Uchaguzi 2020 Huyu mtu anaweza kuchukua hii nchi au anaweza kusababisha mambo yatakayosababisha mageuzi kutokea katika hii nchi

Kuna watu hutokea duniani kazi Yao siyo kuwa Viongozi wakubwa, mf Ndg Malema wa SA, ndug Prof Lumumba Kenya, Ndg Wine Uganda n.k

kazi Yao ni uanaharakati ndio inawafaa, na hata wa kwetu Yuko kwenye kundi hilohilo, kuchangamsha watawala, Uraisi ni kuwaonea. Watavurunda Asubuhi na mapema
 
Subiri kipenga kipulizwe ushindi siku zote ni uwanjani. Hii kaachiwa watu wamshangae ili wakati wa kampeni kusitokee wakutaka kwenda kwa ajili ya kumshangaa. Ndio maana ratiba imepita kwenye ngome zao zaidi.

CCM leo kutangaza majina ya wagombea wao kumeipoteza cdm, je kampeni zitapo anza na tingatinga arudi barabarani?
Kila mtu na mbabe wake! hakuna cha tingatinga wala nini. Airforce one iko angani sasa ni wakati wa kuyaambia hayo mauaji na mijizi ya kura yafanye fyoko yaone. Muwahi kwenda kurecharge pace maker mapema sababu hana ubavu hata wa mita mbili kwe huyo mnyama aliyeangani tayari kupiga!
 
Maybe ni mgeni kwenye siasa
Mrema alikuwa amepandikizwa tu so ccm walikuwa wanajua nn kinafanyika

Lowassa still alikuwa ni Mwanaccm Tena ambae 80% ya maisha yake katumikia Chama

Lisu hajawahi kabisa kuwa ccm
kila siku mambo yanabadilika ndugu,Kuna nyakati vijana hawakujishughilsha na kupiga kura lakini sasa wanapiga,Kuna nyakati hata kura zenyewe hazikuonekani lakini nyakati zinakuja kura zitaonekana,Vyombo vya ulinzi na usalama vilijitanabaisha kua sehemu ya chama tawala lakini nyakati zinakuja vitajitenga nao kwa kua wananchi wa wanaounga mkono chama tawala watakua sawa na wa vyama pinzani.Nyakati zinabadilika hakuna aliyetegemea Lissu kupata haya mapokezi kwa kua matusi kejeli na maaminisho kua ni msaliliti vilimwagwa lakini watu hawasikilizi tena Propaganda zisizo wasaidia.Nyakati zimefika watu hawatazami tena umaarufu wa chama wanatazama watu.Nyakati zimebadilika usikalili.
 
Sio kwa hali ilivyo sasa!

Watu wanaishi maisha magumu wewe unawatangazia ujenzi wa flyover japo zina manufaa lakini watakaokuelewa wachache. Miaka mitano bila kuongeza hata 100 kwenye mshahara? Watu wasio na vyeti unadhani wamesahau walivyofanyiwa unyama ausio?

Wafanyabiasharaa wamepewa makesi ya Uhujumu uchumi kila kukichaaa... Watu wamefunga Biasharaa kila konaa yani ukitembea mabarabarani siku hizi si ajabu kukuta frame 6 kati ya Kumi zilizokuwa zinafanya kazi zamani zimefungwaa. Mashirika na Bank mengi tu yanatambali ulimii.

THIS WONT BE A EASY BATTLE FOR CCM AT ALL..
Mwenyekiti wao jana kasema atafanya zaidi ya alivyofanya katika miaka yake mitano aliyomaliza,hiyo tafsiri yake ni moja tu ambapo kila mbinyo tulioshuhudiautaongezeka.Kama ni mbinyo kwa watumishi utaongezeka,kodi na kesi za uhujumu uchumi zitaongezeka,wakulima mbalimbali walioporwa mazao yao kutaongezeka,wafugaji walioteseka kwa miaka mitano ndiyo hivyo hivyo,wavuvi na nyavu zenu zilizoitwa haramu mtaendelea kupiga mbizi kupata samaki bila nyavu nk.
Hali inatisha,mkuu akisema atajenga sgr kwenda kusini ama kaskazini,akinunua bombadia mara 2 ya alizonunua,bado ugumu huu wa maisha tulioushuhudia utakuwa maradufu huku tukiendelea kukopa na kukuza deni la Taifa kwa kisingizio cha kukopesheka.
Fikiria utakuwa na hali gani wewe mnyonge?Tuepuke ushabiki bila kufikiria yajayo.
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.

Mkuu nimesoma points zako, nani naomba kuweka neno.
kwanza kabisaaa toka mfumo wa vyama vingi uanze Lisu ndiye mgombea mpinzani pekee (asiye na asili ya ccm kabisaa), mwenye uwezo wa kujenga hoja, uelewa mkubwa wa mambo , anaejua kukera bila kuvunja sheria ili ujaesumu.

Unaposema lowasa na mrema hawa hakuwa wapinzani kwa mujibu wa fikra zangu kwa sababu baada ya kukosa nafasi ccm wakaenda kujaribu kutimiza ndoto zao upande wa pili...but kifikra & itikadi walikuwa wana ccm.
Pili unasema ccm imejaa vijana, ebu angalia hao vijana ni wale ambao baba au mama zao ni mazao ya ccm au wana historia ndefu ndani ya ccm. kurithishana.
Kwachadema imewekeza vyuoni na ina pic direct na kuwapa vijana fursa ya kuwa wawakilishi. eg. silinde, lijualikali, wenje, pambalu, nasari. Hata kama baadae wanajifanya kununulika lakini historia inabaki palepale.
 
Huyu ndugu anaweza kuchukua nchi moja kwa moja kupitia sanduku la kura tukiwa na uchaguzi ulio huru na wa haki, lakini pia anaweza kusababisha mambo yatayosababisha mageuzi yatokee katika nchi yetu.

Wanasiasa wa aina hii husababisha katiba na sheria za nchi katika mataifa mbalimbali duniani kubadilishwa ili kua-accomodate wapinzani ndani ya serikali kutokana na kuwa na uungwaji mokono mkubwa wa wananchi na zaidi kuwa na misimamo isiyoyumba ambayo hulazimisha watawla kufanya nao mazungumzo ili mambo yaende kama ilivyotokea huko Zanzibar kwa Maalim Seif kupewa wadhifa wa kuwa makamu wa kwanza wa Raisi mwaka 2015 kama sikosei.

Baada ya Zanzibar,sasa inaweza kuwa ni zamu ya Bara kufanya mabadiliko ya katiba kuwezesha wapinzani kuwa ni sehemu ya serikali ingawa si jambo rahisi kutokea na hata likitoea, basi huwa na mchakato mrefu lakini mwisho wa siku mambo hutimia ingawa inluence ya taasisi za kimataifa na mataifa makubwa huwa pia ni sehemu ya kufanikisha mambo haya hasa pale upinzani unapokuwa na nguvu na kusimama imara.

Lissu akijiridhisha kupata kura nyingi za kumuwezesha kushinda,basi lolote kati ya hayo linaweza kutokea maana najua hatotaka kurudi nyuma zaidi ya kupigania haki yake na hapo ndio inaweza kuwa mwanzo wa haya niyasemayo kutimia bila kujali itachukua muda gani au kutakuwa na ugumu kiasi gani.

Matamshi yake ya leo kuhusu yeye kupigwa risasi na aliowatuhumu/aliemtuhumu,ni ushahidi wa jinsi gani alivyojasiri wa kusema au kutenda mambo yasiyotegemewa na wengi kwani leo kaenda mbali zaidi katika kutoa tuhuma za waliompiga risasi.

kwa kweli huyu jamaa ni jasiri kupita maelezo.
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.
Ww ni binadamu muongo. Mtu yoyote asiyetaka Tl ashinde hawezi kuwa muongo wa kiwango chako Bali yule tu anayetaka kuhadaa ili ashinde.
 
Huyu ndugu anaweza kuchukua nchi moja kwa moja kupitia sanduku la kura tukiwa na uchaguzi ulio huru na wa haki, lakini pia anaweza kusababisha mambo yatayosababisha mageuzi yatokee katika nchi yetu.

Wanasiasa wa aina hii husababisha katiba na sheria za nchi katika mataifa mbalimbali duniani kubadilishwa ili kua-accomodate wapinzani ndani ya serikali kutokana na kuwa na uungwaji mokono mkubwa wa wananchi na zaidi kuwa na misimamo isiyoyumba ambayo hulazimisha watawla kufanya nao mazungumzo ili mambo yaende kama ilivyotokea huko Zanzibar kwa Maalim Seif kupewa wadhifa wa kuwa makamu wa kwanza wa Raisi mwaka 2015 kama sikosei.

Baada ya Zanzibar,sasa inaweza kuwa ni zamu ya Bara kufanya mabadiliko ya katiba kuwezesha wapinzani kuwa ni sehemu ya serikali ingawa si jambo rahisi kutokea na hata likitoea, basi huwa na mchakato mrefu lakini mwisho wa siku mambo hutimia ingawa inluence ya taasisi za kimataifa na mataifa makubwa huwa pia ni sehemu ya kufanikisha mambo haya hasa pale upinzani unapokuwa na nguvu na kusimama imara.

Lissu akijiridhisha kupata kura nyingi za kumuwezesha kushinda,basi lolote kati ya hayo linaweza kutokea maana najua hatotaka kurudi nyuma zaidi ya kupigania haki yake na hapo ndio inaweza kuwa mwanzo wa haya niyasemayo kutimia bila kujali itachukua muda gani au kutakuwa na ugumu kiasi gani.

Matamshi yake ya leo kuhusu yeye kupigwa risasi na aliowatuhumu/aliemtuhumu,ni ushahidi wa jinsi gani alivyojasiri wa kusema au kutenda mambo yasiyotegemewa na wengi kwani leo kaenda mbali zaidi katika kutoa tuhuma za waliompiga risasi.

Mungu alipanga mwisho wa CCM kwa namna ambayo akili ya mwanadamu haiwezi kuelewa kirahisi. Aliamua aje mtu mgeni kwenye chama (Magufuli) ambaye atawanyang'anya chama wakongwe (Makamba, Kinana, Kikwete, Membe nk) na kuingiza watu wake wapya (Bashiru, Makonda, Polepole).

Hawa wapya kwa namna yake watakivuruga chama na misingi yake kwa maagizo yake Mafufuli. Wataleta chuki na maovu kama utekaji (Mo Dewji, Roma ) na uuaaji (Ben Sanane, Azory Gwanda nk).

Halafu watamshambulia mmoja wa viongozi wa upinzani (Lissu) kwa risasi za bunduki ya vita lakini mtu huyo hatokufa. Nchi nzima itashangaa namna mtu huyo alivyoshambuliwa, kunyimwa matibabu, kunyang'anywa mshahara kisha kufukuzwa ubunge.

Wanaposhangaa hayo na kumhurumia ndiyo watataka awe Rais wao wa 2020-25. Mungu ana sababu kwa kila jambo. Mwisho wa CCM ni mwaka huu. Alilopanga Mungu Binadamu hawezi kubadilisha. Hata kama NEC itaiba kura na kumtangaza Maguduli, nguvu ya umma itamtoa tu Ikulu. Wananchi wamechoka maonezi, dhuluma, ukandamizaji, na ubaguzi wa maendeleo.

Enzi ya CCM imekwisha
 
Kuna kauli naitoa humu kila siku na leo narudia, CCM haitapata kura za watumishi wa umma isipokuwa polisi na jeshi nadhan, CCM haitapata kura za wafanya biashara, CCM haitapata kura za baadhi ya wakulima, CCM haitapata kura za vijana walioko mitaani bila kujua kesho yao ikoje, CCM haitapata kura za wanafunzi wa vyuo vikuu, ila maajabu ni kwamba CCM itashinda kwa asilimia kubwa sana na uchaguzi utapita na mambo yataendelea kama kawaida, watanzania wa kuumia watendelea kuumia na wale wa kula keki ya taifa wataendelea kula tu.
Hilo liko wazi
 
Subiri kipenga kipulizwe ushindi siku zote ni uwanjani. Hii kaachiwa watu wamshangae ili wakati wa kampeni kusitokee wakutaka kwenda kwa ajili ya kumshangaa. Ndio maana ratiba imepita kwenye ngome zao zaidi.

CCM leo kutangaza majina ya wagombea wao kumeipoteza cdm, je kampeni zitapo anza na tingatinga arudi barabarani?
Ila kile nimeshuhudia leo Kyela baada ya kutajwa mgombea. Nderemo vifijo bodaboda kelele mji kushangilia.
 
Nimeshasema huko nyuma ashinde asishinde siasa za Tanzania hazitakuwa kama tulivyo zoea. Likizo yao ya miaka mitatu imekwisha. Na kwa sababu CCM ni sauti moja tunahitaji mtu wa kumwambia mfalme yuko uchi ikibidi na hilo CCM hawaliwezi.
Jana nilimsikia mjumbe wa NEC ya CCM akimsifia JPM kuwa "alimuweka kando mtoto wa dada yake baada ya kumuona hatoshi". Kwake hiyo ni sifa ya kiongozi wake, kwangu mmi huo ni ushahidi kuwa kule kuna sauti moja tu.
 
Bila CCM mda huu Tanzania ingekuwa kwenye G5 na kuwa na kura ya veto, Tanzania ni level ya America, German, England, China, Urusi na mataifa mengine tajiri kutokana na Tanzania kumiliki rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, pesa nyingi inapotelea kwenye kudidimiza demokrasia badala ya maendeleo.
Both ways,Nyerere alifunga multiparty system pia akafunga au akapiga marufu kuibiwa mali zetu na makampuni ya kigeni.
Kaja Ben Mkapa tukiwa na multiparty akidhani kuruhusu makampuni ya kigeni yawekeze kwetu itakuwa jambo zuri sana.Hakujua kati yao wamo ruthless investors wasiotaka tubaki na chochote na ndio wengi walikuja kwetu.
Lakini kuja kwa mjomba Magufuli kapinduwa meza kawafungisha virago au wakubali tugawane kwa usawa.
Bila kuwa mkaidi utavuna mabuwa.
 
Tume imeshawatangaza kwamba wamepita bila kupingwa?

Kwa maoni yangu nadhani Chadema wangetafuta sababu yoyote ile, wasusie huu uchaguzi ili kuepuka aibu itakayowakuta. Ikiwezekana hata wampige Lissu jiwe la kichwa lakini lisimuue wala kumjeruhi. Maana jeshi lililotangazwa leo, sioni ni Jimbo gani wanaweza kuchukua. Kila Jimbo amepelekwa mtu sahihi anaetakiwa na kukubalika na wananchi. Cha kufurahisha zaidi, asilimia kubwa ni vijana wachapa kazi.
Ona mawazo ya think tank wa lumumba , mataga mwaka mtaongea yote , mtatapika ndoano.
 
Hakuna mgombea anayeweza kufikisha 70% uchaguzi wa mwaka huu. Itakuwa ni close tie, 50/50; 52/48; 54/46!
CCM vs Upinzani kiujumla.
Serikali ya Umoja wa kitaifa loading...
Umoja wa kitaifa kwa mgombea yopi wa urais? Kwa wabunge wapi? Nipe idadi ya wabunge wa CDM watakao shinda .
 
Asante sana huo ni muono kipofu wako. Umekataa ukweli na ukweli unauona ni uwongo. Tusubiri matokeo.
Matokeo yoyote hayatahalalisha uongo wako, Jpm atakuwa raisi uwezekano ni mkubwa sana ndio. 97% ni raisi ila haitamaanisha kuwa ulisema kweli.
 
Back
Top Bottom