Uchaguzi 2020 Huyu mtu anaweza kuchukua hii nchi au anaweza kusababisha mambo yatakayosababisha mageuzi kutokea katika hii nchi

Maybe ni mgeni kwenye siasa
Mrema alikuwa amepandikizwa tu so ccm walikuwa wanajua nn kinafanyika

Lowassa still alikuwa ni Mwanaccm Tena ambae 80% ya maisha yake katumikia Chama

Lisu hajawahi kabisa kuwa ccm
Toka vyama vingi vianze, huyu ndiyo mgombea halisi wa upinzani. Yeye ni no compromise, mambo ya kumleta TB Joshua kwa huyu wasahau.
Keshasema hamuachii Mungu!
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM, na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.
sikubaliani na hili!
 
Salary Slip,

Naona sasa umeanza kupima kima Cha maji na kuona kirefu.. hapa umeanza kuchambua kiutu uzima tofauti na zamani uliamini Lissu tu ndie atashida Urais.

Lissu Sanasana ataendelea kuumia tu kuona JPM akishinda kwa asimilia 70%.
Hakuna mgombea anayeweza kufikisha 70% uchaguzi wa mwaka huu. Itakuwa ni close tie, 50/50; 52/48; 54/46!
CCM vs Upinzani kiujumla.
Serikali ya Umoja wa kitaifa loading...
 
Kibao kimegeuka. Subiri utaona. Mpaka sasa hivi kuna majimbo 10 chadema wameshashinda kabla ya uchaguzi
Tume imeshawatangaza kwamba wamepita bila kupingwa?

Kwa maoni yangu nadhani Chadema wangetafuta sababu yoyote ile, wasusie huu uchaguzi ili kuepuka aibu itakayowakuta. Ikiwezekana hata wampige Lissu jiwe la kichwa lakini lisimuue wala kumjeruhi. Maana jeshi lililotangazwa leo, sioni ni Jimbo gani wanaweza kuchukua. Kila Jimbo amepelekwa mtu sahihi anaetakiwa na kukubalika na wananchi. Cha kufurahisha zaidi, asilimia kubwa ni vijana wachapa kazi.
 
Wewe hapo ulipo ni kuweweseka tu. Unakumbuka ulimjibu nini Nyani Ngabu alivyotabiri kurejea kwa Lissu? Sasa imetimia. Ulisema hataweza hata kunyanyuka kama atapona: sasa amepona na amenyanyuka. Ukasema, akiweza akinyanyuka hataweza kutembea. Sasa ni wewe au ma.ma yako anambeba mgongoni kwasababu hawezi kutembea? Wewe kwa yale maneno yako miaka 3 iliyopita, ulikuwa na uhakika na uliyoyaongea kwasababu lazima ulikuwa sehemu ya wale waoga ambao walishindwa kulenga shabaha.

Sasa muujiza umetendeka unaanza kuweweseka. Karma is real.
Kumbe jamaa aliongea upuuzi sana kiasi hicho???
 
Tutawapigia kura kama kawaida. Kwasababu, tunajua fedha za kuongeza mishahara ndo zimejenga zahanati na vituo vya afya ambavyo wazee wetu, wake zetu na watoto wetu ndo wanapokwenda kupewa huduma kila wanapougua.

Tunajua pia fedha za kuongezea mishahara ndo zinatumika kugharamia Elimu Bure ili watoto wetu waweze kupata elimu bila vikwazo.

Tunajua pia fedha za kuongeza mishahara ndo zimejenga Miundombinu ya barabara katika kila kona ya nchi hii ambazo hata Tundu Lissu anazitumia sasa hivi kwenda kuomba wadhamini na kufanya mikutano ya hadhara.

Tunajua pia fedha za kuongeza mishahara ndo zimenunua ndege, kujenga SGR, Bwawa la Umeme, Flyover ambavyo hivi vyote vitakuza uchumi na kutuwezesha kuongezewa mishahara mara dufu huko baadae kuliko tungeongezewa sasa hivi.

Kwa maana hiyo, tumekubali nyongeza ya mishahara yetu itumike kuwanufaisha watanzania wote na siyo sisi kundi la watu wachache. Tunakataa UBINAFSI tunatukuza UZALENDO kwa nchi yetu.
Acha kuropoka mwalimu halisi hawezi kuongea hivyo.ungejua maumivu wanayopitia waajiriwa hata usingethubutu kusema chochote.
 
Acha kuropoka mwalimu halisi hawezi kuongea hivyo.ungejua maumivu wanayopitia waajiriwa hata usingethubutu kusema chochote.
Ungejua pia maumivu waliyokua wanapitia kina mama wajawazito na watoto walipokua wanakosa huduma za Afya mpaka wengine kupoteza uhai, watoto waliokua wanakosa elimu kisa Ada, wakulima walishindwa kusafirisha mazao yao kwenda kuuza kisa hakuna barabara. Yote haya ungeyafikiria, usingekimbilia kuja kuropoka usiku wote huu.
 
Hivi wee jamaa hata una Wazazi kweli? Na kama unao huwa hata una muda wa kuwajulia angalau hali? Slow down man, hii Dunia haijaanza leo, utakuja kuishia kujiua siku moja kama ukiendelea hivyo kuabudu takataka, ...
unamsema nani sasa, mleta mada au?
 
Ungejua pia maumivu waliyokua wanapitia kina mama wajawazito na watoto walipokua wanakosa huduma za Afya mpaka wengine kupoteza uhai, watoto waliokua wanakosa elimu kisa Ada, wakulima walishindwa kusafirisha mazao yao kwenda kuuza kisa hakuna barabara. Yote haya ungeyafikiria, usingekimbilia kuja kuropoka usiku wote huu.
Maumivu ya watu wote uliowataja yanatia huruma
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM, na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.
Huyu muacha aongee haijui CCM vizuri.
 
Bila CCM mda huu Tanzania ingekuwa kwenye G5 na kuwa na kura ya veto, Tanzania ni level ya America, German, England, China, Urusi na mataifa mengine tajiri kutokana na Tanzania kumiliki rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani , pesa nyingi inapotelea kwenye kudidimiza demokrasia badala ya maendeleo
Hao chadema unaowategemea wakupeleke kwenye G5 hawana ata office yenye thamani ya 30m kwa zaidi ya 20yrs what a shame!
 
Lowassa na Mrema ndio walio wahi kuitikisa CCM, na haito tokea tena. CCM iko very dynamics inabadilika sana kufuatana na hali halisi na mapenzi ya wananchi kwa wakati huo.

2020 Utaona asilimia 80% ya wabunge CCM ni chini ya miaka orobaini. Upinzani kujivunia vijana haipo tena, wazee ndio wamesheheni upinzani.
1995 then 2015 na Leo 2020baDo unaamini mazingira yanafanana
 
Nina umri wa kutosha wakati huo tayari nimemaliza degree yangu ya pili na nikiwa na akili timamu japo bado kijana sana. (ukipenda nitakwambia CV yangu utaipata wapi publicly)

Umri alio nao Lissu leo ndio umri aliokuwa nao Mrema, wakati huo akiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani (1995) na anaeheshimika sana.

Upinzani nchi hii ni mpaka CCM ipasuke vipande. Kila ilipo pasuka uchaguzi kwao ulikuwa mgumu. Vinginevyo ni vichekesho tuu.

Kwa kulitumia jeshi kumlazimisha Jecha ndio CCM bado haijakatika vipande ??

Hizo degree zako ulizichukulia Kivukoni ??
 
Bad uko kwenye vitu kama Jpm mtaji wa siasa ni watu na hoja za wakati husband
Ndo mnavyodanganyana kuwa mtaji wa siasa ni watu na sio vitu, watanzania wameshachoka na maneno waliyokuwa wanapewa zaman wanataka vitu vinavyoonekana na kwa vitendo bro.
 
Kuna kauli naitoa humu kila siku na leo narudia, CCM haitapata kura za watumishi wa umma isipokuwa polisi na jeshi nadhan, CCM haitapata kura za wafanya biashara, CCM haitapata kura za baadhi ya wakulima, CCM haitapata kura za vijana walioko mitaani bila kujua kesho yao ikoje, CCM haitapata kura za wanafunzi wa vyuo vikuu, ila maajabu ni kwamba CCM itashinda kwa asilimia kubwa sana na uchaguzi utapita na mambo yataendelea kama kawaida, watanzania wa kuumia watendelea kuumia na wale wa kula keki ya taifa wataendelea kula tu.
 
Back
Top Bottom