ananiambiaa wamemzika wiki ilipita.kwa kweli mpaka sasa naumia hadi najilaumu kwa nini ninepiga simu
 
Jaribu kutumia namba nyingine...., Hii dunia ishakuwa tambala bovu jambo ambalo limenifanya niache kuamini watu...., huenda labda ilikuwa ni long CON alivyoona hapo hakupati akaamua kupotezea..., Huenda hata asiwe mdada....

Sisemi kwamba this is the Case ila wengi wamelizwa na Nigerian Princes..., Hii dunia ishakuwa chaka; Alijesemea Marijani (Dunia Sasa Imani Imekwisha)
 
Jaribu kutumia namba nyingine...., Hii dunia kuwa tambala bovu imenifanya niache kuamini watu...., huenda labda ilikuwa ni long CON alivyoona hapo hakupati akaamua kupotezea..., Huenda hata asiwe mdada....

Sisemi kwamba this is the Case ila wengi wamelizwa na Nigerian Princes..., Hii dunia ishakuwa chaka; Alijesemea Marijani (Dunia Sasa Imani Imekwisha)
Nimetumia namba nyingine haipokelewi
 
Jaribu kutumia namba nyingine...., Hii dunia ishakuwa tambala bovu jambo ambalo limenifanya niache kuamini watu...., huenda labda ilikuwa ni long CON alivyoona hapo hakupati akaamua kupotezea..., Huenda hata asiwe mdada....

Sisemi kwamba this is the Case ila wengi wamelizwa na Nigerian Princes..., Hii dunia ishakuwa chaka; Alijesemea Marijani (Dunia Sasa Imani Imekwisha)
Duuh
 
Huu Mwandiko,nishaujua mkuu,kama ni yule dada mjanja mjanja hivi,kila jukwaa yupo,anajua kila kitu,kabadili majina zaidi ya Mara tatu! Basi elewa kua ndiyo tabia zake! Akipataga tu msaada,anakupotezea! Kama ndiyo yeye,now yupo Nyanda za juu kusini!
Boss hajawahi kuomba hela wala chochote ni mtu serious na alikuwa anaumwa kweli hata sauti yake tu ilikuwa inasikika kama mtu anaepumua kwa shida
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom