:::Huyu Mtoto Aende Akasome Chuo Kikuu Kabisa:::

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la
nne kwani hili la3 halinifai.
Mwalimu: Kwa nini unasema hivo?
Mtoto: Nina akili...
Basi mwalimu kamueleza mkuu wa shule na
mkuu kaitisha interview kwa dogo.
Maswali ni haya....
Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20
tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki
mangapi?
Dogo: Yatabaki 19.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo
kwenye friji.
Doo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha
unafunga.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani
kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo
ulemuweka kisha unafunga friji.
Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa
kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro
mmoja. Ni nani na kwa nini?
Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka
kwenye friji.
Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga
na mamba na viboko wakali, aliwezaje?
Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao
walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa
simba.
Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto,
baadae alikufa. Unadhani kwa nini?
Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa
kwenye ndege na kutupa chini.
Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo
kikuu....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom