Huyu Mpumbavu anaweza akasababisha maafa makubwa sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu Mpumbavu anaweza akasababisha maafa makubwa sana

Discussion in 'Jamii Photos' started by BAK, Jun 16, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  <TABLE cellSpacing=0 cellPadding=0 width="100%" border=0><TBODY><TR><TD vAlign=top align=middle>[​IMG]</TD></TR><TR><TD class=kaziBody vAlign=top align=left>Kijana huyu akihatarisha maisha yake kwa kukinga mafuta kutoka kwenye tenki la gari hili likiwa linatembea katika barabara ya Nyerere Dar es Salaam jana. (Picha na Yusuf Badi).</TD></TR></TBODY></TABLE>
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hayo ni mabaki ya mafuta, hilo tank limetoka mkoani/congo/zambia/malawi etc na linakuja Dar kujaza mafuta, hivyo kwenye tank huwa kuna mafuta mabaki kidogo sana NDIO MAANA HATA MADEREVA huwa wanawaruhusu tu na wanawaacha tu wafanya wanachofanya kwasababu hapo wanakuwa wako safarini kwenda kujaza mafuta. ukisimama pale ubungoubungo ni kitu cha kawaida,madereva wanawaona, wanawaacha tu etc.

  HOWEVER, ni hatari sana na inatakiwa kukemewa kwasababu mafuta kidogo tu yakilipuka kama ndo mko pale kwenye foleni mataa ya ubungoubungo walioko kwenye foleni wote inakuwa mshikemshike. hii kitu inafanyika sana pale mataa ya ubungoubungo.
   
 3. k

  kaiya Member

  #3
  Jun 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu mchezo hawa vijana wameshauzoea na wakati mwingine wananyonya mafuta askari wa barabarani wapo wanawaangalia tu. madereva na makondakta wao pia wanawaona hawakemei. barabara ya mandela ndio hasa kunakofanyika mchezo huu maeneo ya buguruni. siku ikitokea maafa (mungu aepushe) sijui itakuwaje na msongamano wetu huu wa barabarani.
   
 4. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2010
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mwenye jukumu la kuwazuia si dereva wala konda, aidha hata uwezo wa kuwazuia hawana. jiulize ni wewe ukiwa barabarani kwenye foleni hawa watu wanaparamia gari lako na mifuko ya rambo utafanya nini??, hata ukisimama na kuwafukuza , ikiwa upo kwenye foleni uingiapo ndani ya gari bado watasogelea na kuendelea na wanachokifanya. chaajabu wanapofanya hivyo wanakuwa hata hawana ukahika na aina ya mafuta yaliyomo ndani. ni jambo la hatari sana ki usalama , pia hata kwa ubora wa mafuta kwani mwisho hayo mafuta wanayokusanya kwa rambo huishia kuchanganywa na na kutumiwa kwenye vyombo vya watu

  dola ndiyo yenye jukumu la mwisho la kuwalinda wazalishaji , walipa kodi na wananchi kwa ujumla. hivyo kwa lugha ya kawaida , jiji wanatakiwa walione hili tatizo, kwa kushirikia na na vyombo vingine kama polisi na hatimaye kuweka utaratibu wa kuzuia haya mambo.
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Watu washasahau yaliotokea Mbeya (njia ya kwenda Tukuyu) miaka ile
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jun 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Tusiwalaumu sana wapo katika kutafuta riziki zao.
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  ....kwenye down flani hivi kabla ya Kiwira pale....weeee!!!!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  washangae wanaonunua mafuta ya kwenye rambo!!!!
  nafahamu wanunuaji wa mafuta hayo ni wenye pikapu za kubeba mizigo, zile zilochoka mbaya!!
  Na bongo kukishakuwa na mnunuaji, basi biashara haiwezi kwisha hiyo!!
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  maisha bora kwa kila mtafuta ugali,
   
 10. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Unanikumbusha biashara ya machangu doa kinondoni enzi za Yusufu Makamba akiwa Mkuu wa mkoa walimwambia mzee nenda ukalae tu hii biashara haiwezi kufa maana wateja wapo wengi tena wengine ni vibosile kabisa...!! Maisha bora kwa kila Mtanzania.:hail::hail::hail::hungry:

   
 11. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #11
  Jun 17, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaaazi kwelikweli, maana hata kule Arabuni wapo hawa, ngoja tuone Lukuwi aah Lukuvi baada ya Ardhi Kinondoni atahamia huku labda!!!
   
 12. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hawa wasinge hatarisha maisha yao namna hii kama wasingekuwa na wateja (wapenda dezo) tayari tayari
   
 13. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Is this not a crimal act? Hawa TigO wao wanashughulika na watanuaji tu au??
   
 14. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Ubungoubungo:picha iyo uwa naipenda sana (ambayo ni avatar yako)

  ila maisha ndo yanafanya mtu ufanye vitu kama ivi ili uishi,kuliko kuwa jambazi!!
  ss wafenyeje?maisha ni kasheshe jamani
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mungu wangu!
  Wengine tunasema safety is our number one value wenzetu .....:embarrassed:
   
 16. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama sijakosea eneo lenyewe lilikuwa linaitwa Kijiji cha Edweli, na mwaka jana tukio kama hilo lilijirudia Kenya...utafutaji riziki wa namna hii ni hatari si wa kuchekewa hata kidogo.
   
 17. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ni hatari sana lakini hapa bongo ni kama imehalalishwa vile, kuna siku nilishuhudia jamaa akijichukulia mafuta kwa staili hiyo hiyo huku nyuma ya hilo lori kuna gari ya polisi ambao walikuwa wakimwangalia na kucheka tu.
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ajira milioni moja za kwenye ilani ya uchaguzi, ndo maana polisi wanaangalia na hawasemi kitu, bado kidogo watatungiwa sheria kuhalalisha
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  Mkuu X-PASTER lakini kutafuta riziki yake kunaweza kabisa kusababisha maafa makubwa kwa mamia kama siyo maelfu ya Watanzania. Fikiria jinsi Dar kulivyo na foleni kubwa za magari halafu hili gari lilipuke na huku lina mzigo mkubwa wa mafuta si kitakuwa kilio cha kusaga meno? Si vibaya kutafuta riziki lakini tufanye hivyo katika njia ambazo hazihatarishi maisha ya Watanzania wenzetu.
   
 20. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  jamani...this is too much...
   
Loading...